Lowassa, Ngwilizi waonya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Ngwilizi waonya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Sep 21, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Ijumaa, Septemba 21, 2012 06:18 Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam

  [TABLE="class: contenttoc"]
  [TR]
  [TH]Sura za Habari Hii[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Lowassa, Ngwilizi waonya [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Uamuzi [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Adhabu [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Habari Yote [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Kurasa 1 kati ya 3
  [​IMG]Edward Lowassa

  *Wavinyooshea kidole vyombo vya habari
  *Ngwilizi: Msiandike habari za shauri la Lissu
  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ameonya kuwa Tanzania inaweza kuingia katika machafuko kama yaliyotokea katika nchi za Zimbabwe na Rwanda kama baadhi ya vyombo vya habari havitaacha kuandika habari za kuwachafua watu.

  Alisema kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kuanzisha vyombo vya habari kwa ajili ya kukomoa na kunyanyasa wengine kwa manufaa yao.

  Lowassa aliyasema hayo jana, wakati akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Usuluhishi na Upatanishi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), dhidi ya Gazeti la Dira ya Mtanzania, ambalo linadaiwa kuandika habari za kumchafua.

  “Tukiruhusu watu waendelee kuanzisha vyombo vya habari kwa lengo la kuchafua wenzao, nchi yetu inaweza kuingia kwenye machafuko na kugeuka kama Zimbabwe na Rwanda,” alisema Lowassa.

  Kamati hiyo, ambayo inaongozwa na Jaji mstaafu Thomas Mihayo, ilisikiliza maelezo ya Lowassa, aliyekuwa analalamikia matoleo kadhaa ya gazeti hilo, aliyodai yana lengo la kumchafua binafsi, chama chake pamoja na kumgombanisha na Rais Jakaya Kikwete.

  Akinukuu moja ya vichwa vya habari katika matoleo hayo, ambacho kilisema ‘Kapteni Lowassa aandaa mashtaka’, alisema habari hiyo ililenga kumgombanisha na Rais Kikwete kama mwenyekiti wake wa chama, lakini pia kama mkuu wa nchi.

  “Pengine walioandika habari hizo wanatumiwa au wanashawishiwa, sina ushahidi, kama wanalipwa, lakini naamini wanatumiwa ili kunichafua.

  “Fikiria nagombanishwa na mwenyekiti wa chama changu (CCM), ambaye pia ni mkuu wa nchi, angeweza kunikamata na kuniweka ndani, lakini wao wanaandika kana kwamba wana ushahidi juu ya jambo hilo,” alisema.

  Malalamiko mengine ya Lowassa, yalikuwa ni habari zilizokuwa na vichwa vya habari vya Lowassa Chenge tena, Nape atonesha kidonda CCM, akumbusha Mwalimu alivyomkataa Kapteni Lowassa, Kapteni Lowassa atajwa vurugu CCM Arusha, Kapteni Lowassa Kikwete basi.

  Nyingine ni Askofu Mokiwa amkana Kepteni Lowassa na CCM yapambana na Kapteni Lowassa.

  Matoleo yote hayo, Lowassa alisema hayakuwa na nia nyingine zaidi ya kumchafua na kumgombanisha na Rais wa nchi.

  Hata hivyo, gazeti la Dira halikufika katika usuluhishi huo, badala yake dakika chache kabla ya shauli hilo kusikilizwa, walituma ujumbe mfupi wakieleza kuwa mhariri wa gazeti hilo amesafiri na vielelezo vyote.

  Kufuatia hatua hiyo, Jaji Mihayo na Kamati yake waliamua kusikiliza shauri hilo kwa upande mmoja tu wa mlalamikaji.
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Lowasa anahaha.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwambieni Lowassa hao wanaoandika kwenye vyombo vya habari wanauliwa kama wanyama pori na Jeshi la polisi. Nini kauli yake akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama?
   
 4. k

  kwitega Senior Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ni uongo alikataliwa na hayati baba wa Taifa? waandishi endeleeni kuanika madudu ya wanasiasa uchwara. Tena chimbueni zaidi na kuanika wazi ili watanzania wajue majitu yanayopora raslimali za taifa.
   
 5. m

  makelemo JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli alichonena, maana hata machafuko ya kenya, Rwanda na Burundi source kubwa ilikuwa media, kama anachafuliwa ni vyema akajisafisha kwa kusema ukweli katika yale anayozungumzwa kuhusu yeye, au aende mahakamani ili ukweli uonekane. kwa nn aende kwenye usuluhishi unaofanyika chumbani? aibuke hadharani ili hata walio nje na vielelezo nao wajitokeze kumtetea kama anasafishika.
   
 6. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo anasumbuliwa na laana ya kumwagia tindikali Saed Kubenea.
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kuwa na mvi kichwa kizima haimaanishi una busara. Wenye busara ni wale wanoona na kusoma alama za nyakati. Lowasa pumzika achana na siasa maana hata ukiwa Raisi muda wako wa kuishi utakuwa ule ule tuuu. You have everything now, the excess you want is damn expensive for you.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  waandishi wa habari wanagombania freedom of press lakini waandike habari za uhakika sio kutupa story za mitaani... am sure hizo habari zinapelekwa huko magazetini na wabaya wake huko huko ccm wala sio kwingine
   
 9. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ki.kwete alikataliwa pia, Nyerere aliuona udhaifu wake toka alipokuwa waziri wa mambo ya nje
  Kumbuka kauli ya Odinga, alipoishangaa Tanzania kumpitisha kikwete, mtu ambae kipindi cha sessions za umoja wa mataifa alikuwa akishinda hotelini na malaya
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwanza, reference ya Zimbabwe na Rwanda haina mashiko kabisa. Zimbabwe vurugu zilitokea kwa sababu chama tawala hakikuwa tayari kuachia upinzani uingie madarakani. Na Rwanda vyombo vya habari vilitumiwa kuchochea mauaji ya kimbari. Sasa hapo inahusianaje na Tanzania?
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Na yeye binafsi anaweza kuwa msafi dhidi ya wenzake? Anaweza kueleza ushiriki wake kwenye campaign ya kumchafua Dr Salim Ahmed Salim 2005 kupitia vyombo hivyo hivyo vya habari?
   
 12. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
   
 13. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Yeye na genge lake walimfanyizia hivyo hivyo Dr Salim Ahmed Salim, Sumaye na Mwandosya mwaka 2005, sasa mambo yamemgeukia analialia!! Ukiua kwa upanga ujue utakufa kwa huo huo upanga!!
   
Loading...