Tutafakari Hoja za HAKIELIMU na Freeman Aikaeli Mbowe kuhusu Kiswahili kama lugha ya kufundishia

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,412
1,960
Assalamualaikum wana JF!
Naenda moja kwa moja kwenye mada yangu hapo juu:

Kupitia hotuba yake katika 'CLUBHOUSE' siku chache zilizopita Freeman Aikaeli Mbowe au FAM alitofautiana kidogo Serikali, HAKIELIMU na labda kundi kubwa la Watanzania wenye msimamo kwamba lazima Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia nchini Tanzania.

Tamko hili muhimu la Freeman Aikaeli Mbowe na hoja alizozitoa mbele ya washiriki wenzake, wasikilizaji kama mimi, na kimsingi kwa Watanzania wote akipingana na falsafa ya HAKIELIMU, na sera rasmi ya Serikali ya JMT; tamko hili linapasa kuibua mjadala mpya na MAKINI, kuhusu elimu yetu na muelekeo wake kitaifa.

Kwasababu Serikali na wafuasi wa sera au falsafa yake ni wengi (hata humu JF) na HAKIELIMU wana hoja zao kwa upande wao, ambazo hazipaswi kupuuzwa.

Lakini ni ukweli pia kwamba hoja za upande wa FAM kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama kikubwa cha siasa Tanzania na wafuasi wa falsafa yake kama mimi; hoja zake hazipaswi kupuuzwa.

Misingi ya hoja za pande hizi mbili za mjadala huu ni za aina nyingi, lakini ipo misingi minne muhimu inayopaswa kuzingatiwa na pande hizo mbili ambayo ni:

1. Misingi ya Kisayansi,
2. Misingi ya Kisiasa,
3. Misingi ya Kiuchumi na
4. Misingi ya Kiutamaduni.

Lengo la mada yangu ni kuonyesha kwamba japokuwa misingi hii minne yote ni muhimu lakini inatofutiana kwa uzito. Na kwa maoni yangu misingi ya kisayansi ina uzito zaidi kuhusu hatma ya elimu yetu katika dunia ya sasa na siku zijazo.

Kwanza kwakuwa tunazungumzia suala la ELIMU, ni lazima kila upande kwanza kabisa uwe na misingi ya kisayansi kuhusu hoja zao kuliko mambo mengine yote. Vinginevyo tutaendelea kubishana miaka nenda rudi na matokeo yake ni sera za elimu zisizo tekelezeka au zisizo na tija kitaifa na kimataifa.

Kwahiyo kupitia hoja zangu katika mjadala huu najikita kwenye misingi hiyo minne muhimu niliyotaja hapa juu. Ingawa ni muhimu nikiri kwamba uwezo wangu wa kuchambua misingi ya kisayansi sio kama wa wataalamu wetu akina Hakielimu, Professor Mkumbo nk. Ambao ni wafuasi wakuu wa sera rasmi ya Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kama lugha ya kufundishia.

Kwahiyo swali la kwanza tunapaswa kujiuliza ni je, kuna misingi na sababu za kisayansi za kufanya iwe LAZIMA Kiswahili kuwa lugha pekee ya kumfundishia mwanafunzi wa Kitanzania katika ngazi zote za elimu Tanzania? Na kama kweli kuna misingi ya kisayansi kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia, kwanini haziwekwi wazi? Tuachokiona ni matangazo ya sekunde chache ya HAKIELIMU kwenye TV ambayo kwa maoni yangu yanamfanya kijana wa Kitanzania ajihisi na kuamini kwamba hana uwezo wa (a) kuijua lugha ya Kiingereza; na (b) kujifunza kwa lugha ya Kiingereza! Jambo ambalo kwa maoni yangu si kweli na linatudhalilisha kama taifa mbele za ulimwengu wa sasa!
Hakielimu kupitia tangazo hili wanauambia umma wa Watanzania na dunia nzima kwamba kijana mwanafunzi wa Kitanzania yuko kama hao kwenye tangazo lao!

Mwanafunzi wa chekechea au shule ya msingi anapata ujumbe gani anapoona tangazo hili kama sio kumkatisha tamaa kwamba 'HAWEZI' badala ya kumtia moyo kwamba 'ANAWEZA' ?

