Usichukue maneno ya mtaani na kuyaleta kwa watu,toa mfano,ameiba hapa kiasi,hiki naushahidi huu,ukisema tuu mwizi haikupi uhalali wa hoja yako,mimi nina mifano ifuatayo,ambayo nina ushahidio juu ya umahiri na uchapa kazi wa Lowwassa,1.Alisimamia kidete wizara ya maji na kufanikisha kuvunja mwiko kwa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria hadi mikoa ya mwanza na Shinyanga na hivyo kuwasaidia watu wetu kupata maji ya uhakika,hili lilihitaji kuthubutu na kusimamia, 2.Serikali ilikosa pesa za kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma ndani ya muda mfupi Lowwasa alisimamia kidete mifuko ja jamii kutoa pesa na kuwajengea watoto wa kitanzania Chuo kikubwa kabisa katika ukanda wa Africa ya mashariki na kusini leo hii tunajivunia chuo hakijaota bali ni mipango na usimamizi wa huyu jemedari wa kazi chini ya mzee wetu Kikwete 3.Lowasa kwa kuona watoto wa wanyonge wanakosa elimu alisimamia kwa dhati na kidete hadi zikajengwa shule za kata nchi nzima na kufanya idadi ya sekondari kuongwezeka kwa asilimia elfu maja na mia tano karibu.4.Palipotokea tatizo la umeme nchni na kuonekaka kuwa Richmond haikua na uwezo wa kuzalisha umeme kwani ilikua ni kampuni isiyo na uwezo,Lowasa alikua tayari kuwajibika na kujiuzulu uongozi mkubwa kabisa wa nchi ili kupunguza joto la kisisa kwa Jemedari wetu Rais Kikwete 5.Lowwasa ameonesha uvumilivu na ukomavu wa kiuongozi baada ya kutukanwa sana na kuamua kukaa kimya jambo ambalo angeweza kukurupuka na kujibu mapigo 6.Lowwasa ameweza kuona tatizo la ajira kwa vijana katika taifa letu jambo ambalo hata Rais wetu Kikwete alilizungumzia kwa mkazo