Lowassa ndani ya Kigoma

Lowassa ndani ya Kigoma

Waziri Mkuu Mstaafu EL amewasili Mkoani Kigoma hv punde. Amealikwa kuja kuendesha Harambee kanisa la PENTEKOSTE ..............
Mengi Tutawajuza.

.
Unafikiri ni kwa nini kina Karanga hawaamini uwepo wa Mungu? Ni kwa matendo kama haya, ya wale wanaojitangaza kuwa waatumishi wa Mungu aliyemtakatifu wakizitamani kwa udi na uvumba pesa za Shetani ili wazifanyie kazi ya kuzitakasa nje ya njia waanayowahubiria wengine. Maana neno la Mungu wanaedai kumtumikia linaagiza mwivi akiiona haki, basi arudishe mali ya wizi kwa wenyewe na kisha amfuate yeye(Mungu).
Yaani nakuhakikishia vyombo vya habari vikikutangaza leo kuwa wewe ni fisadi na umekwapua bilioni kadhaa, kesho yake utaona jinsi utakavyogombaniwa na mialiko mingi ya harambee na viongozi wa dini kuchangia cash.
.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Rais ajeye ni mpemba, Lowasa badili kabila utokee Zenj
 
Usijali mpendwa Mungu wa majeshi Jehova Eloimu hahongeki wala yeye njia zake si zetu; Hasira ya Mungu iko daima na waovu japo yeye huwaacha waovu wajitukuze kwanza ili kwakipimo cha utukufu wao anguko lao liwe saba mara sabini...Gravity haina effect kwake yeye aliye chini ukitaka uone nguvu ya gravity pandaa juu ya kinara alafu kisha pima nguvu yake kwakujidondosha..Acha wafu wazike wafu wao wewe kazana kumsifu Mungu ili atende kwa sifa na utukufu wa jina lake.
 
Rais ajeye ni mpemba, Lowasa badili kabila utokee Zenj

Rais ajaye ni Dr. Wilbroad Petter Slaa...Kila environment tukio la mnyukano ambao tutaanza ku-experience utam favour yeye japo tutapitia katika prukushani za hapa na pale mpaka zitakapobaki camp mbili zenye nguvu lakini kwa utukufu wa Mungu mwenyewe Slaa atapita na kila jicho halitaamini kinachotokea.
 
Lowassa atamaliza mikoa yote kwa hii stail ya harambee kwani anapima maji ya kina gani!!!
 
Usijali mpendwa Mungu wa majeshi Jehova Eloimu hahongeki wala yeye njia zake si zetu; Hasira ya Mungu iko daima na waovu japo yeye huwaacha waovu wajitukuze kwanza ili kwakipimo cha utukufu wao anguko lao liwe saba mara sabini...Gravity haina effect kwake yeye aliye chini ukitaka uone nguvu ya gravity pandaa juu ya kinara alafu kisha pima nguvu yake kwakujidondosha..Acha wafu wazike wafu wao wewe kazana kumsifu Mungu ili atende kwa sifa na utukufu wa jina lake.

.
Afadhali mkuu, umenifaariji. Be blessed!
.
 
EL anashindana na Membe kufanya siasa za kanisani.
 
Unajua, Makanisa mengi yanamtumia huyu jamaa huku wakijua kuwa ni fisadi asiyesafishika. Wao wanachokitaka ni pesa yake na wanajua kuwa kahamishia kampeni za 2015 makanisani sababu hana pengine. waumini wenyewe si wale wale wanaomjua kuwa hafai! wacha ajenge makanisa na kuchangia kwaya lkn uraisi hapati!
 
Umaarufu huu wa makanisani umeonekana kwa wengi baada ya kashfa ya richmond lakini ukweli ni kwamba huyu jamaa ni bingwa wa harambee kabla hata ya hiyo kashfa, tena ilipomkumnba alikuwa akikataa kwenda kwenye harambee nyingine nafikiri alikuwa guilty lakini baada ya kile kikao cha DOM naona kapata nguvu mpya, cha msingi labda wananchi tuseme hatutaki ashiriki harambee zetu la sivyo hiyo ni kete yake ya siku nyingi.

