Lowassa, wananchi wanakuhitaji zaidi ya unavyowahitaji wewe

Lowassa, wananchi wanakuhitaji zaidi ya unavyowahitaji wewe

Mbona majibu tayari mnayo,fuatilia sakata la pesa za account ya escrow utajua ni nani yuko behind the issue of richmond,msiwe tomaso jamani,just streach ua brain a little bit

Tatizo letu watanzania akili zetu zimefungwa na viongozi walio ngazi za juu kwa kutuaminisha kuwa hawawezi kujihusisha na kashfa wakati wanatajwa
 
Umeandika vizuri lakini umehitimisha VIBAYA. Wakati nchi inatawalika CC ya CCM haiwezi kupitisha jina la Lowassa. Lowassa atachiniiwa baharini na CC ya CCM. Kwasababu CCM inaamini kwamba hata ikimsimamisha Dr. Hamis Kigwangallah (no pun intended) atashinda tu. Na hata kama hatashinda basi atashindishwa na NEC.

Labda lowasa wamuue tu lakini kama lowasa anataka urais ataenda chama chochote cha siasa na atapata urais
 
Edward Lowassa ni fisadi na mpenda rushwa aliyebobea hivyo hafahi kuwa rais wa JMT na isitoshe afya yake ni mgogoro watu kama yeye hawastahili kuingia ikulu watanzani wote makini wanajua hilo.

Wewe huna haki popote pale kudhibitisha afya ya mtu yeyote kama siyo doctor
 
gado=ugonjwa wa kutetemeka (parkinson's)?
Wewe Lekakui huujui ugonjwa huu hatari wa neva uitwao Parkinson's unaomsumbua Lowassa.Wewe unasema Satta ndiye
alikuwa mgonjwa? Tumia muda wako kumwombea Lowassa apone ugonjwa huu hatari badala ya kumnadi eti ni rais afaaye nchi hii! Kwa nini unamtakia Lowassa mabaya?

Ugonjwa wa kutetemeka na ukimw ni upi ulio hatari zaidi?
 
Last edited by a moderator:
Wewe huna haki popote pale kudhibitisha afya ya mtu yeyote kama siyo doctor

Ni daktari wa mgonjwa tu ndiyo mwenye authority ya kuelezea ugonjwa wa mtu. Hiyo ndiyo ethics, sasa hawa wanaosema afya yake ni mgogoro hawajui.wasemalo...
 
1.lilipokuja suala la kujenge shule za kata lowassa alilisimamia kwa nguvu na kuna viongozi wengi tu waliwajibishwa walipoonekana kulega lega ktk kulisimamia jambo hili. ni lowassa ambaye kipindi kile alifanya Serikali ionekane ipo tofaut na sasa ni kama imelala usingiz wa pono. Wazir mkuu alikuwa kazini hasa toka mkoa hadi mkoa,wilaya hadi wilaya,kitongoji hadi kitongoji.alionekana akisimamia sera kwa vitendo na pasipo masikhara.katika ili ashakum si matus kuna ambao walikutwa fagio la chuma kutokana na kuwa na utendaji usio Mujarab na fanisi .hili lilifanya shule za kata zijengwe kila sehemu na tumeona zimejengewa na zikaishia hapo toka alipotoka.maana mkakati uliokuwa unafata ilikuwa ni kupeleka walimu huko,pia kujenga vituo vya afya kila sehemu.maskini hili halikufanyika baada ya yeye kujiuzulu.
2.mimi ni mtu mdogo sana kumfanyia kampeni Mh Lowassa. yeye haihitaji kampeni na tunapomwongelea tunamwongelea kwa sabau ni Public Figure na huu ni mtizamo wa sisi vijana wengi ambao sasa tumeelimika na kuuona ukweli.sisi tuliofumbuka macho tukajua propaganda za akina sitta,pinda et all. baada ya kugundua wanamchafua kuficha udhaifu wao tumeamua nasi kusimama kuona Mh huyu Rais Mtarajiwa haachwi peke yake. propaganda is spread over his name.... we cant just sit na kumwacha awe yatima wakati tunajua yeye si yatima ana vijana wengi sana walio nyuma yake.Mimi sipo chama chochote, bahati nzuir au mbaya sipati chcochote na hata hanifahamu mh huyu. faida nitakayopata si yangu peke yangu,hata wewe utaipata ndugu yangu.tunataka rais ambaye atachapa kazi atakuwa serious na asiyependa masikhara.
3. kuna sheria gani nimevunja? hebu nitajie kifungu hicho cha sheria ndugu yangu ili sasas nami niwajibike.maana watanzania huwa mnakurupuka tu mnasema mtu kafanya jambo flan. kama ambavyo mnasema fisasi aalmost miaka 5 sasa.kama unaifaham vizuri sheria si alitakiwa kushtakiwa huyu? maana hapa tu umetoka kunambia nmevunja sheria ingawa hujataja sheria gani basi kama lowassa alivunja sheria huoni alipaswa kushtakiwa ? kampen gani zinazofanywa hapa? haya ni maoni ya watu huru ndugu yangu. kusema flan anafaa kuwa rais ni maoni yangu huru na ni kama wewe kabla ya kuoa au kuolewa unawaza.uliwaza au utawaza kuwa huyu anafaa kuwa mke au mume.hapo hujaenda toa mahari bado.so nikilinganisha na watu wote waliopo na wataokuja huyunndiye anayefaa kuwa Rais kwa sasa na miaka mingine 5 ijayo.
hili taifa kweli halihitaji mzaha kama ambao tulifanya miaka 10 hii. sasa tunahitaj kuwa serious na tunataka mru seious.
 