Lakini sina hakika kwamba tangazo la Hakielimu linatokana na utafiti wa kisayansi kuhusu uwezo au hapana wa watoto wote wa Kitanzania kujifunza Kiingereza na kujifunzia masomo mengine kwa lugha ya Kiingereza.

Na kama kuna utafiti wa kisayansi kudhihirisha maudhui ya tangazo la Hakielimu, lazima tujiulize kwanini watoto wote wa Kitanzania washindwe kufundishika na kujifunza kwa lugha ya Kiingereza? Wana kasoro gani?

Naamini pia kwamba wafadhili wa tangazo hili la Hakielimu wana ajenda zao kuhusu mwelekeo wa elimu yetu ambazo binafsi nazitilia mashaka kwasababu kuna tofauti kubwa kati ya haki ya kupata 'elimu' na haki ya kupata 'Elimu Bora'.

Kama tangazo la Hakielimu lingeonyesha mwanafunzi mmoja akilalamika haelewi na mwenzake akimwambia akazane tu ataweza; ningekubaliana nalo. Mafanikio ya mwanafunzi darasani ni lazima yategemee bidii yake na ya mwalimu. Siyo kufanya tendo la kujifunza darasani kuwa kama mahali pa gumzo la eti Kiingereza kigumu, hesabu ngumu nk.

Lakini vile vile lazima tujiulize kwanini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanaohubiri Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia wengi wao wanapeleka watoto wao kwenye English medium schools? Lengo lao hasa kuhusu sera ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni kuboresha elimu yetu au kutulaghai ili watoto wetu wapate "bora elimu" badala ya Elimu Bora?

Baadhi ya hoja za Freeman Aikaeli Mbowe kuhusu Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia badala ya Kiswahili ni taarifa alizonazo kuhusu uwezo wa Watanzania kushindana na wengine katika masoko ya ajira nje ya Tz na shughuli za kibiashara/kiuchumi katika nyanja za kimataifa. Kwa mujibu wa FAM lugha ya Kiingereza ni kikwazo kikubwa kwa Watanzania kuingia kwenye masoko ya ajira katika nchi kama Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, South Africa nk na hata Ulaya na USA nk.

2. Misingi ya Kisiasa.
Hoja yangu binafsi na naamini haitofautiani na msimamo wa FAM; ni kwamba sera za Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kama lugha ya kufundishia, misingi yake ni ya Kisiasa zaidi kuliko kisayansi. Na hapa ndipo chanzo cha udhaifu wa sera rasmi ya Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kuwa lugha pekee ya kumfundishia mwanafunzi wa Kitanzania.

Kama nilivyosema hapa juu na FAM pia alisema hivyo katika hotuba yake; kwamba baadhi ya wanasiasa na viongozi wa Serikali wanaohubiri Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia wengi wao wanapeleka watoto wao kwenye English medium schools. Lazima tujiulize kama watu wa aina hii (wanafiki) wanawezaje kutunga sera sahihi ya elimu yetu? Watu ambao unafiki wao unafanya iwe lazima tuwe na mashaka kuhusu elimu yao; na kwanini tusiamini kwamba lengo la sera yao ya Kiswahili kuwa lugha pekee ya kumfundishia mwanafunzi wa Kitanzania ni kumdidimiza ili kundi hili la wanasiasa liendelee kutawala?

Ushahidi uko wazi! Watawala wetu hivi sasa wanaendesha Serikali kupitia wanachosoma mafichoni au kusikiliza katika Twitter, Clubhouse, Maria Spaces nk. Sisemi kwamba wasifauatilie kinachoendelea huko lah! Lakini mahali pao sahihi pa kujadili sera za nchi ni bungeni. Kule wananchi na dunia itawaona na kusikia hoja zao na kuzipima kama zinafaa au sivyo.

4. Misingi ya Kiutamaduni.
Kwakuwa nimeshajadili kuhusu lugha ya Kiingereza kuwa kikwazo kikubwa kwa Watanzania kuingia kwenye masoko ya ajira nje ya Tz na shughuli za kibiashara/kiuchumi katika nchi kama Kenya Uganda Zambia Zimbabwe na USA na Ulaya ya Magharibi; naona vema nirukie kwenye misingi ya Kiutamaduni kuhusu Kiswahili au Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia.

Kuna watu wanataka tuamini kwamba Kiingereza ni lugha ya wakoloni kwahiyo kuendelea kuitumia katika elimu yetu ni utumwa, na ni kitendo cha kutoienzi lugha ya Kiswahili na utamaduni wetu!

