SoC03 Jinsi ya kuwa na Elimu yenye mafanikio kwa nchi ya Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Folk Part II

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
294
332
Elimu ni nini? Ni ujuzi ambao kitu chochote au mtu yeyote mwenye ufahamu anaupata ambao atamsaidia katika maisha yake ya kila siku. Unapopata ujuzi katika maisha ni moja ya njia ya kujikomboa na kujua nini kifanyike katika mazingira yanayokuzunguka. Ukiwa na ujuzi wa elimu mbalimbali hapa duniani itakusaidia kujua mambo mengi yanaendaje katika dunia na ni kitu gani kimefanyika mpaka unakiona kitu fulani kipo duniani. Kwa mfano ukiwa na ujuzi wa vifaa vya umeme itakusaidia kujua kwa nini spika ya redio inaongea au ni vitu gani vinafanya spika kuwa na mdundo mkubwa na sheria gani inatumika kutengeneza spika mpaka inatoa sauti. Spika nyingi zimetengenezwa kwa sumaku ngumu na sumaku ya umeme ambayo inatengenezwa kwa kutumia waya wa kopa ambayo huongezeka umeme unavyoongezeka.

AINA ZA ELIMU
kuna aina mbili za elimu
1. Elimu isiyo rasmi
2. Elimu rasmi

ELIMU ISIYO RASMI
hii ni elimu ambayo mtu anaipata kwenye maisha yake ya kila siku. Kwa mfano mtoto kujifunza kuongea, kujifunza kubeba kuni kupitia kwa mama. Na hii ndo elimu pekee ambayo inafanywa na binadamu pamoja na wanyama.

ELIMU RASMI
Hii ni elimu ambayo mtu huipata kupitia taasisi zinazohusika na utoaji wa elimu husika. Kwa mfano shule, kambi za kijeshi, hospitari, mashirika binafsi na taasisi zinginezo.

Elimu isiyo rasmi na elimu rasmi zote kwa pamoja zinahitajika sana katika jamii zetu. Elimu isiyo rasmi kila mtu huwa anaipata lakini elimu rasmi huipata watu wachache na wengine kuishia njiani kutokana na mifumo ilivyo. Elimu rasmi kuna taasisi huwa kuna mitihani ambayo ni kikwazo kwa wengi na hufanya waishie njiani. Lakini kwenye maisha ya kupata maendeleo hazihusiki moja kwa moja, wapo waliofanikiwa kwa elimu isiyo rasmi na wapo waliofeli pia na wapo waliofanikiwa kwa elimu rasmi na wapo waliofeli kimaisha pia, cha muhimu kujiongeza.

MATATIZO YANAYOIKUMBA ELIMU RASMI HAPA TANZANIA KUTOKUWA NA MAFANIKIO

1. Ni elimu inayoamini sana katika vyeti
Hivi umewahi kujiuliza kwanini tanzania kuna maprofesa wengi lakini hujawahi ona bidhaa mtaani ambayo inazalishwa na kusambazwa kutokana na profesa kutengeneza icho kitu ili kisaidie jamii?
Ipo hivi mtu wa kawaida akifanya kitu ambacho hata huyo mwenye vyeti kafanya hawataweza kumwamini kutokana kwamba hana elimu ya kutosha kuhusu hicho kitu na hataweza kutunukiwa uprofesa. Kwa mfano kuna jamaa alitengeneza helikopita zanzibar leo hasikiki hata yuko wapi.

2. Ni elimu inayokutaka uende ngazi kwa ngazi
Au kwanini ili ufike kuwa profesa lazima umri unakuwa umeenda?

Huwezi kuwa profesa kama hauna shahada tatu na kuzipata hizo shahada zinahitaji muda mrefu sana.


3. Mifumo ya elimu rasmi
Je haiwezekani kupata uprofesa ukiwa na umri mdogo?

Jibu rahisi ni ngumu sana kupata uprofesa katika umri mdogo kutokana kwamba mfumo unakutaka uende hatua kwa hatua


4. Ni elimu inayomuandaa mtu kusujudiwa
Kawaida mtu akipata elimu hii ya ngazi ya juu hujiona ni mtu wa juu sana ambaye hawezi kuambilika na mtu wa chini wa elimu yake. Lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu wa chini yake wana mawazo mazuri sana ya kuendeleza ubunifu kuliko ata yeye.


