sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 133
[h=2][/h] Ijumaa, Septemba 21, 2012 06:18 Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
Kurasa 1 kati ya 3
Edward Lowassa
*Wavinyooshea kidole vyombo vya habari
*Ngwilizi: Msiandike habari za shauri la Lissu
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ameonya kuwa Tanzania inaweza kuingia katika machafuko kama yaliyotokea katika nchi za Zimbabwe na Rwanda kama baadhi ya vyombo vya habari havitaacha kuandika habari za kuwachafua watu.
Alisema kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kuanzisha vyombo vya habari kwa ajili ya kukomoa na kunyanyasa wengine kwa manufaa yao.
Lowassa aliyasema hayo jana, wakati akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Usuluhishi na Upatanishi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), dhidi ya Gazeti la Dira ya Mtanzania, ambalo linadaiwa kuandika habari za kumchafua.
Tukiruhusu watu waendelee kuanzisha vyombo vya habari kwa lengo la kuchafua wenzao, nchi yetu inaweza kuingia kwenye machafuko na kugeuka kama Zimbabwe na Rwanda, alisema Lowassa.
Kamati hiyo, ambayo inaongozwa na Jaji mstaafu Thomas Mihayo, ilisikiliza maelezo ya Lowassa, aliyekuwa analalamikia matoleo kadhaa ya gazeti hilo, aliyodai yana lengo la kumchafua binafsi, chama chake pamoja na kumgombanisha na Rais Jakaya Kikwete.
Akinukuu moja ya vichwa vya habari katika matoleo hayo, ambacho kilisema Kapteni Lowassa aandaa mashtaka, alisema habari hiyo ililenga kumgombanisha na Rais Kikwete kama mwenyekiti wake wa chama, lakini pia kama mkuu wa nchi.
Pengine walioandika habari hizo wanatumiwa au wanashawishiwa, sina ushahidi, kama wanalipwa, lakini naamini wanatumiwa ili kunichafua.
Fikiria nagombanishwa na mwenyekiti wa chama changu (CCM), ambaye pia ni mkuu wa nchi, angeweza kunikamata na kuniweka ndani, lakini wao wanaandika kana kwamba wana ushahidi juu ya jambo hilo, alisema.
Malalamiko mengine ya Lowassa, yalikuwa ni habari zilizokuwa na vichwa vya habari vya Lowassa Chenge tena, Nape atonesha kidonda CCM, akumbusha Mwalimu alivyomkataa Kapteni Lowassa, Kapteni Lowassa atajwa vurugu CCM Arusha, Kapteni Lowassa Kikwete basi.
Nyingine ni Askofu Mokiwa amkana Kepteni Lowassa na CCM yapambana na Kapteni Lowassa.
Matoleo yote hayo, Lowassa alisema hayakuwa na nia nyingine zaidi ya kumchafua na kumgombanisha na Rais wa nchi.
Hata hivyo, gazeti la Dira halikufika katika usuluhishi huo, badala yake dakika chache kabla ya shauli hilo kusikilizwa, walituma ujumbe mfupi wakieleza kuwa mhariri wa gazeti hilo amesafiri na vielelezo vyote.
Kufuatia hatua hiyo, Jaji Mihayo na Kamati yake waliamua kusikiliza shauri hilo kwa upande mmoja tu wa mlalamikaji.
Sura za Habari Hii |
---|
Lowassa, Ngwilizi waonya |
Uamuzi |
Adhabu |
Habari Yote |