Sikubaliani na fikra za aina hii. Kwasababu ni upotoshaji mkubwa kusema katika dunia ya sasa Kiingereza ni lugha ya wakoloni kama ilivyokuwa miaka 60 iliyopita! Kiingereza ni lugha ya kimataifa. Na kwa nchi nyingi duniani.

Zaidi ya Canada, Australia, New Zealand na Marekani, na nchi za kiafrika kama Zambia, Malawi, South Africa, Botswana, Namibia, Liberia, Ghana nk huwezi kusema kwakuwa wanaongea Kiingereza ni watumwa wa Uingereza!

Wasomi mashuhuri wa kiafrika kama Whole Soyinka, Chinua Achebe na wengine wa Nigeria, halafu Akina Okot Bitek wa Uganda, wanasifika kwa kuutukuza utamaduni wa kiafrika kupitia lugha ya Kiingereza! Kinyume na wanavyohubiri wanasiasa wetu kwamba Kiingereza kinaua utamaduni wetu.

Kwanza hatuwezi kukataa kwamba ukitaka kukabiliana na adui yako lazima ujue mbinu na mipango yake. Huwezi kufanya hivyo bila kuijua lugha yake! Na kwa mantiki hii ukitaka kujua mbinu za ushindani kwenye dunia ya sasa katika elimu, maendeleo, biashara, sayansi, nk, lazima ujifunze lugha inayotumika kimataifa, iwe Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani nk. Kufanya hivyo sio utumwa. Wala si kuabudu utamaduni wa wengine. Kwani sisi tunapowafundisha Kiswahili Wamarekani au Wanaijeria tunataka wawe watumwa wetu?
Au kuna mtu anaamini hao watu wakijua Kiswahili watasahau au kudharau utamaduni na mila zao?

Katika kudhani kwamba sera za Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni kuenzi utamaduni wa Watanzania; lazima tujiulize kwanini wanaojiita "wasomi" na vijana wa kizazi kipya wanaiga tabia za "wazungu" katika muziki, mavazi, urembo, na lugha na mambo mengine kadhaa majumbani mwao, na katika maeneo ya starehe nk?

Ukweli ni kwamba hatuwezi kujitenga na dunia ya sasa, kiuchumi, kielimu, kisiasa na kiutamaduni. Kama kuna mtu anadhani anaweza kuzuia Tanzania isiwe sehemu ya dunia anachojaribu kufanya ni sawa na kuzuia upepo kwa mikono yake! Haiwezekani!

Mwisho napenda kuomba tuache kufanya elimu ya watoto wetu kama sehemu ya kujifunzia kutunga sera za elimu kila awamu moja baada ya nyingine kwa lengo la kuongeza ufaulu wakati viwango vinashuka. Hatuwatendei haki vijana wa familia za hali ya chini. Badala yake tunazalisha matabaka ya wahitimu feki na wataalamu wa vyeti na madokta magumashi.
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,311
3,047
Nimeishia njiani sijamaliza kusoma,Ila nimekerwa na tabia ya undondocha aliyoionesha mwandishi wa Uzi huu. Amekuja na hoja baada ya kusikia mahojiano ya Mbowe kuhusu matumizi ya Lugha ya kiswahili kufundishia.
Halafu anahoji kama Kuna sababu za kisayansi zinazotufanya tutumie Lugha kiswahili kufundishia badala ya Lugha ya kiingereza? Nadhani mwandishi hapa ulipaswa utoe sababu za kisayansi pia kwanini tutumie Lugha kiingereza kufundishia wakati watoto wetu wanaongea Lugha ya kiswahili na ndio Lugha yao ya Taifa lao?
Au uje na utetezi kwanini wazungu (Waingereza) wasitumie Kigiriki na kilatini kufundishia na badala yake wanatumia Lugha yao ya kiingereza?
Binafsi naona hoja ya mwandishi na hoja Freeman Mbowe imekaa kiunyonge unyonge na kiufuasi wa nyayo za kibeberu Kwa hiyari.
Kwanini tusiwe na maamuzi yetu binafsi!?
Kuna faida lukuki za kutumia Lugha yetu ipasavyo kuliko athari zinazobainishwa kwenye hoja zenu.
Na wengi miongoni mwa wanaotetea matumizi ya Kiingereza kama Lugha ya kufundishia utakuta ni wale uwezo wa kusomesha watoto wao shule Bora hapa nchini na hata nje ya nchi,shule ambazo zina walimu bora wenye uwezo mkubwa.

