Lowassa, wananchi wanakuhitaji zaidi ya unavyowahitaji wewe

Lowassa, wananchi wanakuhitaji zaidi ya unavyowahitaji wewe

wewe timiza wajibu wako upate kibaba cha unga cha kulisha familia yako na jinsi la kufunika makalio yako.wwesio msemaji wa hao wannchi unaosema wanamuhitaji kibaka.
amini usiamini.baada ya uchaguzi mkuu 2015 kibaka huyo atakuwa aidha gerezani au kaburini

Yani mkuu nina hasira na hawa vibaraka wa mafisadi na bahati yao wamejificha nyuma ya pazia
 
Kingunge keshasema wote walioonesha nia hawafai. Sasa Lowasa atateuliwa na chama kipi? Ni vema tukangoja uamuzi wa ccm. mbona tunapakua chakula ambacho bado kupikwa?
 
Kenya walivyowapa chama pinzani madaraka walipata mabadiliko gani? Badala yake watu walikuwa wanakufa hovyo tu....tujifunze kutokana na makosa ya wenzetu
 
Ni Lowassa tu, mtaongea hadi kesho lakini kiongozi mwenye mvuto CCM ni Lowassa tu kwisha.
 
Kwa mimi kama Mimi.......ccm wasipompitisha lowassa basi, kura yangu itaenda kwa Dr slaa. Hawa watu wanashabihiana sana bt lowassa anafaa zaidi
 
Ukweli halisi ni huu hapa wakuu wala msihangaike bure:

Hata kama wapinzani watashinda kwa kupata kura zote hawawezi kuingia magogoni! Magogoni ni kwa ajili ya ccm baasi. Wapinzani baadae sana, sio sasa wakati bado nchi inatawalika. Wapinzani wataingia ikulu pale ambapo nchi haitawaliki lakini si kama ilivyo sasa hv! Niwakumbushe kulalamika lalamika haina maana kuwa nchi haiendi, inaenda sana tu! Si mnakumbuka ishu ya mzee wa vijisenti?Au mmeshamsahau mara hii? Mlilalamaika weeeee lakini juzi kai mzee wa vijisenti ndo anawaandikia katiba! Mpo hapo?

Hii nchi ni ngumu kwa wapinzani!! Kuna mengi hamjui, ila wanajitahidi sana lakini bado kabisa.

Dawa hazipatikani hospitali, wananchi wapo busy na foleni za kuwahi kibaruani kwa wahindi naye rais wao yupo maryland kapumzika kidogo! Mola amjalie afya njema!

Hela za escrow 200bln zinapigwa, wananchi wapo busy na yanga na simba nani mtani jembe!

Nchi bado inatawalika sanaaaaaaaa!! Na kwa hali hii wafuasi wa upinzani endeleeni kuota ndoto zenu za alinacha!
Mkitaka kunielewa jinsi ilivyo ngumu kupenya kwenda kuishi karibu na posta (magogoni) angalieni kwa yanayotokea Syria. Assad kakomaa hatoki ikulu; na ndio maana yake hatoki ikulu ndo habari ya ikulu hio baba/mama!

Sasa nyie ndo muende ikulu kama mnaendeka mlimani city vile kucheki show za akina sitti mtemvu??!! Thubutuuuu!! Acheni utani jamani nyie wapinzani! Sometimes muwe serious walau kidogo! Au mnafikiri ikulu ya Tanzania ni kama ya Burkina Fasso eeeehhhh!!!!! Imekula kwenu wakuu!!

2015 Kidume Edward Lowassa anatinga magogoni rasmi......Asieamini aendelee kuamini hivyo hivyo, Oct 2015 ataelewa ninachokisema hapa!!!!


Jembe Lowassa likiingia ikulu, Tanzania mpya itazaliwa! Unadhani watanzania wanaitaka Tanganyika???? Aaah wapi! System ya nchi ndo imekaa kushoto.....kwa hio wananchi wanatafuta namna ya kukabiliana nayo; yaani ayo ni utanganyika ni mahangaiko tu ya wananchi kukabiliana na mateso ya kiuchumi, kielimu na kiafya na si vinginevyo!

