Lukuvi na Kapteni Komba matatani

Lukuvi na Kapteni Komba matatani

Hivi huko CCM kuna mtu wa kumnyooshea mwenzake kidole kweli?

Huwa nawahesabu CCM kama mavi tu...

Mwingine amejimege eneo la chuo cha Ualimu Bunda/Bunda sec. kajenga nyumba naye anajidai ni msafi na anaweza hata kugombea Uraisi.

Mwingine kamega eneo la shule ya sekondari Morembe kajenga nyumba, naye anajifanya msafi. Hao ndio CCM. Ujambazi mtupu.
 
Hivi angekuwa Lipumba aliyesema huo upuuzi wa Komba leo angekuwa huru uraiani au selo ya polisi?
 
Matendo ya CCM wakati mwingine kichefuchefu kweli kweli ...No wonder wanatu-rank number one kwa kuwa na IQ ndogo...
 
..how about JK?

..unajua matatizo mengi sana ya CCM yanaanzia na JK.

..mtandao, makundi, rushwa ktk uchaguzi, vyote vimetokana na ambitions za JK kuwa Raisi.

..Richmond nayo inaelekea mhusika ni JK kwasababu haiyumkiniki Waziri Mkuu akiuke maagizo ya baraza la mawaziri bila kuwa na baraka za Raisi.

..hata hivyo vitisho alivyotoa Lukuvi ni kama ameiga tu kwa JK.

..sasa mnasema kamati ya maadili itamhoji Lukuvi, kwanini kamati hiyo haianzi na kuifanyia kazi ripoti ya Philip Mangula ambayo ilimtuhumu JK kwa kukihujumu chama??

cc Pasco, Nguruvi3, Mag3
Hili suala la Lukuvi ni la kuangalia sana. Lukuvi hana hatia wala kosa.
Alichokifanya ni kufikisha ujumbe wa serikali akimwakilisha waziri mkuu Pinda.

Utaratibu wa kuwakilisha ni kueleza alichokusudia mwalikwa. Mwalikwa alikuwa Pinda ambaye ni msadizi wa Rais Kikwete.

Hivyo Lukuvi hana sababu ya kujitetea au kuitwa katika kamati ya maadili. Yeye ni mtumishi aliyetumwa na serikali.

Watu wanashindwa kuelewa kuwa katika miaka 50 ya uhuru hakuna kiongozi aliyeweza kuchochea hisia za majeshi kama JK. Mkuu wa nchi ndiye aliyefungua Pandora box, hawa akina Komba wanashadidia maneno ya bosi wao. Kwa lugha nyingine wanasherehesha hoja za JK.

Komba alikuwa mwanajeshi, JK kasema majeshi yataleta taabu kukiwa na S3, alichokifanya Komba ni kuonyesha mfano wa jinsi watakavyoleta vurugu mbele ya safari kama alivyosema Amir Jeshi mkuu JK.

Baada ya maneno ya Lukuvi, kilichopaswa kufanywa ilikuwa kumlazimisha ajiuzulu ili kuisafisha serikali kutokana na uchafu.

JK ndiye aliyemteua hivyo alipaswa kumwajibisha, kama mtumishi wa chini lakini pia Rais anayelinda katiba na umoja wa kitaifa. JK hakufanya hivyo na Pinda hawawezi kumkemea kwasababu ndiye aliyempa ujumbe.

Kwa staili ya JK kukwepa lawama au kutoudhi mtu, suala hilo amelipeleka katika vikao vya chama vya maadili.

Hakuna sababu ya mambo nyeti kama hili la Lukuvi kwenda kwenye chama.
Lukuvi ni waziri wa serikali hivyo ni mtu wa watu wote.

Kama amewakosea hapaswi kuomba radhi kamati ya maaadili ya CCM anapaswa kuwaomba radhi Watanzania.

Kuomba radhi ni kuachia ngazi kwasababu tayari ameshapanda mbegu mbaya sana ambayo siku za usoni inaweza kuligharimu taifa. Aliyepaswa kumsaidia Lukuvi kuomba radhi ni JK kwa kumpunzisha kazi.

Hatua zozote za CCM kumkaripia au vyovyote ni sawa na jibwa lisilo na meno.
Hii ni mbinu ya kumsafisha JK na Pinda ambao sasa wanalielekeza taifa katika pori la dhahma.

CCM ni nani kwa taifa hili? Nape Nanuye anaweza kufanya nini mbele ya Lukuvi. Nchemba atamwambia nini Lukuvi.

Naona watu wanakimbia ukweli na kumshambulia Lukuvi na Komba.
Ukweli ni kuwa hao ni vipaza sauti tu.

Tatizo lote na jukumu lote lipo kwa Kikwete ambaye si kuwa anawatuma tu bali hawezi hata kuwakemea au kuwafukuza kazi.

Hii maana yake ni moja, tayari watu wanajijengea mfano, na nitashangaa kama atatokea kiongozi na kudai ameagiza mabomu na bunduki halafu akachukuliwa hatua.
Hatua gani ambazo Lukuvi hapaswi kuchukuliwa na serikali?

Hili ni la JK wala si Lukuvi. Mwacheni Lukuvi mnamuonea bure.
Hivi kwanini umhukumu karani aliyefikisha jalada la bosi sehemu husika?
Kwani karani amefanya kosa gani?

Mwacheni Komba hana makosa, yeye alichofanya ni kusherehesha maneno ya Amir Jeshi mkuu.

 
Kesi ya panya iendeshwe na uko wa panya ? It is impossible.
 
huenda wakahojiwa na
Kamati ya Maadili ya CCM kwa kauli zao za vitisho na uchochezi. Yumo pia
Balozi Ali Karume.

Waombe Mungu yasitokee mauaji, yakitokea tu wana kesi ya kujibu de. Hague. NAWAOMBENI VIONGOZI MLIOPEWA DHAMANA TUMIENI BUSARA ZENU ZILIZOFANYA MKATEULIWA. MKIKOSA HEKIMA OMBENI DUA KW MUNGU ATAWAPA (YAK 5)
 
hivi siku hizi UHAINI (JINAI) unashughulikiwa na Kamati kuu ya CCM??. duh hii kweli ni nchi ya utawala wa sheria!!! Paradiso bado ni mbali sana
 
watanzania hatuna msimamo nabado tutaendeshwa na hawa walafi mpaka tuone joto la jiwe..... ninawapwnda wazanzibar kwakuwa wanamsimamo naamini watafanikiwa.
 
Back
Top Bottom