Lugha na elimu ya kitanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lugha na elimu ya kitanzania

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Jackbauer, Jan 16, 2011.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wanafunzi wa kitanzania wanakabiliana na kikwazo kikubwa cha lugha katika mafunzo yao.
  Chukulia kwenye mtihani,mwanafunzi kaulizwa swali kwa english itambidi alitafsiri kwa kiswahili halafu kwa kinyumbani(mfano kikwere)
  vivo hivyo akipata jibu atatakiwa ageuze mtiririko niliotaja hapo juu ili kupresent jibu lake.yaani thinking process ya kibongo ni ngumu sana.
  Tupunguze lugha moja kati ya kiswahili na kingereza!
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni sawa kabisa suala ulilolileta hapa. Pamoja na kuwa serikali mara kadhaa imekuwa ikipanga sera ya lugha, lakini tumekuwa hatufiki popote kutokana na ufinyu wa fikira wa viongozi wetu.

  Mimi sina ugomvi na lugha gani itumike, lakini serikali ingepaswa kuwa na sera madhubuti ya lugha, ingawaje kwa mtazamo wangu lugha yetu ya Kiswahili inapaswa kutumika kuanzia msingi hadi chuo. Wnaharakati wa lugha yetu tayari wameshafanya tafiti nyingi zinazoonesha kuwa hili linawezekana. Lakini kwa tamaa za kusaidiwa vijisenti vichache vya kukuza Kiingereza, mpango wa kukifanya Kiswahili lugha ya kufundishia unakwamishwa.

  Wakati umefika tuamuwe kutumia lugha moja ya kufundishia. Hii haina maana kuwa tukitumia moja tutakuwa hatutumii nyengine, lakini kwa mpango wa sasa tunawasumbua na kuwadumaza watoto wetu. Sera ya sasa ni kuwa tunaanza na Kiswahili wakiwa msingi, na tunafundisha kwa Kiingereza wanapoanza sekondari. Matokeo yake watoto wetu hawajuwi Kiswahili wala Kiingereza. Kwa nini isiwe moja tu?

  Imani yangu ni kuwa ikiwa tunataka maendeleo ya kweli, wakati ni huu wa kukikuza Kiswahili chetu kiwe cha kufundishia viwango vyote. Tukumbuke kuwa hakuna nchi yoyote ulimwenguni inayoweza kuendelea ikiwa itadharau lugha yake kama inavyofanywa hapa kwetu. Mtoto hufikiri na kuwa mbunifu kwa kutumia lugha yake na sio kufikiria katika lugha yake na kujieleza katika lugha nyengine. Pia tusizionee haya lugha zetu nyengine. Ingelifikiriwa pia kuangalia uwezekano wa kufundisha lugha zetu za makabila, (angalau kwa matumizi ya ndani, kwani hizi ni lugha kamili) na lugha nyengine za kigeni ili kuwapa fursa na uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa vijana wetu. INAWEZEKANA.
   
 3. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Binfasi ninashauri matumizi ya kiswahili,kuna sababu nyingi sana za kutumia kiswahili.NImewahi kuandika makala ambapo nilielezea faida kadhaa zza kutumia kiswahili na jinsi ya kuzibadilisha lugha za kigeni ili zitunufaishe badala ya kutukandamiza na kuturudisha nyuma,Nenda kwenye makala hii Tunajifunza nini toka maendeleo ya teknolojia ya China – AfroIT Blog-Wazee wa mididi! .

  Pia binafsi siku za kwanza kuanza kutumia kiswahili kufundishia au kuandika makala ilikuwa tabu mno,nilichanganya kiswahili,kingereza na hata kichina ndani yake.Ila leo ninaweza kuandika makala ndefu huku kiwango cha lugha ngeni kikiwa asilimia chini ya tano.Hivyo kama tukiamua na kuwa na malengo tunaweza.

  Tukipe nafasi yake kiswahili halafu tuangalie.Sisi kama AfroIT tumejipanga vya kutosha kwenye hili,naomba muda uchukue nafasi yake tudhihirishe.
   
 4. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani hakuna ubaya. Bora lugha ya shule iwe kingereza sababu concept nyingi ni za kingereza na siku hizi mambo ya globalization yamevunja mipaka. Ni sawa kabisa watu wengi iwezekanavyo wawe fluent katika lugha takriban moja ya kimataifa.
  Kwa upande mngine somo la kiswahili kiendelee kuwepo kama module, ila sio topic zote ziolewe kwa kiswahili. Kiswahili tunakijua toka nyumbani, huko tujifunza safuri tu.
  Serikalini lugha ziwe mbili, kiswahili na kiingereza, na kwenye mikutano yao wnasema kabisa lugha litakalo tumika katika mkutano huu ni kiswahili, au ni kingereza.
  Inawezekana, na nadhani inatakiwa, lugha zote mbili wizepo ila waweke utaratibu maalum wa kujua lugha gani inatumika.inafunzwa wapi
   
 5. T

  Tata JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,731
  Likes Received: 647
  Trophy Points: 280
  Tatizo siyo lugha ya kufundushia yaani ama kiingereza au kiswahili. Tatizo ni shule zinazoendeshwa kihuni zikiwa hazina walimu waliohitimu kwenye fani zao, hazina vifaa vya kufundishia, hazina maabara kwa shule za sayansi, hazina madawati na nyingine hata vyumba vya kusomea ni mgogoro. Hata ukisema leo kuwa lugha ya kufundushia iwe kiswahili kama haya mambo ya msingi hujayatatua utakuwa unatwanga maji kwenye kinu tu. Ukimchukua, mfano, mwalimu kihiyo ukamwambia atumie kiswahili kufundishia bado mwanafunzi hataelewa anachofundishwa.
   
Loading...