Waliokuwa wengi ni wale ambao hawana huo uwezo wa kumudu kuwasomesha watoto wao katika shule hizo.watoto wao wanasoma shule za kata na zile nyingine ambazo ni za kawaida.
Shule ambazo hata walimu wao wengi hawana uwezo mkubwa wa kumudu kufundishia Kwa kiingereza ipasavyo. Kiingereza chenyewe Cha kuunga unga unategemea kutakuwa uelewa na mazingatio Kwa kiasi gani?

Binafsi naunga mkono matumizi ya Lugha ya kiswahili kufundishia mashuleni.
 
Nziiriman

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
293
377
Assalamualaikum wana JF!
Naenda moja kwa moja kwenye mada yangu hapo juu:

Kupitia hotuba yake katika 'CLUBHOUSE' siku chache zilizopita Freeman Aikaeli Mbowe au FAM alitofautiana kidogo Serikali, HAKIELIMU na labda kundi kubwa la Watanzania wenye msimamo kwamba lazima Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia nchini Tanzania.

Tamko hili muhimu la Freeman Aikaeli Mbowe na hoja alizozitoa mbele ya washiriki wenzake, wasikilizaji kama mimi, na kimsingi kwa Watanzania wote akipingana na falsafa ya HAKIELIMU, na sera rasmi ya Serikali ya JMT; tamko hili linapasa kuibua mjadala mpya na MAKINI, kuhusu elimu yetu na muelekeo wake kitaifa.

Kwasababu Serikali na wafuasi wa sera au falsafa yake ni wengi (hata humu JF) na HAKIELIMU wana hoja zao kwa upande wao, ambazo hazipaswi kupuuzwa.

Lakini ni ukweli pia kwamba hoja za upande wa FAM kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama kikubwa cha siasa Tanzania na wafuasi wa falsafa yake kama mimi; hoja zake hazipaswi kupuuzwa.

Misingi ya hoja za pande hizi mbili za mjadala huu ni za aina nyingi, lakini ipo misingi minne muhimu inayopaswa kuzingatiwa na pande hizo mbili ambayo ni:

1. Misingi ya Kisayansi,
2. Misingi ya Kisiasa,
3. Misingi ya Kiuchumi na
4. Misingi ya Kiutamaduni.

Lengo la mada yangu ni kuonyesha kwamba japokuwa misingi hii minne yote ni muhimu lakini inatofutiana kwa uzito. Na kwa maoni yangu misingi ya kisayansi ina uzito zaidi kuhusu hatma ya elimu yetu katika dunia ya sasa na siku zijazo.

Kwanza kwakuwa tunazungumzia suala la ELIMU, ni lazima kila upande kwanza kabisa uwe na misingi ya kisayansi kuhusu hoja zao kuliko mambo mengine yote. Vinginevyo tutaendelea kubishana miaka nenda rudi na matokeo yake ni sera za elimu zisizo tekelezeka au zisizo na tija kitaifa na kimataifa.

Kwahiyo kupitia hoja zangu katika mjadala huu najikita kwenye misingi hiyo minne muhimu niliyotaja hapa juu. Ingawa ni muhimu nikiri kwamba uwezo wangu wa kuchambua misingi ya kisayansi sio kama wa wataalamu wetu akina Hakielimu, Professor Mkumbo nk. Ambao ni wafuasi wakuu wa sera rasmi ya Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kama lugha ya kufundishia.

Kwahiyo swali la kwanza tunapaswa kujiuliza ni je, kuna misingi na sababu za kisayansi za kufanya iwe LAZIMA Kiswahili kuwa lugha pekee ya kumfundishia mwanafunzi wa Kitanzania katika ngazi zote za elimu Tanzania? Na kama kweli kuna misingi ya kisayansi kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia, kwanini haziwekwi wazi? Tuachokiona ni matangazo ya sekunde chache ya HAKIELIMU kwenye TV ambayo kwa maoni yangu yanamfanya kijana wa Kitanzania ajihisi na kuamini kwamba hana uwezo wa (a) kuijua lugha ya Kiingereza; na (b) kujifunza kwa lugha ya Kiingereza! Jambo ambalo kwa maoni yangu si kweli na linatudhalilisha kama taifa mbele za ulimwengu wa sasa!
Hakielimu kupitia tangazo hili wanauambia umma wa Watanzania na dunia nzima kwamba kijana mwanafunzi wa Kitanzania yuko kama hao kwenye tangazo lao!

