Lowassa: Tutachukua nchi asubuhi

Lowassa: Tutachukua nchi asubuhi

Mimi si mwanachama wa CCM kama unavyodhani, lakini pia siyo mwanachama wa CHADEMA, ila ni mchangiaji wa pande zote. Jambo zuri kwa CCM naunga mkono hoja na likiwa baya napinga. Hali kadhalika kwa CHADEMA. Niko huru, sifungamani na upande wowote. Kama utakumbuka vizuri mijadala ya humu ndani nilianza kumpinga Edward Ngoyai Lowasa muda mrefu kabla hajahamia CHADEMA.Nilikuwa naiunga mkono CHADEMA kabla ya Lowasa kujiunga. Sikufurahishwa na maamuzi ya kipurure ya uongozi wa CHADEMA kumkaribisha na kumfanya mgombea wa nafasi ya uraisi tena kufuata njia za kidemokrasia. Siichukii CHADEMA na sera zake ila nachukia maamuzi yasiyofuata katiba ya chama na simfagilii Lowasa kuwa Raisi wa Tanzania. Kumkataa Lowasa hakunipi kadi ya uanachama wa CCM. La msingi kulijua ni kwa kuna mambo nayaamini, yanaweza kupatikana ama CHADEMA ama CCM. Ndiyo raha yangu sifungwi na mawazo ya mtu yeyote. Niko huru tangu 1961
mr bantulile, Jf si kama chombo chadema kama unavyodhani, Hapa kuna mkusanyiko wa watu wote kama hivi unavyoona, wewe ni ccm na upo hapa, tatizo ni kwamba ni dalili za kushindwa ndo zinawafanya mjifiche,

kwa maana unayoipeleka ukisema Jf ni kama chombo cha chadema ni sawa na kusema Tanzania ni chombo cha Ccm kitu ambacho hakipo
 
Jamani kwanza niwapongeze kina Mwigulu Nchemba, Anjela Kairuki, Januari makamba na wengine wengi kwa propaganda zao japo hazikua na tija wala mvuto lakini walijitahidi, niseme tu kwamba ndo ulipoishia uwezo wao japo najua hata saivi wako mahali wanapanga mikakati lakini wameshindwa...

Hawa wanadamu walichosahau ni kwamba "Tanzania hii ya leo ina watu makini sana" hata wale wasio soma Mungu amewapa upeo wa tofauti ni ajabu sana, wanaweza kuchambua mambo wakajua wapi mbivu, wapi mbichi, saivi mi naona tufanye jambo moja Tanzania ili tuwamalize kabisa hawa mafarao....Tuwapuuze kabisa wakimleta Dr slaa tusimsikilize, Wakimleta mama nyerere tumwambie muda umepita,wakimleta mama magufuli tumuulize alikuwa wapi muda wote?

Hebu watanzania twendeni na kauli hii hadi tar 25/10/2015 kauli yenyewe ni! "Lowasa ikulu hata kama Slaa akiwa kampeni manager wa CCM"

"Lowasa ikulu hata slaa akiwa kampeni manager wa CCM"
 
pombe kilabuni,makufuli mlangoni lowassa magogoni
 
We"Unasema Slaa mkuu,Hata aje Obama Lowasa ni direct ikulu
 
Naunga mkono. Nimeshangaa eti CCM wataleta mabadiliko, wakati katiba yetu iliyotarajiwa kuleta mabadiliko wameichakachua na kuirudisha ya zamani!! Hivi sasa wameiweka pending kama vile haipo ili muwape madaraka na kwakuwa Baadhi ya wenzetu ni wasahaulifu wameshasahau na wanaimba nyimbo zao za Richmond. Wamesahau juzi tu Mkuu wetu amesimamia wizi wa Escrow na kutuambia hela sio yetu bali ya rafiki zake hao. Ajabu ya karne wameshasahau alituahidi maisha bora na kila mtu aliaminishwa hivyo leo yako wapi? Hapana inatosha ngoja tugeuze upande wa pili kwa mwizi mmoja aliyekataliwa na wezi wenzake kuliko kumpa mwema mmoja anaeungwa mkono na wezi wengi.
 
CCM wameishiwa ... Wakimpeleka Mkapa anaishia kuharibu zaidi, wakimpeleka JK ghafla makomeo anaharibu...hawa jamaa hawa click hata chembe .... wanavurugana na sasa wanaishia kudesa kila kitu cha UKAWA ...
 
Kwani ikulu ni mochwari?

Acha matusi mbona hata aliyeanguka jukwaani kaongoza na anakaribia kulitua zigo la ikulu. Ikulu siyo mahali pa kufanyia biashara za sare za kijani ni mahala patakatifu japo pamekwishaanza kufanyiwa biashara tangu enzi za mzee nanii vile
 
Watu wengi wanasahau sana huyu Slaa kaanza kutumiwa tangu zamani na CCM. Sakata lote la Richmond waliliasisi CCM wakamkabidhi nyaraka Slaa ili ionekane ni hoja ya wapinzani lakini walikuwa ni CCM hao hao. Shida yao ni kumuogopa Lowassa ili asiingie ikulu mwaka 2010. Shida ilikuwa ni kumchafua Lowassa maana waliona speed yake ilikuwa kubwa kiasi kwamba Jk asingefuta mbele yake. Hadanganyiki mtu wao CCM na Slaa tulikwishawastukia kitambo kwamba ni wamoja
 
Mawazo ya kijinga kabisa! Hivi we unadhani Lowasa ana uchungu na maisha yako? Yeye ana uchungu na urais tu! Je asingekatwa ccm wewe ungekuwa ukawa? Na kama unajua yule ni oportunist kwa nini mnamwita kamanda wakati hajawahi kuipigia kura ya ndio katiba ya Warioba!! Na angekuwa anagombea kwa ccm leo mngekuwa na kauli zipi dhidi yake hasa akina Lisu na wenzake waliomuita fisadi!? Jitambue ndugu, Lowasa hana uchungu na umaskini wako, yeye anaitaka ikulu kwa namna yoyote! Mpenda nchi na amani hawezi kumchagua mpiga dili kuja kuuza nchi ni ujinga wa hali ya juu!
 
Back
Top Bottom