Nyie watu hamna Akili kweli , huyu mzee mamvi anataka nini ? Kama kufisadi kafisadi tayari , si atulie akale pesa zake.!
Anataka kuiba mpaka lini
?

Kama ni rais msafi ki hivyo basi atoke nje ya ccm, lakini kama anatoka ccm basi afadhali huyo lowasa
 
TUMETESEKA SANA,TUMENYANYASIKA VYA KUTOSHA,MUNGU AMETUPA NAFASI TUJITETEE, Tusifanye Makosa Kwenye Utetezi Wetu Hapa Ni Tumaini Letu E. N. Lowasa Au Dr. W. P. Slaa
 
Ukweli halisi ni huu hapa wakuu wala msihangaike bure:

Hata kama wapinzani watashinda kwa kupata kura zote hawawezi kuingia magogoni! Magogoni ni kwa ajili ya ccm baasi. Wapinzani baadae sana, sio sasa wakati bado nchi inatawalika. Wapinzani wataingia ikulu pale ambapo nchi haitawaliki lakini si kama ilivyo sasa hv! Niwakumbushe kulalamika lalamika haina maana kuwa nchi haiendi, inaenda sana tu! Si mnakumbuka ishu ya mzee wa vijisenti?Au mmeshamsahau mara hii? Mlilalamaika weeeee lakini juzi kai mzee wa vijisenti ndo anawaandikia katiba! Mpo hapo?

Hii nchi ni ngumu kwa wapinzani!! Kuna mengi hamjui, ila wanajitahidi sana lakini bado kabisa.

Dawa hazipatikani hospitali, wananchi wapo busy na foleni za kuwahi kibaruani kwa wahindi naye rais wao yupo maryland kapumzika kidogo! Mola amjalie afya njema!

Hela za escrow 200bln zinapigwa, wananchi wapo busy na yanga na simba nani mtani jembe!

Nchi bado inatawalika sanaaaaaaaa!! Na kwa hali hii wafuasi wa upinzani endeleeni kuota ndoto zenu za alinacha!
Mkitaka kunielewa jinsi ilivyo ngumu kupenya kwenda kuishi karibu na posta (magogoni) angalieni kwa yanayotokea Syria. Assad kakomaa hatoki ikulu; na ndio maana yake hatoki ikulu ndo habari ya ikulu hio baba/mama!

Sasa nyie ndo muende ikulu kama mnaendeka mlimani city vile kucheki show za akina sitti mtemvu??!! Thubutuuuu!! Acheni utani jamani nyie wapinzani! Sometimes muwe serious walau kidogo! Au mnafikiri ikulu ya Tanzania ni kama ya Burkina Fasso eeeehhhh!!!!! Imekula kwenu wakuu!!

2015 Kidume Edward Lowassa anatinga magogoni rasmi......Asieamini aendelee kuamini hivyo hivyo, Oct 2015 ataelewa ninachokisema hapa!!!!


Jembe Lowassa likiingia ikulu, Tanzania mpya itazaliwa! Unadhani watanzania wanaitaka Tanganyika???? Aaah wapi! System ya nchi ndo imekaa kushoto.....kwa hio wananchi wanatafuta namna ya kukabiliana nayo; yaani ayo ni utanganyika ni mahangaiko tu ya wananchi kukabiliana na mateso ya kiuchumi, kielimu na kiafya na si vinginevyo!

Lowassa akiingia ikulu tu baasi Tanganyika inasahaulika kabisa! Subirini muone!

Mungu iendelee kubariki uwepo wa Lowassa!

Ahsanteni sana wakuu!

Absolute garbage,huna sifa yoyote ya kumjadili Lowassa,tunaomuunga mkono Lowassa tupo lakini hatuwazi ovyo kama unavyowaza wewe
 
kwanini awaambie scandal ya RICHMOND? kwani sakata la ESCROW mliambiwa na nani? kwani haoahao si awaambie? mtatafut lakini mtashindwa. mtachimba kaburi kwa ajili ya mtu asiye na hatia mtadumbukia. hakika "THE DAY IS VERY CLOSE" Mpe salamu Kubenea amabaye amekuwa sana msemaji wa CCM kuwa Lowassa atafukuzwa.
 
LOWASSA matendo yake mazuri yanamuuza kuliko wanavyojiuza wengine kwa propaganda.
 
Mwakyembe alisema kuna manbo wameyaacha na hapo ndipo utajua kuwa Lowassa aliundiwa zengwe tuu ili kuwaficha wahusika wakuu na wenye Richmond na ndio maana iliendelea hata baada ya Lowassa kujiuzulu.
Mbona majibu tayari mnayo,fuatilia sakata la pesa za account ya escrow utajua ni nani yuko behind the issue of richmond,msiwe tomaso jamani,just streach ua brain a little bit
 
Back
Top Bottom