Ludovick Utouh: Hatuwajibiki Kumshukuru Rais, Kujipendekeza Hakutusaidii

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Ludovick Utouh amesema sio sawa kwa Watu kumshukuru Rais kwasababu anachokifanya ni Uwajibikaji na Fedha zinazotumika ni Fedha za Serikali na sio za Mtu.

Amesema "Kama kushukuru inabidi Kuishukuru Serikali lakini sio mtu, na sasa hivi kuna tabia ya kijikomba na kujipendekeza ambayo haitupeleki mbele inaturudisha nyuma. Pale kwenye ukweli tuseme ukweli, tusiweke Chumvi na tusigope kusema, tusiwe wachochezi".

Akielezea dhana ya Uwajibikaji, amesema ni Usimamizi wa Mahusiano kati ya Serikali na Wananchi kwa kutoa Taarifa Muhimu kwa Wananchi na huo ndio Uwazi kwasababu Wananchi wana Haki ya Kujua.
 
Kwa hiyo kwa haya mawazo yake ya kutomshukuru Rais anataka kutuaminisha kuwa Rais si taasisi tena bali ni mtu!
Ajitafakari !
 
Wangekuwa wanaume kweli wangesema hayo mbele ya JPM,Kwa sasa midomo mirefu kama imedonolewa na nyigu
 
ASANTE SANA CAG MSTAAFU BW LUDOVIC UTOUH KWA KULIZUNGUMZIA HILI BILA KUPEPESA MACHO YANI HILI JAMBO LINAKERA SANA WANAMSIFIA UTADHANI NI HISANI AU PESA KATOA MFUKONI KWAKE

WATANZANIA TUBADILIKE HASA VIONGOZI YANI WANAONA WASIPOMTAJA TEUZI ZITAWAPITA PEMBENI KITU AMBACHO SIO SAWA SANA SANA WANAONYESHA LEVEL YA JUU KABISA YA KUJIKOMBA

HILI TAIFA SIJUI HATA LINAKWENDA WAPI

INASIKITISHA SANA.
 
Kasema ukweli kabisa.wtz kwwnye ukweli tuseme ukweli.na mimi nasema uuzwaji wa bandari na mikataba mingine yenye utata kama wa LNG Ni upuuzi mtupu ambao hauna tija kwa taifa.
 
Yalianza na awamu ya 5 yataendelea hadi atapojitokeza atayekataana kukemea
 
Kweli inatiakinyaa sana yaani iwe kupokea mwenge, hafla ya kitaifa, ufunguzi au uzinduzi wa mradi unakuta lijitu na mav*zi linakazi ya kujikombakomba tu utasikia
"pongezi za dhati ziende kwa rais wetu mama yetu Mheshimiwa Daktari Mama S.S.H kwakufanikisha suala hili"
Jamani suala la usalama, umeme, maji, barabara, huduma bora za afya sio hisani ni wajibu wa Serikali kuyafanya haya maana pesa haitoki mfukoni kwao ni hizihizi kodi zetu wanazotulima kila uchwao.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Ludovick Utouh amesema sio sawa kwa Watu kumshukuru Rais kwasababu anachokifanya ni Uwajibikaji na Fedha zinazotumika ni Fedha za Serikali na sio za Mtu.

Amesema "Kama kushukuru inabidi Kuishukuru Serikali lakini sio mtu, na sasa hivi kuna tabia ya kijikomba na kujipendekeza ambayo haitupeleki mbele inaturudisha nyuma. Pale kwenye ukweli tuseme ukweli, tusiweke Chumvi na tusigope kusema, tusiwe wachochezi".

Akielezea dhana ya Uwajibikaji, amesema ni Usimamizi wa Mahusiano kati ya Serikali na Wananchi kwa kutoa Taarifa Muhimu kwa Wananchi na huo ndio Uwazi kwasababu Wananchi wana Haki ya Kujua.
Mzee Utouh nimekuelewa asante Kwa uwazi wako. Juzi Mwigulu analalamika Bungeni kwamba kuna watu Kodi zikiwekwa wanaziita Kodi za Samia na wengine Kodi za Mwigulu. Lakini ni huyu huyu na kundi lake Serikali ikitoa fedha hizo hizo za Kodi kugharamia miradi wanaziita fedha za Samia.
 
Kwa unakuta mtu mzima na usomi wake anasema: Tunamshukuru Rais kwa kutuletea fedha za ujenzi zahanati!
Badala ya kusema tunaishukuru serikali ya CCM chini ya Rais_ kwa kutuletea fedha za ujenzi wa zahanati.
Rais hatoi fedha zake mfukoni mwake, hizo ni fedha za umma, ni kodi zetu,yeye Rais ni msimamizi tu.
 
Back
Top Bottom