Lowassa ni msafi, Lakini kuna kitu hiki...

Lowassa ni msafi, Lakini kuna kitu hiki...

Geza Ulole, ngoja nikusanye orodha ya mashamba yake, sehemu yalipo na jinsi alivyoyapata. Nadhani hii itasaidia kumjua zaidi mwizi huyu wa mali za umma.
 
Jamani nisaidieni! Huyu Lowasa lini aliishi Mwanza na kumzalia huko huyu Fredrick kama siyo uongo huu ni nini hii? Nimeshindwa kuielewa hii picha. Halafu watu wana mihela mpaka wanaenda kununua majumba katikati ya London Jamani tutapona hapa kweli!??
 
Jamani nisaidieni! Huyu Lowasa lini aliishi Mwanza na kumzalia huko huyu Fredrick kama siyo uongo huu ni nini hii? Nimeshindwa kuielewa hii picha. Halafu watu wana mihela mpaka wanaenda kununua majumba katikati ya London Jamani tutapona hapa kweli!??

Mkuu..Frederick Edward Lowasa ni mtoto wa Edward Ngoyai Lowasa waziri mkuu wa zamani yawezekana aliwahi fanya kazi zamani huko mwanza akamzaa...kwani mwaka 1977 ni kitambo kidogo
 
Naamini watu mtaweza kukipakua na kutoa maoni yenu...

Kumbuka: Nyaraka hizi ni za SIRI KUBWA

Mkuu hapo red unatania au?

but this is probably a tip of an iceberg, tukiendelea kuyaibua mengine zaidi nguvu ya umma is coming tomorrow!
 
Hivi ukiwa mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Mambo ya Nje inaweza kukusaidia kwenye baadhi ya haya mambo ee?
 
Jamani RA na EL wakimwaga makontena ya kofia, vitenge na kanga kuna wa kuwazuia? Si wamemwaga kofia na kanga uchaguzi uliopita na wakapeta. Sasa kuna nini cha kuwazuia wakimwaga kanga tena hiyo 2015?
In short tumekwisha
 
Lowasa Achoka Kuzushiwa

Novemba 27, 2010

WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ameeleza kushangazwa na mwenendo wa kisiasa wa siku za hivi karibuni ambao unaliingiza jina lake katika matukio makubwa ya kisiasa yanayotokea. Mbali ya kueleza mshangao wake huo, Lowassa alikwenda mbele zaidi na kusema alikuwa amefikia hatua ya kuchoshwa na aina ya siasa zinazomhusisha na mambo yasiyo na ukweli wowote.

"Nimechoka kukaa kimya kila mara zinapotengenezwa habari za uongo juu yangu. Imefika mahali sasa nimeamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale ambao kwa makusudi na kwa nia mbaya wanafinyanga uzushi dhidi yangu na wakati mwingine dhidi ya familia yangu," alisema Lowassa aliyezungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana.


Akitoa mfano .....................
[not relevant here]

Mbali ya hilo, Lowassa alisema, watu wasiomtakia mema, ambao hata hivyo hakuwataja, wamefikia hatua ya kuanza kuipaka matope hata familia yake katika mambo ambayo si ya kweli. Lowassa alikuwa akizungumzia habari zilizomhusisha mtoto wake Frederick Lowassa katika tuhuma za kuchunguzwa na taasisi za ndani ya nchi na zile za nchini Uingereza kwa madai ya kusafirisha fedha nje ya nchi katika mazingira yenye utata.

Habari hizo zilizoandikwa katika gazeti moja linalochapishwa mara moja kwa wiki, zilimhusisha Frederick na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya pauni za Uingereza 475,000 (takriban shilingi bilioni moja) ambayo inatajwa katika maelezo ya awali iko mtaa wa Leinster Gardens, jijini London.

"Habari hizo zinazomhusu Frederick na ambazo zililitaja pia jina langu hazina ukweli wowote. Nimechoka kuzushiwa na kushambuliwa kwa mambo ambayo si ya kweli. Nimekuwa kimya na sasa wameanza kuichafua hata familia yangu.

"Nimewasiliana na Frederick mwenyewe ambaye amenihakikishia kuwa tayari ameshaanza kuchukua hatua za kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya kimaadili na kisheria kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na mahakamani ili kulisafisha jina lake," alisema Lowassa.
[Emphasis added]

Chanzo cha Habari: Tanzania Daima


Angalizo kwa waliokuwa wanamtetea Lowassa baada ya kuongea na TBC

Siku hizi inabidi kabla hujasema jambo ufanye uchunguzi wa kina na ufahamu cha kweli kipi na cha uwongo kipi, la sivyo unaweza jikuta katika matata mazito, hasa kama unafanya mambo kishabiki. Pia nimnukuu mdau mmoja kwenye blog moja: "kama kweli hii familia inasingiziwa, nadhani litakuwa ni jambo baya sana kutendewa, lakini kama wanatuambia wanasingiziwa na habari ni nyingine basi tukae na kutazama mchongo mzima unavyokwenda.."
 
