Lowassa: Nitafuta misamaha yote ya kodi

Lowassa: Nitafuta misamaha yote ya kodi

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
21,854
Reaction score
26,091
Alitamka hayo akiwa iringa,Nitafuta misamaha yote ya kodi,Mara nitakapoingia ikulu na kuhakikisha bandari yetu inafanya kazi KWA SAA 24.
Nitafanya kazi na wananchi wangu bega kwa bega! hapa hapa,

Nitapunguza gharama za safari za nje KWA 90%

Sitaki kuona hats shilingi moja inapotea katka bandari yetu!

Tutakaa chini pamoja NA mabenki yetu kuona jinsi tutakavyoweza kupunguza riba na jinsi tutakavyoweza kurahisi mikopo ili kila mtanzania aweze kukopa benki katika kipindi kisichozidi Sikh 45--60,
***hakika amenigusa sana ndg Edo!
 
Lowassaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, ikuluuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.

Mimi sihitaji hotuba kumchagua lowassa wala sihitaji ahadi za kufuta kodi nampa kura zangu.

Ccm kwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Sio nyie tu...wengi tume muelewa jamaa sio maneno mengi....ccm walituzoesha maneno meeeengi utekelezaji ziroo! sasa mwaka huu lowasa kaja na kampeni za aina yake....lowasa ni genious! Viva LOWASA.
 
Bandari ikisimamiwa vizuri,

Misamaha ya kodi ya kijinga ikifutwa,

Safari za kijinga na matumizi yasiyokuwa ya lazima yakikatwa,

Tunao uwezo wa kuendesha bajeti yetu na ku-fund maendeleo yetu bila kutegemea "kutembeza bakuli" nje.....

Ombaomba ni moja kati ya vitu vinavyotia aibu kabisa....tabu unazunguka kuomba huku deni la taifa likizidi kupaa (nje pamoja na ndani)
 
Bandari ikisimamiwa vizuri,

Misamaha ya kodi ya kijinga ikifutwa,

Safari za kijinga na matumizi yasiyokuwa ya lazima yakikatwa,

Tunao uwezo wa kuendesha bajeti yetu na ku-fund maendeleo yetu bila kutegemea "kutembeza bakuli" nje.....

Ombaomba ni moja kati ya vitu vinavyotia aibu kabisa....tabu unazunguka kuomba huku deni la taifa likizidi kupaa (nje pamoja na ndani)

na mwingine anatumia milioni 500 kwenda kuomba anapewa msaada milioni 200
 
Huyo kutembea hawezi ataweza kusafiri, mie naona gharama za kusafiri hizo 10% zitakuwa za kuendea hospital,


Maguguli ndiye anaweza kutembea? Nasikia anatamani kwenda tena Loriondo kutafuta kikombe kingine maana hali yake siyo nzuri!
 
aanze na Vodacom pia aeleze zile bilioni 600 za shovacom,alphatel wazirudishe hapo ndio tutamwelewa kwa sababu ndietutamwelewa kwani na yeye ni mnufaikaji mkubwa wa ukwepaji wa kodi
 
Naona Lowasa kaeleza vizuri sana... wale wenye damu ya kijani hawamwelewi kabisaaa
 
****Kila enzi na zama zake!****
uwapo ndani ya ukawa,haupo juu ya utaratibu na agenda za ukawa!
 
Kufuta misamaha ya kodi ni uchizi Kuna mahospitali mashule yatima makanisa na misikiti Bila misamaha itakuaje?
 
aanze na Vodacom pia aeleze zile bilioni 600 za shovacom,alphatel wazirudishe hapo ndio tutamwelewa kwa sababu ndietutamwelewa kwani na yeye ni mnufaikaji mkubwa wa ukwepaji wa kodi
haisaidii kitu iyo Vodacom cjui nn wewe jifarij tu kura tunampa name ikulu anaingia hata kama alikwepa kodi
 
Mimi Edward Lowasa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naapa kuwa endapo nitachaguliwa kuwa rais nitatekeleza ahadi iliyoshindikana kwa miaka mingi ya kuboresha elimu ya mtanzania kwa kufanya yafuatayo:
Nitahakikisha walimu wanalipwa Stahiki zao zote kwa wakati.
Nitahakikisha madeni yote ya walimu yanalipwa ndani ya mwaka mmoja.
Nitahakikisha walimu wanapata teaching allowance & house allowance.
Nitahakikisha Mishahara ya walimu inalipwa kulingana na viwango vya elimu ikilinganishwa na kada nyingine kama afya.
Nitaweka posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu.
Nitahakikisha kila mwanafunzi anakalia dawati/kiti na ana meza.
Kila shule itapata computers kwaajili ya kufundishia wanafunzi na somo la computer litakuwa la lazima. Nitajenga maabara ya computer kila shule ya sekondari.
Nitaondoa michango yote mashuleni ikiwemo michango ya ulinzi, taaluma, ujenzi//ukarabati nk. Serikali . Itasimamia sehemu hiyo kwa ustadi mkubwa kuhakikisha walinzi wanalipwa na serikali, shule zinapata walimu wa kutosha, ujenzi/ukarabati unasimamiwa na serikali na unafanyika kwa wakati.
kama hayo niliyoyataja hayatatekelezwa ndani ya miaka 2 ya uongozi wangu, nitajiuzuru ili nishitakiwe kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusema uongo na kuwalaghai watanzania.MY TAKE WALIMU MSIMCHAGUA LOWASA MTAPATA LAANA
 
Back
Top Bottom