Ludovick Joseph: Kilio cha usaliti - Sehemu ya pili

Ludovick Joseph: Kilio cha usaliti - Sehemu ya pili

Heading inasema Ludovick Joseph while content inamzungumzia Deus Mallya,nawashauri CCM wangewatumia watu wengine wangeweza kuwashawishi watu lakini hawa Shonza na Mwampamba hata kujieleza hawawezi,hawaijengi CCM
Arsenal mnacheza lini?
 
JF...naomba niseme hivi, nguvu anazotumia Mtela hapa JF na kwenye Facebook kuandika haya yote, anasutwa na video aliyoiweka ya Lwakatare, naanza kuamini kwamba yeye anahusika 100% kuweka video ile. Aliiongelea sana na ni wazi ameshiriki kuitengeneza maana anaonekana anajua mambo mengi kuhusu mbinu zote alizofanya na waliomtuma.....inabidi awekwe ndani mpaka upelelezi utakapokamilika.
 
Naomba uwabainishie
Umma wa wanaJF kuwa lipi katika niliyoyaandika hapo juu si sahihi
kuhusiana na DEUS na kukanwa kwake na watu hao. Na kwa bahati nzuri
hatukuwa tunafanya mazungumzo ya mdomo pekee, ninazo meseji za simu na
hata kauli za Mallya kwenye inbox yangu ya facebook yanaeleza haya
niliyoyaeleza hapa.

Naomba kabla haujachelewa na kuonekana ni miongoni mwa wenye ukame wa
fikra, njoo hata kwa kutunga uongo wako ubainishe ni kipi si sahihi ama
ni uongo katika hayo niliyoyaandika.

Mwampamba: Hivi ulitokaje cdm? Kuna jamaa hapa wanabisha, nawaambia na wewe ulitoka cdm kama Kamanda Mawazo alivyotoka ccm. Hebu tusaidie mkuu tumalize ubishi.
 
Tabia kama hii anayoionyesha mtoa mada, ni hatari sana. Haina tofauti sana na blackmaillers...siku zote, dawa ya blackmailers inajulikana... Sasa kwa wanasiasa kama yeye, tena wachanga, ndiyo anajiharibia zaidi, si CDM si CCM. Kwa CCM, anaji expose sana weakness yake hiyo kuwa akija kuhama CCM, hicho ndicho atakachokifanya...kusema yale ambayo hakuweza kuyasema alipokuwa CCM...na hapo ndipo atakapokumbana na wazoefu...
 
Mkuu watakutana sana lakini usichoke mwishowe watanyamaza na hakika watanzania tutakuwa tumefunguka na kujua hasa malengo ya CHADEMA katika msatakabali wa taifa letu.
Mimi ni kijana sijaona cha kunifungua hapo,ila ninachojua sasa hivi hatutawaelewa kabisa ukichukulia nchi yetu bado ni masikini,watanzania wanahali ngumu kimaisha lakini hawa wapumbavu ambao tuliwaamini,kama wapambanaji wanataka kuturudisha kule tuliko toka,kwa kutushawishi tuihurumie ccm,inamaana kuwa wewe Mwampamba,unaweza kutuaminisha kuwa wewe unatuonea huruma sana vijana tulioko CHADEMA?Ama kweli nyani halioni kundule.Jitafakari na dhambi hii muliyoifanya kwa CHADEMA na huyo mke wako shonza,ndipo utushawishi na sisi.
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa CCM ndiyo mahali bora kwa vijana wa Kitanzania? Ulipokuwa mpiganaji CDM ni nini ilikuwa imani yako? Kuwa CCM ni safi na inafaa kuongoza taizfa hili? Si ni wewe uliyekuwa unaitukana CCM kwamba chama cha mafisadi? Je ufisadi wao umekwisha? Wala usiwaogopeshe vijana kwa sababu ya makosa madogo madogo ya kibinadamu. Nchi hii inahitaji ukombozi na huo hautaletwa kamwe na chama chako (CCM), najua hata dhamiri yako inakuambia hivyo, isipokuwa njaa ni mwanaharamu, ameondoa uanaharakati wako kabisa na kuungana na mafisadi.

