Lubuva na mikakati ya kuibeba CCM - tusilaumiane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lubuva na mikakati ya kuibeba CCM - tusilaumiane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Mar 26, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tunapozungumzia uchaguzi katika nchi yetu, tunatarajia uchaguzi uwe huru, wa haki usio na vitisho, wala usio na ghiliba. Uchaguzi usio na rushwa na wagombea wanaofuata maadili ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010.

  Licha ya sheria hiyo kutofuatwa na Chama cha Mapinduzi kwa kutumia mamilioni hata kabla uchaguzi haujafika, lakini pia kasoro nyingi zilizojitokeza mwanzoni wakati zoezi hili linaratibiwa, zinathibitisha kuwa mpindishaji mkuu wa mambo katika uchaguzi ni Tume ya
  uchaguzi.

  Kama kutatokea machafuko Arumeru katika uchaguzi unaolazimishwa kuwepo siku ya
  Jumapili Aprili mosi, 2012, basi Tume ya Uchaguzi itakuwa imehusika sana na kuchangia Watanzania kupigana, kuuana, au kusababisha madhara yoyote.

  Kwa muda uliopo tume haina nafasi ya kujikwamua katika lawama hizi. Imefanya yale iliyokusudia, na inakusudia kuyatekeleza. Nini hatima ya Watanzania katika Mazingira hayo?

  Tuchukue mifano miwili ya mambo ya kitoto kabisa ambayo hayakutarajiwa kuonenaka Arumeru, yaliyosababishwa na Tume ya Uchaguzi. Tume ambayo mimi ninasadiki inaongozwa na watu wasomi, wenye akili, tena waliobobea katika sheria.

  Hoja ya kuwa tume yetu ya uchaguzi imefanya marekebisho madogo katika daftari la jimbo hilo baada ya kujitokeza kwa wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya mara moja na baadhi yao kutokuwapo katika daftari la kudumu la wapigakura kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuchafuka kwa fomu wakati wa zoezi la uandikishaji. Ikumbukwe kuwa kabla ya uchaguzi, baadhi ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi katika Jimbo la Arumeru viliomba kufanya mabadiliko ya daftari la wapiga kura, lakini Tume ya Uchaguzi ilikataa na kusisitiza kuwa daftari litakalotumika ni lile lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Je, kauli hii waliitoa katika maana ipi? Kwanini sasa wamefanya mabadiliko katika daftrari hilo?

  Je, walipofanya mabadiliko hayo walishirikisha wadau gani wa daftari hilo la wapiga kura?

  Vyama vipi vya siasa vilishiriki katika maboresho hayo? Kama hakuna vyama vilivyoshiriki kufanya maboresho hayo kwanini tume imefanya zoezi hilo kinyemela?

  Haiingii akilini kwa njia rahisi kusikia kuwa baada ya marekebisho hayo daftari litakuwa na wapiga kura 127,455 ikilinganishwa na daftari lililotumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 lililokuwa na wapiga kura 127,429,” Hii ni kauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Lubuva. Kwanini idadi ya wapiga kura imeongezeka?

  Kama kulikuwa na kasoro kubwa za kuongeza wapiga kura wengi hivi kwa Jimbo la Arumeru ni majimbo mangapi ambayo tume imeongeza wapiga kura kinyemela kama ilivyofanya kwa Arumeru? Tungetegemea kuwa Jaji Lubuva angesema kuwa idadi ya wapiga kura imepungua kwa kuwa wamefanya maboresho kuondoa wale waliojiandikisha mara mbili, au waliokufa, au waliohama. Lakini hesabu ya Jaji Lubuva inajumlisha tu? Inaondoa waliojiandikisha mara mbili, inarekebisha wale ambao fomu zao zilichafuka, lakini idadi inaongezeka. Jaji Lubuva kwa hesabu za aina hii umechangia sana kuharibu uchaguzi
  unaotarajiwa kufanyika.