Haya mambo tusubiri tuone, maana hiyo kampuni ya Integrated ni ya Wasomali ambao ni matajiri sana wana kampuni makubwa nje, lakini hebu tuangalie siri ya biashara za Wasomali kushamiri kwa kasi katika miji ya Dar es Salaam na Mombasa na hali ya sasa ilivyo, je Usalama wetu uko wapi?

Naambiwa hawa Intergrated wanannua majumba ya watu na viwanja kwa fujo maeneo ya Kurasini karibu na bandari yetu, je, watu wa TISS mpo? munalijua hilo maana hata watu nyeti wamelazimika kuuza nyumba zao huko maana jamaa wanatoa Cash kwa bei utakayo wewe

Na pirates wanacheza katika anga zetu! Tusijekuta hivi karibuni wakaanza kupaki meli huko Kurasini!

Amandla......
 
Naamini watu mtaweza kukipakua na kutoa maoni yenu...

Kumbuka: Nyaraka hizi ni za SIRI KUBWA


Beast in Make.

Lile DUDE la kuwabana na kuwaminya mbavu Watanzania wote linazidi kuumbwa kwa nguvu zetu wenyewe.

Nia na Madhumuni ya Lowassa ni kuingia Ikulu yeye na Maharamia wote.

Akisha fika huko ninyi akina INVISIBLE nilazima mtafute ardhi nyingine ya kuishi.

Lowassa ni MAFIA mkubwa juhudi zake za kuingia Ikulu ni lazima zinyimwe Oxygen.
 
Inasikitisha. Angalau hivyo vijisenti wangekuwa wanaviwekeza huku huku vingesaidia uchumi wetu kwa namna fulani.

Halafu kila siku mnawaandama hao mnaowaita wahindi kuwa wanapeleka vijisenti nje!

Amandla......
 
Halafu kila siku mnawaandama hao mnaowaita wahindi kuwa wanapeleka vijisenti nje!

Amandla......

Issue ya dual nationality inapingwa vikali kwa kuhofia wahindi wataitumia kuhamishia fedha nje wakati wamasai......
 
Ndio maana nawaambieni kuwa huyu jamaa akitangaza kugombea urais ndio siku naanza kuhesabu nilichonacho na kuhama nchi huyu jamaa ni hatari sana kwa nchi na akiteuliwa mjue ndio mmeumia.
 
Hahaha, mkuu taratibu... Nilimwangalia majuzi nikadhani bora nyaraka hizi tugawane na kulinganisha na kauli yake ya majuzi ambayo ni wazi inaashirikia mbio za kuelekea 2015

Familia ya huyu mzee inadhani watanzania mabwege watuambie zile nyumba wanazomiliki South Africa, Marekani wamezipataje? Bado hatujaanza kufichua katika account zao nje ya nchi wanakiasi gani.

Kuna rafiki yangu aliwahi kuniuliza wakati alikuwa anafanya kazi katika benki mmoja ulaya ila haifahamu Tanzania akauliza Lowassa unamjua nikamdadisi fikra zake zilimpelekea labda ni mfanyabiashara maarufu Tanzania. Kumbe angelijua ni mtumishi wa umma nikaamua kumezea tu....
 
Utu uzima ni dawa. Mwalimu Nyerere alipomkataa hadharani mwaka 1995 Edward Lowassa, alikuwa ana maana kubwa ambayo ndiyo tunajionea sasa. Viongozi wa jinsi hii ya Lowassa ni wa kuogopwa kama ukoma kwani hawana uchungu kabisa na nchi hii zaidi ya kujilimbikizia mali wao na familia zao. Hawajali amani ya nchi hii ambayo waasisi wetu wameitunza kwa miaka mingi sana.

Fikiria mtu wa jinsi hii akiwa Rais nchi itakuwaje? Tusidanganyike kwa maneno matamu ya watu wenye tamaa na selfish kama Lowassa na kundi lake.

Lakini cha ajabu ni kwamba hata wabunge wetu ambao tunaamini ni wasomi na waelewa, wanawezaje kumchagua mtu wa jinsi hii kuongoza kamati ya Bunge nyeti kama ile? Hasa tunapozungumzia usalama wa nchi yetu?

Inasikitisha sana.
 
Wana JF,

Napenda kuwaomba msamaha kwa dhati kabisa. Nilikuwa mstari wa mbele kumtetea Lowasa kwamba si fisadi, na nilikuwa nafikiri kwamba kujiuzulu kwake kulitokana na uwajibikaji. Lakini tokana na ukweli uliwekwa hapa jamvini ninaamini kwa 1000% kwamba Lowasa ni fisadi na pia ni mtu hatari sana kwa taifa letu. Watanzania ni lazima tuingie mitaani kuwafukuza wezi na washenzi kama Lowasa.
 
Mungu wangu mwingi wa Rehema naomba unipe moyo wa uvumilivu juu ya mambo haya yasiyovumilika
 
Back
Top Bottom