Historia itakuja kukuhumu hivyo. NO MATTER WHAT, THE FREEDOM IS COMING TOMORROW.
 
Mimi naona hoja za Mwampamba zina mashiko sana, na kwa wale vijana na watu wanaoona Mwampamba anatapata hapa wamelamba galasa. Mtela kabadirika sana kwa sasa anakuja na hoja za maana zinazoamsha fikra na mawazo ya vijana kujitambua. Kuna thread iliwahi kuletwa humu kwamba Mtela Mwampamba na Juliana Shonza ni watu hatari sana kwa ustawi wa Chadema watu watu wakachukulia mzaha.

Pole tena pole sana! Hivi unahitaji uambiwe na nani ndo ujue mwandishi wa habari hii sio Mwampamba?
 
Kondomu huwa haitumiki mara mbili,nenda lumumba kachukue fedha ya msosi manake njaa tupu hata mbeya kwenyewe hutaki kwenda kwa dhambi ya kusaliti umma!!
 
Yuo want to be a gentlemen! Avoid cricsms! Umekosa hekima, na mwisho wa siku utakuwa trash! Ona mbele, tafakali!
 
... ............................ Mfikirie na m'Tanzania wa kawaida anaye hitaji ukombozi toka hali mbaya tuliopo sasa!

Mtela Mwampamba ni mnafiki na mbinafsi wa kutisha, nimeishawahi kuhudhulia mkutano wake mmoja wakati wa kampeni za mwaka 2010 nikiwa kikazi Mbeya, huyu huyu @Mtela Mwampambwa alinifurahisha sana namna alivyoweza kujenga hoja ni kwanini anaichukia CCM na ni kwanini anaamini haitakiwi kabisa kuwepo madarakani, alitoa mifano mingi iliyomfanya aingie katika vita vya kupambana na CCM.

Moja kati ya facts nyingi alizozitoa dhidi ya CCM ni jinsi ambavyo amekuwa akishuhudia vifo vya wajawazito na vifo vya wagonjwa ambao kimsingi wanakufa kutokana na huduma mbovu, alitoa kisa kimoja cha mama mjamzito aliyefariki akiwa njiani kuelekea kituo cha afya kilicho mbali sana na wakazi, akawaeleza wananchi kwamba CCM ingepunguza ufisadi hata kwa 10% tu maisha ya maelfu ya watanzania wa kipato cha chini waliofariki wangekuwa hai kushiriki katika ujenzi wa Taifa, hii statement iliwafanya watu wengi watokwe na machozi na kufurahia kwamba idadi ya wakombozi inazidi kuongezeka.

Kwanini namuita Mwampambwa ni mnafiki na mbinafsi? Mwampambwa alikuwa hana nia ya kupigania Taifa na kuwakomboa wanyonge kutoka katika makucha ya kifisadi ya CCM, mimi nilitegemea badala ya Mwampambwa kwenda CCM angeenda NCCR Mageuzi, TLP nakadhalika, hii ingeonyesha kwamba bado nia yake ya kuwakomboa Watanzania ipo pale pale kilichotokea ni kwamba kwa bahati mbaya katofautiana kifikra na wapambanaji wenzake(CHADEMA).

Hivi Mwampambwa atawaambia nini wale wananchi waliotoa machozi kwa kuguswa na kauli zake dhidi ya CCM? Je atawaambia ameenda CCM baada ya kugundua wamejirekebisha au atakiri kwamba alikuwa anawadanganya? AU atawaambia nayeye alikuwa anaburuzwa na viongozi wajuu ili wafikie malengo yao? Naomba Mungu nimshuhudie tena Mwampambwa akiinadi CCM pale Mbeya akiwaomba kura walewale wapiga kura.
 