  Lubuva sema vizuri hao wapiga kura 26 umewaongezea kutoka wapi? Kwanini? Kuna uwezekano kulikuwa na kasoro kama ambavyo umetaka kutusadikisha, lakini kwanini kasoro hizo hazikufanyiwa marekebisho tangu mwaka 2010 hadi leo? Na kwanini marekebisho hayo yafanyike siku chache kabla ya Uchaguzi? Kwanini hamkuyafanya kabla ya kutangaza tarehe ya Uchaguzi ya Jimbo la Arumeru ili kuondoa shaka ya kudhaniwa vibaya kuwa mnapendelea mgombea fulani wa chama cha kisiasa kinachoshiriki uchaguzi?

  Nawasilisha.
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu watanzania wataka mabadiliko tena kwa hamu kubwa ila tutakuwa na uchaguzi wa huru na haki pale tutakapokuwa na tume huru ya kujitegemea lakin siyo ambayo imeteuliwa na raisi wa chama cha mapinduzi
   
 3. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ndio maana tunasema tume hii inapokea maagizo kutoka kwa viongozi wa ccm,hapo wakuu hakuna uchaguzi kunakupotezeana wakati tu upuuzi kama huo vyama vya upinzani vinaukubalije kirahisi namna hiyo kulalamika tu bila kuchukua hatua kali hakutasaidia lolote kwa Cdm dawa ni kulianzisha mapema kama watagoma Cdm kulichunguza kwa kina hilo daftari la uchaguzi.
   
 4. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mimi nafikiri baada ya huu uchaguzi wa Arumeru ni vema CDM wakakadi kuhakikiwa kwa daftari la kupiga kura.
   
 5. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Punguza riwaya,
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  KWA HALI iliyopo Arumeru SASA, jeuri za kitoto za kuongeza watu 26 hazitasaidia kitu, maana tayari kule washaikataa ccm waziwazi!
   
 7. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  ODINYO, vipi tena? unaijua riwaya?
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Kwa nini iwe baada ya huu uchaguzi na sii kabla?
  .
   
 9. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Damu za Wameru zitakazomwagika ni kweli kwa 75% zitakuwa na tume na zilizobaki kwa Lowasa ambaye anang'ang'ania mkwe apite kama vile mtu alioa anavyohangaika na kupata mtoto!!!!!
   
 10. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Makamanda wapo vitani nafikiri ni wakati muafaka kumaliza hii vita dhidi ya manyangau na itatupa dira ya hali halisi then tunapokuja kwenye madai inakuwa tunayo referance ya arumeru.

  Pia wadau wa mabadiliko tujiandaye hii miaka mitatu itakuwa ni ya changamoto kubwa sana kwa upinzani.

  CCM wanajipanga kurudisha majimbo yaliyopotea kwa ngarama yoyote na mikakati hiyo imeshaanza.

  Niwakati muafaka kujipanga na kuweka mikakati ya kichama kuhakikisha majimbo hayaendi ccm kuliko kuwaachia wagombea wao pekee yao.
   
 11. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hii vita inabidi tupambane pamoja dhidhi ya hawa wanaizaya wa kijani/njano
   
 12. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
   
 13. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,163
  Likes Received: 10,365
  Trophy Points: 280
  Kila siku nasema hawa CCM hapo walipo hawataweza kutoka kwa amani bila ugomvi na kwa kuwa wanaotaka mabadiliko ni vijana hamna cha kupoteza maana hawana hata ajira na wanaowaharibia maisha ni hao wanaong'ng'ania madaraka. Ni kulianzisha tu watu lazima tutaheshimiana. Hawa majaji uchwara wa tume njaa zinawafanya washindwe kusimamia taaluma yao wanabaki kujipendekeza kwa viongozi tena wenye elimu ya vyeti vya bandia. Na kama sikuona watu ni wajinga iweje watu wanaojiita wana elimu kwenda kugawa mahindi wakati wa kura na huyo anayejifanya msajili wa vyama vya siasa yuko kimya halafu wanataka tuamini nchi inafuata utawala wa sheria.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Enyi MAFISADI wote pamoja na chama CCM eleweni hili vema na kwa uwazi wake wote, ukweli wote ni kwamba;

  ... WaTanzania sote TUMESHAAMUA kwamba mambo yote ya ukombozi wa MTANZANIA kuondokana na MAFISADI ni kwa CHADEMA.

  Je ni nani tena wa kutuzuia?????????????
   
Loading...