Lowassa: Waliniombea kifo, asema mabadiliko hayazuiliki

Lowassa: Waliniombea kifo, asema mabadiliko hayazuiliki

Lakini la ajabu na la kusikitisha,nyumbu Hao hao wa Lumumba,kwa sasa wanamsema vibaya sana Mwenyekiti wao wa chama.

eti wanadai kawazibia mianya ya kupiga hela chamani.
Hawajielewi hao Mkuu
 
Lowassa ni mshindani wa kweli,asiekata tamaa.Bila ushindani tutarejea kulekule.
 
huyu siyo waziri mstaafu bali ni alijiudhuru kwa kashfa za kifisadi na rushwa iliyokithiri !!!! ni ujinga kumuita waziri mkuu mstaafu.... lowasa alijiudhuru mwenyewe pale mambo yalipokuwa magumu chini ya kamati ya MWAKYEMBE... dr.slaa....zitto kabwe.... fisadi ni fisadi tu hata ajisafisheje kwa watanzania atabakia kuwa adui namba moja wa tanzania ... watanzania bado tunaikumbuka sana Richmond ya lowsa
Usisahau pia kuwa lowasa alipiga za ESCROW,LUGUMI na KIVUKO FAKE. Lowasa ndio fisadi pekee tanzania,belive me or not
 
Huyu mzee inawezekana aliwahi kuulizwa na Mungu kwamba Lowassa unataka nikupe nini? yeye akaomba "Hekima". Mwingine yeye aliomba apewe milki ndo haya tunayoshuhudia sasa hivi, busara kichwani ni ZERO (isome kwa kiswahili)
 
Lowasa waziri mkuu aliyefukuzwa kwa kashfa ya Richmond fisadi namba moja Tanzania,hivi bado anahutubia kwa dakika 2?
Jana huko Zanzibar hakusema CCM oyeeeee?
Mkuu mtabirie kifo basi au unaogopa
 
..nyeupe ni jizi, jambazi, fisadi, ongo, muongo, tapeli, hawezi kuwa kushinda uchaguzi wowote Tanzania
Mahakama ya mafisadi haina kazi kwa sababu mafisadi hakuna. Harrison mwakyembe waziri wa Sheria.
 
Hivi kwa mfano ukawakuta JK na EL sasa hivi wanapiga story wazo gani la kwanza litakujia wanazungumza kuelekea 2020?
Jk atakuwa Ana mueleza kuwa,kisa cha kukuengua muda wako ulikuwa haujafika!Wewe Ni WA 2020!
 





Arusha.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea duniani katika kipindi hiki hayawezi kuzuiliwa na mifumo iliyopo.

Akizungumza jana na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mateves katika Halmashauri ya Arusha Vijijini, Lowassa alisema nguvu kubwa ya mabadiliko inayoonyeshwa na Chadema itawaletea wananchi maendeleo.

Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, chama chake kilipata kura nyingi kwenye maeneo mengi licha ya kutokuwa washindi na kwamba wamejipanga katika uchaguzi wowote utakaofanyika kuhakikisha kinashinda kwa kishindo.

“Ninazindua kampeni za uchaguzi huu mdogo nikiwa na imani kubwa kwa Chadema. Nina imani kuwa mgombea wa chama hiki atatekeleza anayoyaahidi na kuondoa kero zenu na ndiyo maana Chadema inaungwa mkono zaidi nchini,” alisema Lowassa.

Alisema katika mpango wa kukiimarisha chama hicho, wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wanazunguka nchi nzima kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.

Katika harakati za kuhakikisha kwamba upinzani unaibuka na ushindi katika chaguzi ndogo zote zilizopangwa kufanyika Januari 22, Lowassa alisema leo atakuwa Zanzibar katika uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa Dimani kwa tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan na baada ya hapo ataelekea Bukoba katika kampeni za Ukawa.

Uchaguzi wa Kata ya Mateves unafanyika baada ya Mahakama kuagiza urudiwe kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi ulipita ambao mgombea wa CCM alitangazwa mshindi.
 
Hata kama tunataka mabadiliko siyo kwa kumtumia Lowassa!! Yeye hawezi kutusaidia zaidi ya kujinufaisha mwenyewe!! Ndio maana anatumia Fedha nyingi kuusaka Urais!! Atalipaje?? Tumieni akili nyie Bavicha!!
 
jamiiforums-20170108-0001.jpg
. Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, E. Lowassa amesema Serikali ya CCM ina watu wabaya sana kwani walimuombea kifo wakati wa kampeni.

Adai mabadiliko hayazuiliki kwani ndio muelekeo wa dunia kwa sasa.
 
Mungu ndio anapanga hatma yetu wote.Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kumpangia mtu kifo.Nafikiri hata Lowassa alivyo muumini mzuri wa dini yake analijua hilo.Mengine ni maneno tu.
 
Back
Top Bottom