Kombo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,812
- 511
Kuna wakati huko nyuma niliuliza lakini hata Mzee Mwanakijiji alishindwa kunisaidia, Lowasa alijiuuzulu uwaziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond ili amnusuru rafiki yake BoyZ to Men Mheshimiwa Jakaya Kikwete.
Kwa upeo wangu mdogo mtu akijiuzulu anakosa sifa ya kuwa mstaafu kwa hiyo Kama CCM wanamwita mstaafu ni kosa kubwa na Waziri wa fedha pamoja na Rais hawakupaswa kuidhinisha Edward Lowasa(MB) kulipwa mafao ya Waziri Mkuu mstaafu ambayo ni asilimia 80% ya Mshahara wa Waziri Mkuu anayeko madarakani.
Once tukijua hicho kiasi ndipo tukokotoe hizo gharama anazochangia makanisa na kipato chake Halali of course aliiba sana na anazo pesa nyingi no doubt, hii inanipa wakati mgumu pia na usafi wa haya makanisa ambayo siku hizi yameanza biashara na kwa kuwa yana wafuasi wengi ni jambo la hatari kwa mwanasiasa kukaa nyuma ya dini.
All the time religious extremism is a cancer "whether Muslim or Christian " misingi yake mikuu ni ubaguzi : sisi na wao: mwisho wa siku ni vita. Tumwogope mwanasiasa staili ya Lowasa na lazima aangushwe at any cost!
Nitajibu moja tu hapo:
Sehemu kubwa ya pesa anazotoa "Mgeni/mwongoza harambee" hutoka kwa marafiki zake na watu wema wengine-si zake!
Kwa viongozi wa Serikali walioko madarakani na wenye mafungu ya kuchochea maendeleo kwenye ofisi zao huweza kutoa sehemu ya pesa za kuchochea maendeleo kama mchango kwenye harambee zenye faida kwa jamii.