Mwanafunzi wa chekechea au shule ya msingi anapata ujumbe gani anapoona tangazo hili kama sio kumkatisha tamaa kwamba 'HAWEZI' badala ya kumtia moyo kwamba 'ANAWEZA' ?

Lakini sina hakika kwamba tangazo la Hakielimu linatokana na utafiti wa kisayansi kuhusu uwezo au hapana wa watoto wote wa Kitanzania kujifunza Kiingereza na kujifunzia masomo mengine kwa lugha ya Kiingereza.

Na kama kuna utafiti wa kisayansi kudhihirisha maudhui ya tangazo la Hakielimu, lazima tujiulize kwanini watoto wote wa Kitanzania washindwe kufundishika na kujifunza kwa lugha ya Kiingereza? Wana kasoro gani?

Naamini pia kwamba wafadhili wa tangazo hili la Hakielimu wana ajenda zao kuhusu mwelekeo wa elimu yetu ambazo binafsi nazitilia mashaka kwasababu kuna tofauti kubwa kati ya haki ya kupata 'elimu' na haki ya kupata 'Elimu Bora'.

Kama tangazo la Hakielimu lingeonyesha mwanafunzi mmoja akilalamika haelewi na mwenzake akimwambia akazane tu ataweza; ningekubaliana nalo. Mafanikio ya mwanafunzi darasani ni lazima yategemee bidii yake na ya mwalimu. Siyo kufanya tendo la kujifunza darasani kuwa kama mahali pa gumzo la eti Kiingereza kigumu, hesabu ngumu nk.

Lakini vile vile lazima tujiulize kwanini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanaohubiri Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia wengi wao wanapeleka watoto wao kwenye English medium schools? Lengo lao hasa kuhusu sera ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni kuboresha elimu yetu au kutulaghai ili watoto wetu wapate "bora elimu" badala ya Elimu Bora?

Baadhi ya hoja za Freeman Aikaeli Mbowe kuhusu Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia badala ya Kiswahili ni taarifa alizonazo kuhusu uwezo wa Watanzania kushindana na wengine katika masoko ya ajira nje ya Tz na shughuli za kibiashara/kiuchumi katika nyanja za kimataifa. Kwa mujibu wa FAM lugha ya Kiingereza ni kikwazo kikubwa kwa Watanzania kuingia kwenye masoko ya ajira katika nchi kama Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, South Africa nk na hata Ulaya na USA nk.

2. Misingi ya Kisiasa.
Hoja yangu binafsi na naamini haitofautiani na msimamo wa FAM; ni kwamba sera za Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kama lugha ya kufundishia, misingi yake ni ya Kisiasa zaidi kuliko kisayansi. Na hapa ndipo chanzo cha udhaifu wa sera rasmi ya Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kuwa lugha pekee ya kumfundishia mwanafunzi wa Kitanzania.

Kama nilivyosema hapa juu na FAM pia alisema hivyo katika hotuba yake; kwamba baadhi ya wanasiasa na viongozi wa Serikali wanaohubiri Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia wengi wao wanapeleka watoto wao kwenye English medium schools. Lazima tujiulize kama watu wa aina hii (wanafiki) wanawezaje kutunga sera sahihi ya elimu yetu? Watu ambao unafiki wao unafanya iwe lazima tuwe na mashaka kuhusu elimu yao; na kwanini tusiamini kwamba lengo la sera yao ya Kiswahili kuwa lugha pekee ya kumfundishia mwanafunzi wa Kitanzania ni kumdidimiza ili kundi hili la wanasiasa liendelee kutawala?

Ushahidi uko wazi! Watawala wetu hivi sasa wanaendesha Serikali kupitia wanachosoma mafichoni au kusikiliza katika Twitter, Clubhouse, Maria Spaces nk. Sisemi kwamba wasifauatilie kinachoendelea huko lah! Lakini mahali pao sahihi pa kujadili sera za nchi ni bungeni. Kule wananchi na dunia itawaona na kusikia hoja zao na kuzipima kama zinafaa au sivyo.

