Unajua maana ya heshima ww? Fisadi hana heshima mpaka siku anaingia kaburini. Si ajabu hata kaburi lake likawa vandalized! Tutakuwa tumepotea kama taifa tukianza kuheshimu wezi eti kwa kuwa ni marais. Mwizi ni mwizi tu hata awe malaika na bila kujali ametoka chama gani. I got no respect whatsoever for dem thieves....!
Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa Mwanamke pamoja na mtoto wa miaka 12 waliopoteza maisha kufuatia msongamano mkubwa uliotokea kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mungu awatie nguvu na subira wafiwa wote.
Angalizo kwa vyama vya siasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi.
1. Ni vyema vyama vikazingatia zaidi kueneza sera za vyama vyao zikubalike kwa wananchi na wasishindane ni chama kipi kinajaza watu kwenye mikutano.
2. Tabia za vyama kusomba watu kwa magari kuwapeleka kwenye mikutano ziepukwe kwani zinafanya kutokuwa na uwiano sawa kati ya eneo husika na idadi ya watu waliohudhuria.
3. Tunajua umuhimu wa wasanii katika kuhamasisha na kama mjuavyo wasanii wengi wa Tanzania wanapendwa na makundi tofauti kama watoto, vijana na akina mama hivyo kama chama ikabidi kuwa na wasanii kwenye kampeni kihakikishe mahala kusanyiko litakapofanyika kuna usalama na nafasi ya kutosha.
Kuwa na maamuzi ya busara
1. Kama kiongozi wa nchi, na mgombea uraisi mnakuwa kwenye mkutano na kusifia umati mkubwa ambao hamjawahi kuuona and yet mnashindwa kuona athari iliyopo mbele kwa raia wenu huo ni udhaifu mkubwa kwenye maamuzi na maono yenu. Kama hiyo ilitokea mbele yenu basi mjue kuwa hata nyie hamkuwa katika usalama kwani lolote lingeweza kutokea. Je kwa hali hiyo mnahitaji kura kweli ikiwa hamjali usalama wa raia wenu?
2. Iweje uwanja una mageti 8 then mamlaka husika ifungue mageti matatu tu ili watu waingie na kutoka? Kilikuwa na hofu gani ya kufungua mageti yote? Mamlaka husika inabidi iwe responsible kwa yote yaliyotokea na wawajibishwe. Hapa ni viongozi wote waliokuwepo wanatakiwa kushare responsibility.
UJUMBE.
Mafuriko ya kutengeneza yana madhara. Tuache maji yafuate mkondo wake kwani nature ina namna ya kuyadhibiti. Ukitengeneza mafuriko wakati uko bondeni kwanini yasikudhuru?