Tuna mafisadi wengi tu low-profile lakini hakuna hata senti yao inatumika kokote, mimi naamini kuwa huyu si rais ajaye maana 2015 naamini rais atatoka upinzani na yeye hawezi kupokelewa na upinzani ila tumwache afanye harambee zake kwa amani kama ni ujenzi wa makanisa poa tu, mbona wengi wanapata hofu wakati takwimu zinaonyesha wakristo ni 35% ya watanzania wote? Bado anakazi kubwa kwa 65% iliyosalia kuwafikia kwa njia hiyo.
 
Mungu ameshamuonesha njia Mh Lowasa.Kwa wale wasio na 200 wapige mbizi lakini taka wasitake Raisi 2015 ni Edward Lowasa.
 
Waziri Mkuu Mstaafu EL amewasili Mkoani Kigoma hv punde. Amealikwa kuja kuendesha Harambee kanisa la PENTEKOSTE ..............
Mengi Tutawajuza.

UPDATE:

Lowassa achangishia kanisa mamilioni

Zaidi ya Shilingi milioni 125 zilipatikana katika harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari
Kidingo mkoani Kigoma iliyoendesha na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Lowassa na marafiki zake walichangia Sh. nilioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo iliyoko Kata ya Mwandiga wilayani Kigoma.

Uchangiaji huo ulifanyika jana katika Kanisa la FPCT na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge wa mkoa wa Kigoma na madiwani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Lowassa alisema watu wengi wanapenda kuitumia nguvu ya maaadamano badala la nguvu ya kuleta maendeleo katioa ujenzi wa shule.

Alisema kuna vijana wengi waliokosa ajira, ambao alisema ni bomu linalosubiri kulipuka. Alisema vijana wengi wanamali za shule na vyuo, lakini wanakosa ajira.

Aliiomba serikali na wadau mbalimbali nchini kukaa chini kupanga mikakati ya namna ya kuwasidia wapate ajira.

Aidha, aliwataka watu waliomali za masomo wasisubiri ajira za serikali badala yake wajiunge katika vyuo vya ufundi stadi ili wajiajiri.

CHANZO: NIPASHE (Jan 10, 2012)

Hapo kwenye RED ni Kabingo
 
Watanzania kama hamtakuwa makini siku zote tutaishia kulalamika tu! Nakumbuka mwaka 2005 mojawapo ya kitu lilichomfanya Kikwet kushinda kwa kishindo ni ahadi zake kuhusu mikataba ya madini. Watanzania wengi tulitegemea mara tu baada ya Kikwete kukabidhiwa rungu ni kushughulikia mikataba mibovu ya madini. Akiwa na Lowasa huyuhuyu nini kilifanyika na ni nini kimefanyika mpaka leo hii kuhusu mikataba mibovu ya madini kama si kuongeza mikataba mingine zaidi feki? Watu hawa Kikwete na Lowasa ni watu makini katika kupanga mikakati ya kuingia Ikulu, Lowasa ameishaona tatizo la ajira kwa vijana na atalitumia vyema kama Kikwete alivyotumia mikataba mibovu ya madini.
 
lowassa lowassa lowassa... ubarikiwe sana kwa kuchangia mkoa wa kigoma, mungu aendelee kukuongoza na kukulinda. daima wewe ndio chaguo langu. nimesikia mufti mkuu kamualika kwenye msikiti hapa dar kufanya harambee na amekubali.

watumishi wengi wa serikali na great leaders wanaalikwa issue ni wao kujipanga kufanya hivi vitu. membe alienda last time akaambulia kuchangisha sijui 15m, sumaye akachangisha 23m, akienda lowassa anagonga 100m. mi nadhani ni influence aliyonayo tu. naona watu wengi hujitoa kumchangia kila sehemu anapoalikwa. juzi tu harambee ya mwaka jana alipigiwa simu rafiki yangu na wenzake kuomba kuchangia harambee. raha aliyoipata pale bar akachanganyikiwa kabisa, akafurahi sana kuombwa, akaomba tuchange tupate 5m tumsindikize lowassa.

mi naona ni influence aliyonayo, raha kuwa karibu nae, raha kuona uchapakazi wake, raha kuona anavyoipenda hii nchi na kuipigania.
 
Back
Top Bottom