Lulu za Mkondoni : Utukufu wa Akili na stahiki yake

Kisai

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
28,074
28,184
Siandiki kuhusu falsafa na wenyewe kuwarejea, tena siandiki kuhusu mzaha ili wale kuwatania, bali naandika kuhusu amana kwa watu wake kuirejesha,tena nasisitiza naandika kuhusu neema ya akili popote kuizungumzia.

Akili kwa ufupi sana na kwa lugha nyepesi ni kizuizi kinachomfanya mtu asitumbukie katika makosa, na kujua lipi baya na lipi zuri, lipi linafaa na lipi halifai, kuiongelea akili kuna hitaji muda mwingi na marejeo tele. Lakini leo nawakumbusha jamaa, watoto na wavyele juu ya utukufu wa akili, kwa kumili katika maswali mawili ya msingi sana, na kwa kutumia akili ipasavyo utaona hazina iliyofichika.

Fikiri kwa makini na utafakari, juu ya maswali haya mawili hapa chini, kisha utuonyeshe ulichokiona.

1. Kwanini watu wanaomba uongozi, yaani wanaomba kupewa uongozi na wawe viongozi ? Je hili lina faa na ni jambo la busara au kinyume chake?

2. Je, kwanini watu wanachagua viongozi ? Ni nani mwenye sifa madhubuti na stahiki ya kuchagua kiongozi ?
 
Uongozi! Inategemea na aina gani ya uongozi.

Lakini kama ni uongozi wa mamlaka za kiserikali ama kijamii, basi uongozi ni kwa ajili ya kutengeneza haiba na kipato.

Kuchagua maana yake ni kusimama na kuunga mkono upande wa mchaguliwa ambao ni kama kumshabikia tu, aidha kutokana na sifa zake njema ama mtu anavyohisi kumpenda mhusika na hakuna faida ya moja kwa moja itokanayo na kumchagua mtu ili awe kiongozi.
 
Uongozi! Inategemea na aina gani ya uongozi.

Lakini kama ni uongozi wa mamlaka za kiserikali ama kijamii, basi uongozi ni kwa ajili ya kutengeneza haiba na kipato.

Kuchagua maana yake ni kusimama na kuunga mkono upande wa mchaguliwa ambao ni kama kumshabikia tu, aidha kutokana na sifa zake njema ama mtu anavyohisi kumpenda mhusika na hakuna faida ya moja kwa moja itokanayo na kumchagua mtu ili awe kiongozi.
Je, kila mtu anauwezo wa kuona sifa nja za mtu ?
 
Sasa ni ipi njia sahihi na lipi linafaa na ni lipi la kuishi nalo ? Ili kuwaondoa mashabiki na wanao faa ?
Si rahisi kuigeuza jamii kirahisi namna hiyo!

Wapenda vyeo na wasaka tonge, wanategemea sana mashabiki na mambumbumbu ku servive!

Sielewi bado ni mfumo gani ufanyike kuweza kubalansi ama kumaliza haya mambo.
 
Siandiki kuhusu falsafa na wenyewe kuwarejea, tena siandiki kuhusu mzaha ili wale kuwatania, bali naandika kuhusu amana kwa watu wake kuirejesha,tena nasisitiza naandika kuhusu neema ya akili popote kuizungumzia...
Aisee chalii yangu kwenye heading unamaanisha lulu za nini? Ama za zizini?
 
Akili Ni Nini?
Nini tofauti ya busara, hekima, akili na maarifa?
Busara ni kufanya jambo kwa uzuri, ni kama hekima tu ila busara imeambatana sana na upole.

Hekima ni kuweka kitu mahala pake.

Akili nimeigusia ila kwa ziada ni kuwa tamko akili kiasili ni tqmko la kiarabu na akili iliitwa akili kwa kuangalia kazi yake, kwa waarabu kilq kinacho funga kitu fulani na kuzuia kitu hicho kisitoke mahala pake kiliitwa Akili, mfano Ngamia anapofungwa kwa kamba sehemu au mbuzi, ile kamba huitwa akili kwa tamko letu ila kwao hutamkwa " 'aql".

Maarifa ni kujua jambo baada ya kutokulijua. Sisi husema fulani ana maarifa ya jamii, huyu ameyajua mambo ya jamii baada ya kuto yajua.
 
Back
Top Bottom