maganjwa
JF-Expert Member
- Sep 11, 2012
- 2,806
- 2,349
waliopo matatani ni Watanzania kwa usingizi wao wa pono
Walioko matatani ni wanzania kweli kabisa tuko matatani mkuu sio mchezo hao hatua waliyofikia sio nzuri.
waliopo matatani ni Watanzania kwa usingizi wao wa pono
watanzania hatuna msimamo nabado tutaendeshwa na hawa walafi mpaka tuone joto la jiwe..... ninawapwnda wazanzibar kwakuwa wanamsimamo naamini watafanikiwa.
Kwa mainterahamwe ni uzushi, haiwezekani wakahojiwa!
huenda wakahojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM kwa kauli zao za vitisho na uchochezi. Yumo pia Balozi Ali Karume.
Kweli ndugu yangu, JK mwenyewe alisema wakipendekeza serikali 3 kuna hatari ya jeshi kuchukua nchi kwa hiyo na yeye ahojiwe.
Hili suala la Lukuvi ni la kuangalia sana. Lukuvi hana hatia wala kosa.
Alichokifanya ni kufikisha ujumbe wa serikali akimwakilisha waziri mkuu Pinda.
Utaratibu wa kuwakilisha ni kueleza alichokusudia mwalikwa. Mwalikwa alikuwa Pinda ambaye ni msadizi wa Rais Kikwete.
Hivyo Lukuvi hana sababu ya kujitetea au kuitwa katika kamati ya maadili. Yeye ni mtumishi aliyetumwa na serikali.
Watu wanashindwa kuelewa kuwa katika miaka 50 ya uhuru hakuna kiongozi aliyeweza kuchochea hisia za majeshi kama JK. Mkuu wa nchi ndiye aliyefungua Pandora box, hawa akina Komba wanashadidia maneno ya bosi wao. Kwa lugha nyingine wanasherehesha hoja za JK.
Komba alikuwa mwanajeshi, JK kasema majeshi yataleta taabu kukiwa na S3, alichokifanya Komba ni kuonyesha mfano wa jinsi watakavyoleta vurugu mbele ya safari kama alivyosema Amir Jeshi mkuu JK.
Baada ya maneno ya Lukuvi, kilichopaswa kufanywa ilikuwa kumlazimisha ajiuzulu ili kuisafisha serikali kutokana na uchafu.
JK ndiye aliyemteua hivyo alipaswa kumwajibisha, kama mtumishi wa chini lakini pia Rais anayelinda katiba na umoja wa kitaifa. JK hakufanya hivyo na Pinda hawawezi kumkemea kwasababu ndiye aliyempa ujumbe.
Kwa staili ya JK kukwepa lawama au kutoudhi mtu, suala hilo amelipeleka katika vikao vya chama vya maadili.
Hakuna sababu ya mambo nyeti kama hili la Lukuvi kwenda kwenye chama.
Lukuvi ni waziri wa serikali hivyo ni mtu wa watu wote.
Kama amewakosea hapaswi kuomba radhi kamati ya maaadili ya CCM anapaswa kuwaomba radhi Watanzania.
Kuomba radhi ni kuachia ngazi kwasababu tayari ameshapanda mbegu mbaya sana ambayo siku za usoni inaweza kuligharimu taifa. Aliyepaswa kumsaidia Lukuvi kuomba radhi ni JK kwa kumpunzisha kazi.
Hatua zozote za CCM kumkaripia au vyovyote ni sawa na jibwa lisilo na meno.
Hii ni mbinu ya kumsafisha JK na Pinda ambao sasa wanalielekeza taifa katika pori la dhahma.
CCM ni nani kwa taifa hili? Nape Nanuye anaweza kufanya nini mbele ya Lukuvi. Nchemba atamwambia nini Lukuvi.
Naona watu wanakimbia ukweli na kumshambulia Lukuvi na Komba.
Ukweli ni kuwa hao ni vipaza sauti tu.
Tatizo lote na jukumu lote lipo kwa Kikwete ambaye si kuwa anawatuma tu bali hawezi hata kuwakemea au kuwafukuza kazi.
Hii maana yake ni moja, tayari watu wanajijengea mfano, na nitashangaa kama atatokea kiongozi na kudai ameagiza mabomu na bunduki halafu akachukuliwa hatua.
Hatua gani ambazo Lukuvi hapaswi kuchukuliwa na serikali?
Hili ni la JK wala si Lukuvi. Mwacheni Lukuvi mnamuonea bure.
Hivi kwanini umhukumu karani aliyefikisha jalada la bosi sehemu husika?
Kwani karani amefanya kosa gani?
Mwacheni Komba hana makosa, yeye alichofanya ni kusherehesha maneno ya Amir Jeshi mkuu.
Matendo ya CCM wakati mwingine kichefuchefu kweli kweli ...No wonder wanatu-rank number one kwa kuwa na IQ ndogo...
hongera lukuvi
Hivi zile kauli za inchi hi haitotawalika iliwahi kutolewa na kiongozi gani vile Upinzani? Na Je alichukuwa hatua gani kisheria?
Hivi vitisho vilitolewa kuwapa wapiga kura hofu na kweli wapiga kura zaidi ya 10,000,000 waliogopa kujitokeza kupiga kura na Kikwete alishinda kwa kura 5,000,000! Kwa sasa Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo ni Balozi wetu China! Jeshi na siasa wapi na wapi!Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo - Mnadhimu Mkuu JWTZ said:Vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au taasisi yoyote itakayokwenda kinyume na (cha) sheria, kuchochea au kufanya fujo, kuvunja amani kwa mujibu wa sheria. Aidha, kuchochea kuyakataa matokeo.
Vyama vya siasa vifanye kampeni kwa ustaarabu na kufuata sheria na kanuni za uchaguzi, visitukane vyombo vya dola wala kuvichokoza kwa vile havihusiki na siasa zaidi ya kulinda amani na utulivu
huenda wakahojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM kwa kauli zao za vitisho na uchochezi. Yumo pia Balozi Ali Karume.
Kuna waliozuiwa kufanya harambee misikitini na makanisani wakaamua kuongeza kasi ya kuhudhuria misiba!