5. Ni elimu ambayo inafundisha nadharia ambazo ata haziendani na wakati.
Walimu wengi au wafundishaji hutumia mwongozo unaowaongoza wawafundishe nini wanafunzi wao ambapo hicho kitabu cha mwongozo wao hutungwa na wadau wa elimu ambao hawajafanya hata utafiti kwamba mwanafunzi akisoma hiki kitamsaidiaje katika maisha ya kawaida.


6. Ni elimu ambayo inaubaguzi wa kifikira
Kwanini wenzetu wanaotengeneza vitu hivi kwa mfano mitandao ya kijamii unakuta ni watu wenye umri mdogo sana?

Mtu ambaye atapata elimu hii ya juu au rasmi huwa anaamini kwamba ili mtu mwingine avijue vitu kama vyake basi lazima apitie au ahenyeke kama yeye alivyohenyeka lakini wenzetu ni tofauti mmoja akipata elimu hii darasani wengine inabidi awafundishe wakiwa eneo la kazi hapa huchukuliwa watoto wanaojua kuandika na kusoma kiingereza au lugha ya taifa lao hata kama hawajui zile hesabu za kutafuta thamani ya x ilimradi tu anaonyesha kitu kwa kile ambacho profesa kasomea ndo mana unakuta ni mtoto mdogo sana lakini anajua na amefanya mambo makubwa sana na vinatumika katika jamii kuliko hata profesa wa bongo au Afrika.

7. Ni elimu ambayo ina mfumo wa vita kati ya mwalimu na mwanafunzi.
Elimu rasmi inavikwazo vingi sana ili uweze kufaulu na mtega vikwazo huwa ni mwalimu ili mwanafunzi avitegue. Mara nyingi mwalimu huwa anafundisha huku akificha mbinu za kujibia maswali ambayo yanakuja kwa mitego mikali ili aje awakamate kwenye mtihani. Nikili wazi kuna maswali ya mitego unaweza kutegua kwa kutumia ulichofundishwa lakini mengine ni ngumu sana kama hujawahi kuliona au kukutana nalo linajibuwaje. Wengi humu tumesoma haya maswali yalikuwepo ili ulijibu unakuwa umekalili tu. ili ujibu hili swali ukifika sehemu fulani unafanya ivi ukiulizwa kwanini unafanya ivo hata huna maelezo jibu lako ni kwamba ndo huwaga wanafanya ivoivo. Kwa mfano kuna kozi hii Thermochemistry niliisoma pale UDSM hata thermo ya fizikia ilikuwa cha mtoto sana. Na hii Stastical biology waliozipitia wanazijua ugumu wake.

MWONGOZO MZURI WA KUWA NA ELIMU RASMI YA MAFANIKIO

Ili tuwe na mafanikio inatupasa tuwe na vitabu vizuri vya mwongozo wa kufundishia. Wanaotunga hivi vitabu wawe ni watu wanaofikilia kesho ya taifa lao na kuendana na wakati uliopo wa sayansi na tekinolojia na sio hawa wanaong'ang'ania elimu ifundishwe kwa kiswahili wakati huohuo hawafikilii kwamba bidhaa nyingi hawatengenezi apa wanaziingiza kutoka mataifa ya nje ambapo maelezo ya mwongozo wa matumizi wa hiyo bidhaa ni lugha ya nchi husika na kingereza.

Pili tutengeneze mazingira ya hawa wanaopata uprofesa wawe wanafanya tafiti zenye tija kwa jamii fulani na ikiwezekana kwa taifa nzima. Kwa mfano tutengeneze viwanda ambavyo wakifanya tafiti yao iwe ni moja ya bidhaa katika kiwanda icho na sio kuwapa uprofesa kwa maandishi ya makaratasi tu. Na msimamizi wake kukubali hii ni kweli wakati huku kwenye jamii hakina faida yoyote.

Tatu waliosomea vitu vikubwa na wanauelewa navyo jinsi ya kuunda vitu chukua vijana wa fani mbalimbali wanaohusika na uundaji wa hivyo vitu vinavyounda kitu kimoja ili kuifanikisha iyo bidhaa tusiwe wabinafsi.

MWISHO

Unaweza kuongezea kwa masirahi ya taifa letu ningeendelea idadi ya maneno yaliyopangwa imefika mwisho.

Ni mimi Folk Part II

Ubarikiwe sana

Naomba kura yako kwa kubonyeza Vote hapa chini
 
Back
Top Bottom