Kwa hiyo wangwe? CDM? Aisee
Hii muvi hii kali sana.

Hii movie ya Kihindi, waigizaji ni Wachina, inachezewa Hollywood, Ma-director ni akina Ray na JB na producers wametoka Northwood "Nigeria"
 
Mtela Mwampamba... Kusema kweli haijalishi kama haya ni kweli ama ni uongo. Inachojalisha ni kuwa wewe ndiye umeyatoa, baada ya kuwa mwana CCM baada ya kushindikana kuwa mwana CDM. Kwamba siku zote uliona sawa kumezea na sasa ndiyo wakati wa kuyaanika?

Kwa mwananchi yeyote atakae kuwa anatumia habari hizi ama Siasa za gutter politics zinazotumika kama kigezo pekee cha kuki judge Chadema atakuwa bado ni mchanga katika kutambua vigezo vya kuchagua chama na ni dalili ya kuwa ndiyo wale washabiki hata kura siku ya mwisho hapigi!

Hakuna Chama kisicho na madhaifu, kama ilivyo Chadema na madhaifu yake... Ila hii nguvu na devotion yenu juu ya Chadema na Viongozi wake inatupa walakini wa nia yenu huku ikitoa picha ya woga mkubwa mlio nao juu ya Chama na viongozi wa Chadema.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa inafanywa na vijana ambao wanawaza kuwa tegemezi katika taifa kwa kuwawakilisha wananchi ipasavyo badala ya kukesha kila siku kwa kuwaza namna ya uharibifu na uteketezi wa chama kingine! Punguzeni selfshness jamani... Mfikirie na m'Tanzania wa kawaida anaye hitaji ukombozi toka hali mbaya tuliopo sasa!


Asante Bibie kwa Ushauri mzuri kwa vijana wa staili kama hii.

Na wasiwasi Kijana huyu kama akili yake iko sawa sawa!.Haitatokea kamwe akaaminiwa tena sehemu nyingine isipokuwa kwa wenye mapungufu ya kufikiri kama yeye baada ya kujianika kuwa yeye ni mtu wa aina gani katika Jamii.

 
Kwahivyo hoja anayoijenga MTELA hapa ni kuwa Ludovick ni mtu wa Chadema na amesalitiwa sio?
 
....kama haya yote uliyajua ulikua wapi mbona hukuyasema tangu awali? Endeleeni na Research zenu mkishindwa kufanya Analysis tuiteni.
 
Mtela Mwampamba ni mnafiki na mbinafsi wa kutisha,

Hivi Mwampambwa atawaambia nini wale wananchi waliotoa machozi kwa kuguswa na kauli zake dhidi ya CCM? Je atawaambia ameenda CCM baada ya kugundua wamejirekebisha au atakiri kwamba alikuwa anawadanganya? AU atawaambia nayeye alikuwa anaburuzwa na viongozi wajuu ili wafikie malengo yao? Naomba Mungu nimshuhudie tena Mwampambwa akiinadi CCM pale Mbeya akiwaomba kura walewale wapiga kura.

Kwakweli huyu bwana hajatumia busara... ni sawa na ndege akiamka asubuhi unaponda kiota alicholala lakini ikifika jioni anarudi pale pale kiotani.
 
hata wakati KARL MAX anaandika maandiko yake alionekana kichaaa na punguwani! leo machapisho yake yanaheshimika na kutambulika nchi nzima! hongera kijana ipo siku wananchi watakumbuka ulichokisema, si mara ya kwanza chadema kukana vijana wake!

Mtake radhi Karl Marx. Usilinganishe ukahaba wa kisiasa na falsafa za kimapinduzi.
 
Mtela Mwampamba ningekuelewa vizuri sana kama ungeyasema haya mapema wakati ukiwa nao kwani sheria ingechukua mkondo wake...Napata shida kuamini kama hukuusika kwenye mipango ya kuwasaliti.
 
Back
Top Bottom