Mimi namlaumu Lowasa na kambi yake kwa kushindwa kujibu hoja uchwara na za kujinga zinazoelekezwa kwake kama tuhuma.
Nafikiri hata wapinzani wake wametambua kuwa huyo mh. ana domo zege ndio maana kila kukicha wanamtukana na yeye anakaa kimya tu wakati sheria zipo wazi kumlinda. Hata sheria za mitandao zimepitishwa ili kulinda haki za mtu lakini bado ameshindwa kuzitumia.Mbona Mwakyembe alipoona mitandao inatumika vibaya akaamua kuwasaka wabaya wake na akawapata.
Hapo ndipo ninapojiuliza kuwa kama Lowasa anashindwa kutetea haki yake mwenyewe na utu wake na heshima yake atawezaje kutetea haki na heshima ya watanzania.
Hata washauri wake naona ni watu wasiojishughulisha kupata habari na kumjulisha nini kinaendelea na ajitokeze vipi kujibu.
Mfano ni juzi tu Madabida amemkashifu kiongozi mkuu wa waislam mtume Mohamad.Labda hakua na nia mbaya. Lakini kama kweli hakuwa na nia mbaya ni kwanini mpaka leo sio Lowasa wala Madabida aliyejitokeza kuwaomba masamaha waislam wa Tanzania na dunia msamaha.
Je,ina maana Lowasa na kampani yake hawaoni madhara makubwa ya nayoweza kujitokeza kwa kupuuza suala hili. Na haoni kuwa watu wanaomzunguka wanaweza kuwa wametumwa na watawala ambao kwa kiwango kukibwa ndio wanaompiga vita!! Hivi Kweli washauri wake wanashindwa kumshauri namna ya kujitokeza na kuwaomba msamaha waislam ambao kwa asilimia kubwa ndio na watawala kutekeleza azma yao.Au anasubiri mpaka waislam wasambaze waraka nchi nzam wa tamko la kumkataa ?.
Hivi Lowasa anashindwa kujitokeza na kutoa ufafanuzi juu ya hicho kinachoitwa MOU ammbachokimetajwa sana kwamba ndiye aliyesababisha wakristo wawe wanachotewa mabilioni ya pesa na serikali. Hili nalo linamwia gumu kufafanu?
Na kama kweli mpaka sasa hajawajua watu wanaotumia vijana wasomi kumtukana na kumchafua kwenye mitandao basi ataingoza nchi kwa tabu kwani hatapata taarifa toka chini mpaka juu.Kama ana taarifa amechukua hatua gani ili kuondoa hizi siasa za majitaka.
Kama Lowasa na kundi lake wanashindwa kupambana kisheria na kubaina kakundi kadogo ka vijana wanaotumiwa na mahahasimu wake kiasiasa kwa lengo la kumchafua tu badala ya kuwanadi watu wao, atawezaje kupambana na uhalifu nchi nzim?