Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,872
Edward Kwanini nchi Ilipokuwa Njiapanda Ulikaa Kimya? Ni Kiongozi waaina Gani Wewe?Kuna wakati nchi ilipita kipindi kigumu sana cha sintofahamu.
Kwanza ilikuwa wakati wa Bunge Maalumu la katiba ambapo nchi iliyumba na kutokea kutokuelewana kwa hali ya juu. Na kama sio wapinzani kuamua kutoka nje hakika bunge lile lingeishia waheshimiwa kupigana na kuvuana nguo kabisa.
Edo kama mjumbe ndani ya BMK hakuwahi kusikika akichangia kitu wala kutoa ushauri wakati ule mgumu kwa taifa katika kupata maamuzi yenye tija. Ni kiongozi wa aina gani asiyejihusisha au kuonyesha busara zake pale jambo zito linapo wakanganya watu?
Kukaa kimya ni kuonyesha huna upande au hujui utatuzi wa jambo hilo? Kama ulishindwa utatuzi wa utata wa Katiba jee changamoto za nchi itakuwaje?
Kulijitokeza suala lingine la Tegeta Escrow ambalo kidogo liiangushe serikali ya chama chako Bungeni, mapesa mengi yalichotwa na serikali na chama chako kilivuliwa nguo hadharani ila wewe hakuna aliyekusikia ukisema au kuchangia chochote katika jambo kubwa kama lile jee ulikuwa hujui ufumbuzi wake?
Au wewe ulikuwa huna uchungu na kilichotokea kwa vile wewe hupati maumivu ya hasara ile?
Ukiwa kama Mbunge lile lilikuwa jukwaa lako la kusemea hisia zako, sasa mbona watu leo hawajui kuhusu hisia zako katika lile? Huoni kuwa uwepo wako Bungeni ulikuwa sawa na kile kiti tuu, maana kiti Bungeni huwa kipo mwanzo mwisho wa kikao lakini hakina mchango wowote wa maana kwa kile kizungumzwacho.
Ndio maana watu wanaamini habari kuwa kuna watu matajiri wanamwaga mapesa yao kuhakikisha kuwa unashika nafasi ya juu kabisa kwa vile mambo mabaya kwa nchi hutasema, utakuwa BUBU kama ulivyokuwa Bungeni.