Mkuu kule kuna watu wenye fani zao yaani fani unazoziona uraiani zote kule zipo kuna wanaojua kusuka, kushona,kufuma, mafundi uashi, mafundi selemala hata walimu, wafanyabiashara wakubwa na wadogo wapo kule, yaani kule anaenda yeyote kumbuka kile ni kijiji cha Mtakuja yaani utake usitake na siku saa usioitegemea wewe unaweza kwenda hata kama ni kwa masaa, hata viongozi wa dini wapo kule ukitaka kuamini nenda kamtembelee mfungwa au mahabusu yeyote utajionea mwenyewe halafu wana tabia ya kubadilishana ujuzi usishangae kuona dada yetu naye karudi na kaujuzi!