Lukuvi na Kapteni Komba matatani

Lukuvi na Kapteni Komba matatani

Hebu niambie kama komba anasema maneno kama hayo inaonyesha jinsi gani viongozi wanavyo wadharau wananchi.

Kwani Komba ni kiongozi wa nchi siyo kwamba ana uzoefu wa kuongoza ngoma tuuu. Sasa unategemea nini kutoka kwake, je ni askari kweli maana ninajua huo ukaptain alipewa kama zawadi ya kuimba. Wale walio uhenyea unawasikia wakibwabwaja ovyo?
Fikeni mahali tuwatofautishe viongozi na wacheza ngoma.
 
Chuki za Lukuvi kwa Waislam, maji shingoni!

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Urataibu wa Bunge), William Lukuvi, amezidi kukaliwa kooni kwa kutakiwa kujiuzulu kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi kanisani.

Msimamo huo ambao ni wa pili kutolewa dhidi ya waziri huyo, ulitolewa jana katika Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zenye msimamo mkali.

Mbali ya kujadili kauli ya Lukuvi, kongamano hilo pia lilijadili umuhimu wa kufanya maboresho kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, ambalo wanadai limekuwa likiwaacha nje baadhi ya vijana wa Kislamu waliofikia umri wa kujiandikisha kupiga kura.

Kongamano hilo liliwakutanisha watoa mada mashuhuri, wakiwemo maimamu wa misikiti mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani. Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao, Msemaji wa Taasisi hiyo, Sheikh Rajabu Katimba, alisema lengo la kukutana na wanajumuiya hizo ni kufanya maazimio ya pamoja juu ya kauli za uchochezi zilizotolewa na Lukuvi pamoja kujadili daftari la kudumu la wapiga kura.

"Bado tunaendelea na msimamo wetu juu ya mchochezi huyo anayetaka kuvuruga amani, hatutaishia kwenye kongamano hili, tutafanya nchi nzima na kutoa uelewa kwa Waislamu na Watanzania wapate kujua madudu aliyosema Lukuvi," alisema Katimba.

Alisema licha ya kusambaza nakala kwa viongozi wakubwa wa nchi na Watanzania, wataendelea kulaani kauli ya Lukuvi hadi Rais Kikwete atakapoamua kumwajibisha.
"Kauli za Lukuvi hazivumiliki kwani ni hatari kwa taifa, kiongozi mkubwa kuongea vitu kama vile haifai, tena badala ya kwenda bungeni kuomba radhi kwa Waislamu na Watanzania, yeye kazidi kuonyesha uhodari wa kuchochea uvunjifu wa amani," alisema Katimba.

Aliongeza kuwa wamekuwa na utaratibu wa kufanya makongamano mara kwa mara ili kutoa elimu zaidi kwa Waislamu, pamoja na kujadili mchakato wa katiba na sio kwa Mkoa wa Dar es Salaam bali watahakikisha wanazunguka nchi nzima kutoa elimu hiyo.

"Hatujasitisha makongamano, tutaendelea kama kawaida mpaka tutakapopata muafaka juu ya kiongozi huyo, la sivyo tutazidi kuongeza kasi ya kuwafikia Waislamu na Watanzania popote pale walipo, na wakati huo tukifanya utaratibu wa kuchukua hatua za kisheria," alisema.

Kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura, Sheikh Katimba alisema liboreshwe kwani kuna vijana wa Kiislamu waliotimiza umri wa miaka 18 mwaka 2014 na wengine mwaka 2013, lakini hawamo kwenye orodha ya wapiga kura.

"Endapo vijana wetu waliotimiza umri huo wa kupiga kura wasipoandikishwa kwenye daftari hilo, hatutokubali na tutakuwa tayari kwa lolote lile mpaka kieleweke, pia tutasimamia haki yao hadi ipatikane, kwani kuna vijana wetu wengi wanaachwa na kukosa haki zao za msingi kumchagua kiongozi wanayemtaka," alisema.
Aliilaumu serikali kwamba imekuwa haizingatii kutenda haki kwa Waislamu katika masuala ya elimu.

"Tunaminywa haki zetu Waislamu, Mahakama ya Kadhi imetupiliwa mbali, hata katika masuala ya kiuchumi bado tunasumbuliwa, hasa kwenye Umoja wa Kiislamu (OIC), kwa mfumo huo hatutakubali na tutadai haki zetu hadi kieleweke kupitia makongamano haya," alisema Katimba.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu na Mihadhara Zanzibar ya Uamsho, Abdallah Said Ally, ambaye alikuwepo katika Msikiti wa Mtambani jana, alisisitiza kauli waliyoitoa hivi karibuni ya kumtaka Lukuvi kuachia ngazi.

