Wala sio kitu cha kuongea kwa kigugumizi,ndio kiongozi pekee ambaye anaweza kusafisha hii nchi,am sure ndo kiongozi pekee anayeweza ku rescue hii elimu ya tanzania,naamini ndo kiongozi pekee anayeweza vunja mtandao wote wa ufisadi,naamini ndio kiongozi pekee tunayeweza sema NI CHAGUO LA MUNGU
Go baba Go baba Tuko nyuma yako makamanda wako and we pray GOD will give you strength tuweze fika huko
Lowasa -atupe Jina la Mgombea Mwenza
Sote tunakubali kwamba mhe. Edward Lowasa amefanya juhudi kubwa kujisafisha na kushawishi watanzania wamuunge mkono katika harakati zake za kuwania urais mwaka 2015. Kwa kiasi fulani amefanikiwa kwani amepata wafuasi wengi wanaompigia -chapuo na kumtetea kuwa anafaa kuwa rais. Amepewa sifa za kila aina kama vile mchapa kazi, mfanya maamuzi magumu nk.
Jambo ambalo -wapambe wa karibu wa mhe. Lowasa wanalifahamu kwa dhati ni kuwa pamoja na kumwagia sifa kemkem Boss wao, ipo sifa moja ambayo hawawezi kumpa- -Lowasa hana siha njema. Ugonjwa alionao wa PARKINSON unashambulia na kuharibu sehemu ya ubongo wake. Ugonjwa huo ambao HAUNA -TIBA ni endelevu kadri miaka inavyokwenda na uharibifu wake hauna kikomo. Dalili kubwa za ugonjwa wa parkinson ni kutetema kwa viungo vya mwili (tremor) kama vile mikono; mwendo pole (bradykinesia); na kukaza misuli (rigidity).Athari zake zinamfanya mgonjwa apoteze kumbukumbu na kushindwa kumudu shughuli za kawaida za kila siku. Ndio kusema, kadri umri unavyokwenda mgonjwa wa parkinson anakuwa -hajiwezi (disabled) kimwili na kiakili.
Kwa maana hiyo, ugonjwa wa -Mhe. Lowasa utamfanya, miaka michache baada ya kuingia madarakani (kama akifanikiwa), ashindwe kumudu majukumu mazito ya Urais. -Bahati nzuri Rasimu ya Katiba -inaeleza vizuri kwenye Ibara ya 84 sehemu 1-3 endapo Rais atashindwa kumudu madaraka kutokana na maradhi ya mwili na akili nini kitatokea. Ibara hiyo inasema wazi kuwa Makamu wa Rais ndiye ataapishwa kuwa Rais. Sasa swali la WATANZANIA ni hili: Je, nani atakuwa makamu wa rais wa Lowasa?. maana huyo ndiye rais wetu -mhe Lowasa itakaposhindwa kumudu madaraka ya rais.
Kutokana na ukweli huo, tunamwomba Lowasa ahakikishe mgombea mwenza wake ni solid, maana huyo ndiye atayemrithi. Yeye akishakamilisha ndoto yake, ampishe makamu wa rais atuongoze. Tutakuwa tayari kumsaidia akamilishe ndoto ya kwenda Ikulu endapo Lowasa atatuchagulia mgombea mwenza makini, mchapa kazi na anayechukia ufisadi. Tunataka Lowasa amtaje mgombea mwenza wake, ama sivyo atakuwa sio mzalendo wa kweli.
LOWASA ni tumaini la Watanzania!
Ukweli halisi ni huu hapa wakuu wala msihangaike bure:
Hata kama wapinzani watashinda kwa kupata kura zote hawawezi kuingia magogoni! Magogoni ni kwa ajili ya ccm baasi. Wapinzani baadae sana, sio sasa wakati bado nchi inatawalika. Wapinzani wataingia ikulu pale ambapo nchi haitawaliki lakini si kama ilivyo sasa hv! Niwakumbushe kulalamika lalamika haina maana kuwa nchi haiendi, inaenda sana tu! Si mnakumbuka ishu ya mzee wa vijisenti?Au mmeshamsahau mara hii? Mlilalamaika weeeee lakini juzi kai mzee wa vijisenti ndo anawaandikia katiba! Mpo hapo?
Hii nchi ni ngumu kwa wapinzani!! Kuna mengi hamjui, ila wanajitahidi sana lakini bado kabisa.
Dawa hazipatikani hospitali, wananchi wapo busy na foleni za kuwahi kibaruani kwa wahindi naye rais wao yupo maryland kapumzika kidogo! Mola amjalie afya njema!
Hela za escrow 200bln zinapigwa, wananchi wapo busy na yanga na simba nani mtani jembe!
Nchi bado inatawalika sanaaaaaaaa!! Na kwa hali hii wafuasi wa upinzani endeleeni kuota ndoto zenu za alinacha!
Mkitaka kunielewa jinsi ilivyo ngumu kupenya kwenda kuishi karibu na posta (magogoni) angalieni kwa yanayotokea Syria. Assad kakomaa hatoki ikulu; na ndio maana yake hatoki ikulu ndo habari ya ikulu hio baba/mama!
Sasa nyie ndo muende ikulu kama mnaendeka mlimani city vile kucheki show za akina sitti mtemvu??!! Thubutuuuu!! Acheni utani jamani nyie wapinzani! Sometimes muwe serious walau kidogo! Au mnafikiri ikulu ya Tanzania ni kama ya Burkina Fasso eeeehhhh!!!!! Imekula kwenu wakuu!!
2015 Kidume Edward Lowassa anatinga magogoni rasmi......Asieamini aendelee kuamini hivyo hivyo, Oct 2015 ataelewa ninachokisema hapa!!!!
Jembe Lowassa likiingia ikulu, Tanzania mpya itazaliwa! Unadhani watanzania wanaitaka Tanganyika???? Aaah wapi! System ya nchi ndo imekaa kushoto.....kwa hio wananchi wanatafuta namna ya kukabiliana nayo; yaani ayo ni utanganyika ni mahangaiko tu ya wananchi kukabiliana na mateso ya kiuchumi, kielimu na kiafya na si vinginevyo!
Lowassa akiingia ikulu tu baasi Tanganyika inasahaulika kabisa! Subirini muone!
Mungu iendelee kubariki uwepo wa Lowassa!
Ahsanteni sana wakuu!
Unahangaika sana ndugu yangu wagonjwa ni kama wakina Marehemu rais Sata,lowassa yuko gado kuliko unavyomfikiria,hayo maneno yenu ni yawaliokata tamaa,but the fact is ufe,ulie,ujinyonge LOWASA Is the NEXT Amiri jeshi Mkuu wa majeshi,usijali tutakualika kwenye inaguration worry not
Fisadi amalize ufisadi! Wewe ni mtanzania wa kwanza kuwa na IQ ndogo.