RGforever
JF-Expert Member
- Apr 3, 2011
- 6,878
- 5,424
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.
Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.
Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza.
SOURCE: ITV
Breaking News: Msanii Maarufu Lulu Michael anayekabiliwa na tuhuma za mauaji ya Msanii mwenzake Steven Kanumba amepata dhamana leo. Baadhi ya masharti aliyopewa Lulu ni pamoja kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani na wafadhili kuweka bondi ya Shilingi mil 20
UPDATES:
- Sasa ndio wanakagua documents za wadhamini mahakamani...
- Kuna mambo hayajakamilika hivyo anarudi jela, hadi kesho...
FINAL UPDATE (03:00 PM, 28, Jan, 2013)
Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho kwakuwa Msajili wa Mahakama Kuu hakuwepo na hii ilikuwa ni kesi ya 'Kuua bila kukusudia'.
Kesho wadhamini watawasilisha nyaraka zao mbele ya msajili ndipo anaweza kuachiwa...
Tutawafahamisha kitachojiri mahakamani kesho