Lowassa akiingia ikulu tu baasi Tanganyika inasahaulika kabisa! Subirini muone!

Mungu iendelee kubariki uwepo wa Lowassa!

Ahsanteni sana wakuu!

Acha kutumika vibaya ni dhambi, bora utumike sehemu moja tu na HALALI kuliko utumike sehemu zote HARAMU.
 
Hapa wadau wote tunaomkubali EL tukutane kwa ajili ya kupena Updates na kukumbushana mawili matatu juu ya Mheshimiwa huyu ya Rais Mtarajiwa. Huyu ni kiongoz ambaye tumempoteza miaka mingi sana aina ya akina Sokoine. kiongozi mwenye uthubutu, msimamo,mtizamo,falsafa,kujiamini na mwenye maamuzi . Huyu ndiye anayejua uelekeo wa tanzania miaka kadhaa ijayo. acaheni wanaopiga kelele za Hovyo za wimbo ule ule wa miaka yote. Hapa tutamwongelea zee wetu ambaye ameonekana kupendwa na makabila yote na dini zote. na ndo maana hujamsikia akizungumziwa vibaya kwa mambo hayo kawa kuwa anajua yeye ni mtanzania na si Mmasai. Huyu mzee ndiye pekee ambaye ameonesha kuwa anaweza simamia jambo na likawa kama ambavyo amepanga liwe.ni mengi sana amezushiwa, ametukanwa lakini siku zote amkekuwa mkmya na kimya chake ndo kimesababisha wakati mgumu zaidi wa wapinzani wake wanaopiga kelele kila kona.wadau tusisite kuleteana habari katika thread hii.nami sasa naingia jikoni kuleta habari nyingi sana za Mh Lowassa na wapinzani wake akina bwana pinda,membe,sitta,wasira na wengineo. hapa tutawekana sawa tu. na hatulali mpaka TUMEWAELEWESHA.

LOWASSA 2015 .
Pokea like kibao. Mkuu umetishaje! Tuko pamoja mpaka tuwaweke sawa wote akili mgando.
 
Ni Lowassa tu, mtaongea hadi kesho lakini kiongozi mwenye mvuto CCM ni Lowassa tu kwisha.

NAWE BAKI NJIA KUU ACHA MCHEPUKO, MVUTO WAKE UKO KWAKO HUKO CCM KWA WACHACHE NA SI KWA WENZAKO.

NA UACHE KUTUMIA TUNGO TATA, JE WAJUA MAANA YA MVUTO vs JINSIA YAKO?
 
Edward Lowassa is back on the newspapers again! Kila gazeti ni edward Lowassa

Mwamba wa kaskazini! Juu ya mwamba huu nitalijenga taifa langu!

Jiwe walilolikataa waashi litafanywa jiwe kuu la pembeni!
 
Ukweli ni kuwa Mh Lowassa tulio wengi tunamhitaji. Hata walio wachache nao tunawaomba watuunge mkono huyu mzee wetu arejeshe nidhamu Serikalini.
 
Utachonga sana ndugu,maneno yako usije jutia 2015,ila Baba Lowassa hana mpinzani hao wote unaowaona ni wasindikizaji,siunafahau kwanye msafara wa mamba kenge pia hawakosekani...............

alivopigiwa makofi na vijana wa komba pale kwenye besidei ya ccm unaona ndio ameshakuwa mkulu!!!
 
Lowassa ni tumaini la mafisadi, wezi, wahuni, majangili na magaidi na wauza unga nchini. Haiwezekani kiongozi mzuri mwenye sifa za kuiongoza nchi aanze kampeni zake kwa kutoa rushwa ya mamilioni katika nyumba za ibada halafu akadaiwa eti ni "tumaini la Watanzania"
Sasa mbona ulideki barabara na kuzungusha mikono kumsapoti Edo?
 
Back
Top Bottom