LUKU zaleta kizaazaa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LUKU zaleta kizaazaa Dar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzalendo_Mkweli, Sep 3, 2012.

 1. M

  Mzalendo_Mkweli JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 719
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Wana JF mwasemaje? Sababu ni nini? Je huu usumbufu ungeweza kuepukwa?

  Home
   
 2. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  usumbufu gani huo maana wengine tumefuata maelekezo na tumefanikiwwa bila shida
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  LUKU zaleta kizaazaa Dar
  By Moshi Lusonzo  2nd September 2012.

  Zoezi la ubadilishaji wa mfumo mpya wa kununua ankara za umeme wa Lipa Umeme Kadri Unavyotumia (Luku) umezua kizazaa jijini Dar es salaam baada ya watu wengi kufurika katika vituo vya kuuzia umeme.

  Hivi karibuni Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limetangaza kubadilisha mfumo wa ununuaji umeme wa Luku na kuanzisha mfumo mpya ulioanza kutumika rasmi jana, ambapo wananchi walitakiwa kwenda kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kuingia kwenye mfumo mpya wa ulipaji ankara.

  Vituo vilivyotembelewa na Gazeti hili, ilishuhudia misururu mirefu ya wananchi nje ya vituo mbalimbali wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.
  Baadhi ya vituo vilivyoonekana kuwa na watu wengi ni pamoja na Magomeni Makanya, Mwenge, Kijitonyama, Ilala, Temeke na katikati ya jiji.

  Baadhi ya wananchi waliotakiwa kuelezea zoezi hilo, walisema pamoja na Tanesco kuamua kuanzisha mfumo huo kwa nia ya kuboresha mapato yao, lakini kumekuwepo na upungufu ikiwemo mawakala wengi kutojiandaa na zoezi hilo.

  Muhidini Issa mkazi wa Kijitonyama aliyekutwa kituo cha kuuzia umeme cha Oilcom alisema watu wengi wamejikuta wakisimama kwenye foleni kwa muda mrefu wakisubiri kupatiwa huduma kutokana muuzaji wa kituo hicho kufanya kazi taratibu.

  "Nilichogundua wauzaji wengi walikuwa hawajajiandaa na zoezi hili kwani wanafanya kazi taratibu sana na kusababisha kuwepo na foleni, angalia mwenyewe jinsi watu walivyojaa hapa kituoni," alisema Issan
  Hata hivyo, Muuzaji wa umeme kituo cha Fountain eneo la magomeni Makanya, Twaha ramadhani alisema kiujumla walijiandaa kikamilifu katika zoezi hilo na kwenye kituo chake hakukuwepo na foleni kubwa baada ya kutumia Kompyuta kwa ajili ya kuwahudumia watu badala ya mashine ndogo.

  Alisema zoezi la kubadilisha mfumo wa ulipaji unafanyika mara moja kwa mteja kupewa namba za aina tatu ili kufanya Luku yake itambuliwe na mfumo huo na baada ya hapo mteja atanunua umeme kama ilivyo zamani pamoja na kwenye simu zao za mkononi.  SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kiarticle hakijaeleza sababu ya mabadiliko.

  Nna mashaka hata muandishi anajua.
   
Loading...