Kuhusu Muungano

Akizungumza katika kongamano hilo, Sheikh Ali Baseleh, amesema kuwa mamadiliko ya katiba lazima yafanyike kwa sababu ya katiba ya sasa ina kasoro kubwa katika muundo wa Muungano.

Sheikh Baseleh, alisema sio kweli kuwa waliopendekeza na wanaounga mkono muundo wa serikali tatu, wanataka kuvunja Muungano.

"Kama maoni ya wananchi kuhusu serikali tatu yalikuwa hayatakiwi, kwanini zimetumika pesa nyingi kuunda tume ili ishughulikie suala la katiba mpya?" alihoji.

Alisema wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, walipaswa kujadili maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu, lakini waliyaacha na badala yake walikuwa wakipeana mipasho na kudhalilishana na hadi lilipoahirishwa, hakuna jambo la maana lililokwishafanyika.

"Haya maoni ya wananchi yameletwa kwa ajili ya kuboresha katiba kwa sababu ya sasa ina kasoro nyingi, leo Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawataki, wanataka kuleta maoni yao ya serikali mbili ambayo hayamo kwenye rasimu," alisema.
 
... leo Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawataki, wanataka kuleta maoni yao ya serikali mbili ambayo hayamo kwenye rasimu,” alisema.
Lakini waisilamu hao hao walimuunga mkono JK wa CCM mwaka 2010 kwa maelekezo ya Lipumba wa CUF. Kwa ujumla waisilamu ni watu wa kutumiwa tumiwa hivi!
 
tatizo la waislam umoja haupo hatupendani wacha yatufike mpaka pale tutakaposimamia maamrisho ya alwah na kuacha unafiki
 
Hawajaongelea pia "mfumo Kristo" pamoja na kuwa MARAIS wote watano wa nchi hii ni Waislamu?
 
Watu hatujamwelewa Komba, amesema kwamba serikali 3 zikipita yeye atakwenda msituni kujificha!!
 
Kusema aseme lukuvi akisema ponda lawamaa

Awajibike tuh kihiyo huyo
 
Nilimsikikia mjumbe wa bunge la katiba Capt Komba akitoa maoni yake kwamba kama nchi itakuwa ya serikali tatu akakimbimbilia msituni kupinga serikali tatu. Kwanza kabisa napenda kumuuliza huyo anaetaka kujiita askari wa msituni
ni mara ngapi amesha enda front line kukabiliana na adui . Nina imani kabisa kama askari yeyote yule amesha enda front line sijui kama suala la kupigana vita ni good option for him , .Pata ushauri wa bure kwa Yoweri Museveni.

Usilitie madoa jeshi jeshi letu. Hivi tunapozungumzia vita vya siku hizi ukikabidhiwa kikosi kuelekea front line kweli mtarudi ?. Nategemea ulikuwa na maaana ya kwenda msituni kujisaidia tu sio kupigana hapo nitakusamehe
 
tupo pamoja waislam wenzangi

Kwa nini waislamu wenzako tu?Unadhani tuliowakristu hatuioni impact ya kauli ya Lukuvi?Unadhani tumefurahishwa nayo?Imagine unashemeji,wifi,shangazi,binamu nk nk ni waislamu utaenda kuishi nao vipi kwa kauli ya Lukuvi?

Upande wangu nimemuona hata huyo mchungaji wa kanisa hakuwa na busara ya kumruhusu kusema aliyosema,siyo mahala pake.Imapct yake ingekuwa ndogo sana kama angesemea kwenye mikutana yao ya siasa,au chama siyo kanisani?

Hivi wanasheria na wale wanaojiita watetea haki za binadamu wako wapi?Waandishi wa habari je?Mpaka wanasiasa wetu waione Afrika ya Kati ndani ya Tanzania ndiyo watajifunza kufunga midomo yao?Leo wanaohangaika kuleta AMANI afrika ya kati ni Mashekhe na Maaskofu,wanasiasa wapo ughaibuni wanasubiri kutulie warudi kusaka KURA na ULAJI tu.

I wish tungekuwa na Rais mwenye uelewa wa kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom