Lowassa: Nimeishafunga magoli ya urais

Lowassa: Nimeishafunga magoli ya urais

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,867
Reaction score
25,194
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, amezidi kupata maelfu ya wanachama wa CCM kumdhamini huku akisema kutokana na wingi wa watu wanaojitokeza tayari ameshafunga magoli ya urais.

Lowassa aliwasili jana katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea Tanga na kupata wadhamini 33,780 katika mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi, Lowassa alisema anajivunia rekodi yake kwa Watanzania kutokana na kumjua na kujua nguvu yake katika utendaji kazi.

"Nadhani wale wenzangu 36 wakiona umati huu watajua na kujionea kuwa nimeshafunga magoli, tena magoli yenyewe ni sawa na yanayofungwa na Ronaldo (Cristian) na Messi (Lionel) hayana ubishi," alisema Lowassa.

Alisema nia yake ya kugombea urais ni kutokana na kujiamini, ana uwezo, anatosha na amegombea ili ateuliwe na Chama hicho aweze kupambana na umaskini katika Taifa lenye rasilimali nyingi.

Akitangaza idadi ya watu waliojitokeza kumdhamini Lowassa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Cyril Chami, alisema Lowassa amepata wadhamini 33,780 katika mkoa huo.

Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani humo, Vick Nsilo Swai, alisema akinamama wa mkoa huo watahakikisha anashinda katika safari yake ya matumaini kutokana na utendaji aliouonyesha.


Chanzo: NIPASHE

MAONI YANGU
Ni magoli gani aliyoyafunga huyu FISADI hadi anafika hatua ya kutamba kiasi hiki? Je, anadhani kwamba fedha zake za wizi zinaweza kumnunua kila mtanzania?

:israel:
 
mtatukana sana,lakini Edo ndo rais, mtamchafua sana lakini Edo ataibuka mshindi
 
Lowassa kafungwa magoli ya urais ,uadirifu wa mashakamashaka goli moja,sifa 13 alizotangaza Mangula magoli 4 amfungwa Lowassa

Hebu oneni:-
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Kigezo [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Jaji Agustino Ramadhani [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Edward Ngoyayi Lowassa [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Umri [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Miaka 70 [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] 62 [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Elimu [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Ni ya juu ngazi ya shahada ya sheria [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Elimu ya juu ngazi ya shahada [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Uzoefu wa kazi [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Amebobea kwenye mhimili wa dola upande wa mahakama [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Amebobea kwenye mhimili wa dola upande wa serikali na bunge [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Uadirifu [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Hakuna mashaka yoyote kuhusu uadirifu wake [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Kuna mashaka mengi sana kuhusu suala la uadirifu [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Kazi alizofanya [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Jaji, mwanajeshi, mchungaji [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Kichunga ng`ombe, katibu wa chama, mkurugenzi IACC, mbunge, waziri, waziri mkuu. [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Historia kazini [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Amefanya kazi serikalini hadi amestaafu kwa mjibu wa sheria [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Alijihudhuru uwaziri mkuu kwa tuhuma ya kuipa tenda ya kufua umeme na kuiuzia Tanesco kampuni ya richmond ambayo haikuwa na sifa [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Kugombea urais [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Hajawahi kugombea labda hii itakuwa ni mala ya kwanza [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Aligombea mwaka 1995 jina lilikatwa kwa kukosa sifa [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Hali ya kugombea urais iliyopo hivi sasa [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Ameombwa agombee tena ameombwa sana [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Alianza mda mrefu kuonyesha nia ya kugombea urais, kuna mashaka mengi anahonga, ananunua makundi ili yamuunge mkono [/h] [/TD]
[TD="width: 186, bgcolor: transparent"] [h=1] Afya [/h] [/TD]
[TD="width: 327, bgcolor: transparent"] [h=1] Afya yake ni imala sana [/h] [/TD]
[TD="width: 257, bgcolor: transparent"] [h=1] Afya ni mgogoro mala nyingi huenda Ugermani kupima afya, mala kadhaa huwa na kitetemeshi hasa asubuhi, hana uwezo wa kuhimili mikikimikiki kwa mda mrefu [/h] [/TD]
[h=1] [/h]
 
Safari ya matumaini imezidi kushika kasi. Hakuna namna tena ya kuirudisha nyuma.
 
Lowasa ni alianza na Mungu atamaliza na Mungu,God bless our president

Tuta fungal na kusali na mungu atasikia kilio chetu.tumechoka kuburuzwa na michui ilio vaa ngozi ya kondoo. Ni heri Nchi iongozwe na simba mla watu kuliko kondoo ambae mna mjua. Kumbe sii kondoo ni chui alie jificha kama kondoo, atawamaliza atakula weeengi bilateral kumjua.
 
tpaul

Kama Raia niliyehudhulia udhamini wa wana CCM waliojitokeza mkoani Kilimanjaro kumdhamini, LOWASSA alichosema ni kwamba ashawapiga magori wagombea wengine wa CCM hasa kwa kupata idadi kubwa ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini.

Ufisadi unaousema ungetuonesha hapa vyanzo vya taarifa ya ufisadi wake tungeamini lakini kwa kuwa unaongea usichokijua nakuona kama mwehu, No research No Right to speak
 
Last edited by a moderator:
tpaul

Hivi Lowassa anawatetemesha sana ee??? .mkiamka Lowassa, mkila Lowassa. ..si ajabu hata mkiwa na wake zenu mnamtaja Lowassa. Sasa kwa nn mnapingana na nafasi zenu kua Lowassa ndio mpango mzima. Ndio jembe, jemedari wetu atakaempokea kijiti Rais wetu mpendwa JK.

Wakati mnanung'unika huku kwa maswala yasiyo na tija. LOWASSA NDIO ANAZIDI PASUA ANGA. Tunaelewa anatimua vumbi kali lazma muweweseke kidogo.

Ushauri wa bure badala ya kubakia kutimuliwa vumbi mgetumia hiyo nguvu kwenda kujenga hoja za wagombea wenu kwa wananchi ili angalau kujaribu kupunguza kishindo cha ushindi wa Lowassa kupunguza aibu .isiwe kubwa sana. Maana safari hii hata wapinzani watampigia kura EDWARD LOWASSA.

Mjiandae kisaikolojia ushindi wa Lowassa ni wa uhakika kwani alianza na Mungu na atamaliza na Mungu.
 
Last edited by a moderator:
tpaul


UNAPOTUHUMU MTU,
UJUE NA JINSI YA KUTHIBITISHA!
AMKA!! PELEKA VITHIBITISHO VYAKO MAHAKAMANI ,MAHAKAMA ZIPO WAZI ZINASUBIRI USHAHIDI WAKO,./i
 
Last edited by a moderator:
mtatukana sana,lakini Edo ndo rais, mtamchafua sana lakini Edo ataibuka mshindi

ndiyo. atakuwa rais wa ukoo wenu...kamwe FISADI lowassa ataingia kaburini anauota urais na hataupata milele. mijambazi sugu inayopaswa kuwa gerezani ndiyo inausaka urais wa nchi hii!
 
Back
Top Bottom