4. Misingi ya Kiutamaduni.
Kwakuwa nimeshajadili kuhusu lugha ya Kiingereza kuwa kikwazo kikubwa kwa Watanzania kuingia kwenye masoko ya ajira nje ya Tz na shughuli za kibiashara/kiuchumi katika nchi kama Kenya Uganda Zambia Zimbabwe na USA na Ulaya ya Magharibi; naona vema nirukie kwenye misingi ya Kiutamaduni kuhusu Kiswahili au Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia.

Kuna watu wanataka tuamini kwamba Kiingereza ni lugha ya wakoloni kwahiyo kuendelea kuitumia katika elimu yetu ni utumwa, na ni kitendo cha kutoienzi lugha ya Kiswahili na utamaduni wetu!

Sikubaliani na fikra za aina hii. Kwasababu ni upotoshaji mkubwa kusema katika dunia ya sasa Kiingereza ni lugha ya wakoloni kama ilivyokuwa miaka 60 iliyopita! Kiingereza ni lugha ya kimataifa. Na kwa nchi nyingi duniani.

Zaidi ya Canada, Australia, New Zealand na Marekani, na nchi za kiafrika kama Zambia, Malawi, South Africa, Botswana, Namibia, Liberia, Ghana nk huwezi kusema kwakuwa wanaongea Kiingereza ni watumwa wa Uingereza!

Wasomi mashuhuri wa kiafrika kama Whole Soyinka, Chinua Achebe na wengine wa Nigeria, halafu Akina Okot Bitek wa Uganda, wanasifika kwa kuutukuza utamaduni wa kiafrika kupitia lugha ya Kiingereza! Kinyume na wanavyohubiri wanasiasa wetu kwamba Kiingereza kinaua utamaduni wetu.

Kwanza hatuwezi kukataa kwamba ukitaka kukabiliana na adui yako lazima ujue mbinu na mipango yake. Huwezi kufanya hivyo bila kuijua lugha yake! Na kwa mantiki hii ukitaka kujua mbinu za ushindani kwenye dunia ya sasa katika elimu, maendeleo, biashara, sayansi, nk, lazima ujifunze lugha inayotumika kimataifa, iwe Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani nk. Kufanya hivyo sio utumwa. Wala si kuabudu utamaduni wa wengine. Kwani sisi tunapowafundisha Kiswahili Wamarekani au Wanaijeria tunataka wawe watumwa wetu?
Au kuna mtu anaamini hao watu wakijua Kiswahili watasahau au kudharau utamaduni na mila zao?

Katika kudhani kwamba sera za Serikali ya JMT kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni kuenzi utamaduni wa Watanzania; lazima tujiulize kwanini wanaojiita "wasomi" na vijana wa kizazi kipya wanaiga tabia za "wazungu" katika muziki, mavazi, urembo, na lugha na mambo mengine kadhaa majumbani mwao, na katika maeneo ya starehe nk?

Ukweli ni kwamba hatuwezi kujitenga na dunia ya sasa, kiuchumi, kielimu, kisiasa na kiutamaduni. Kama kuna mtu anadhani anaweza kuzuia Tanzania isiwe sehemu ya dunia anachojaribu kufanya ni sawa na kuzuia upepo kwa mikono yake! Haiwezekani!

Mwisho napenda kuomba tuache kufanya elimu ya watoto wetu kama sehemu ya kujifunzia kutunga sera za elimu kila awamu moja baada ya nyingine kwa lengo la kuongeza ufaulu wakati viwango vinashuka. Hatuwatendei haki vijana wa familia za hali ya chini. Badala yake tunazalisha matabaka ya wahitimu feki na wataalamu wa vyeti na madokta magumashi.
Nimekuelewa vizuri: Ukiitaka kumshinda adui lazima ujue mbinu anazotumia ktk mapambano. Kujua lugha yake ni mwanzo mzuri wa kujua mbinu zake.
 
Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
2,680
3,780

Waalaykum salaam
 
Internet-Money

Senior Member
Apr 20, 2021
157
283
Ni Jambo ambalo haliwezekani,
Tutenganishe siasa na mambo muhimu.
Usitake kufananisha kichina , kikorea , Spanish , french na lugha ya kiswahili
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom