Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Suala hili lilitokea muda mrefu kidogo lakini nalirudisha tena kwa sababu binafsi nadhani halikupewa uzito unaostahili na hivyo kufifia wakati ni suala ambalo leo hii ndilo linalo tuweka kama taifa katika hatari ya kutumbukia katika mgogoro mkubwa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa alitoa kauli juu ya matatizo ya kiuongozi yanayokikabili chama cha CCM, kauli ambayo iliamshwa mjadala mkubwa nchini. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Lowassa alinukuliwa akisema yafuatayo kuhusu CCM na uongozi wake:
"Pamoja na uzuri wake, muundo wa chama chetu ni mzuri sana, imani ya chama chetu ni nzuri sana, misingi inayoongoza chama chetu ni mizuri sana, lakini tuna tatizo la utendaji na uongozi ndani ya chama chetu."
Lowassa pia aliongeza kusema:
"…Ama katika kufanya maamuzi, ama kufanya maamuzi yasiyo sahihi au kutochukua hatua kwa matatizo yanayowakabili wananchi kwa wakati muafaka..."
Pamoja na umuhimu wa hoja hii, hasa katika nyakazi hizi ambazo CCM inatakiwa kujisahihisha kama ina nia ya kuendelea kupewa dhamana ya kuongozo nchi, badala yake hoja ya Lowassa ilibezwa na viongozi wengi ndani ya CCM, lakini mbaya zaidi ni kwamba hata jamii haikupa uzito unaostahili na hivyo kuifanya hoja ififie mapema. Wengi tunakumbuka kwamba Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kwamba CCM ikiyumba, nchi itayumba. Huu ndio uhaliasia wa mambo baada ya miaka zaidi ya kumi na tano tangia Nyerere atoe utabiri wake kwani leo hii nchi yetu inapita katika kipindi kigumu pengine kuliko vyote tangia uhuru na sababu kuu ya tatizo hili ni matatizo ya uongozi ndani ya chama. Imekuwa ni jadi kwa jamii kushuhudia jinsi gani mienendo na lugha za baadhi ya viongozi wa CCM na baadhi ya wabunge wa CCM inavyozidi kukigharimu chama. Kwa mfano, kwa wengi wa wanaofuatilia kikao cha sasa cha bunge watakubali kwamba udhaifu wa kiuongozi miongoni mwa wabunge wengi wa CCM unazidi kulipeleka taifa letu kwenye hali ya hatari kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani vikatumia muda na nafasi hii kujifunza juu ya matatizo na changamoto zinazokikabili CCM badala ya kutumia muda mwingi kucheka na kuikebehi CCM kwani matatizo yanayokikabili CCM yanaweza kukikumba chama kingine chochote kitachofanikiwa kushika madaraka ya nchi yetu siku za usoni.
Tukirudi kwenye hoja ya Lowassa juu ya CCM na matatizo ya uongozi, moja ya sababu kubwa ya tatizo hili ni CCM kujaa wanasiasa huku kikipungukiwa viongozi wa kisiasa. Ni muhimu tukatambua kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya Mwanasiasa na Kiongozi katika utawala wa nchi. CCM kama chama lakini pia kama taasisi ina hazina kubwa sana ya wanasiasa, huku kikiwa na uhaba mkubwa wa viongozi. Nitajaribu kufafanua huku nikitaja tofauti zilizopo baina ya neno Mwanasiasa na Kiongozi.
1. Kiongozi anajali watu/wananchi anaowatumikia; Mwanasiasa anajali chama chake, nafsi yake, familia yake, lakini muhimu zaidi viongozi wake wakuu, hasa waliomteua kushika wadhifa husika. Mara nyingi tumeona jinsi gani wanasiasa wa CCM wamekuwa na unconditional obedience kwa wakubwa waliowateua. Hili linachangia sana matatizo ambayo Lowassa anayazungumzia.
2. Kiongozi ni mtu ambae hufanya maamuzi yanayolenga maslahi ya taifa au jamii inayomzunguka; Mwanasiasa hufanya maamuzi yanayokilinda chama chake, lakini hasa kuwaimarisha wanasiasa au makundi yaliyomfadhili/yaliyompa nafasi yake ya uongozi.
3. Kiongozi uhimiza matumizi ya fedha za walipa kodi kwa ajili ya miradi ya muda mrefu na yenye manufaa kwa jamii/maslahi ya taifa; Mwanasiasa uangalia zaidi miradi ambayo aidha inamnufaisha yeye binafsi katika kipindi chake cha madaraka au pamoja na wote waliomfadhili wadhifa husika;
4. Kiongozi hufukuza kazi watumishi wa umma wasiofaa; Mwanasiasa huwajenga na huwakinga kila wanapofanya maovu;
5. Kiongozi hujifunza kutokana na makosa; Mwanasiasa hakubali makosa, badala yake hujiona yupo sahihi wakati wote;
6. Kiongozi hufanya kazi vyema na wenzake bila ya kujali itikadi za vyama ili mradi ni kwa manufaa ya umma/maslahi ya taifa; Mwanasiasa mara nyingi huwa ni mnafiki, mfitini na mwoga. Mara nyingi, mwanasiasa hutumikia waliomteua au mfadhili wadhifa wake na hivyo huwa anaishi na kufanya kazi katika mazingira yaliyojaa hofu ya kuvuliwa wadhifa alionao, aidha na chama chake au wakubwa zake.
7. Kiongozi wakati wote husema ukweli; kwa Mwanasiasa, ni desturi kuwa muongo na mara nyingi huwekeza zaidi katika kugeuza uongo kuwa ukweli;
8. Na mwisho, katika usimamizi wa fedha za walipa kodi na rasilimali za umma, Kiongozi hujali kubana matumizi yasio ya lazima, na uhimiza matumizi yenye kulenga kuendeleza taifa na watu wake; Mwanasiasa mara nyingi hujikitika zaidi kuhakikisha fedha za walipa kodi na rasilimali za umma zinamnufaisha yeye na familia yake pamoja na wale waliompa fadhili ya uongozi.
Ningependa kuendeleza hoja ya Lowassa katika mazingira ya kuchambua aina ya viongozi waliopo ndani ya CCM. Nimefanikiwa kubaini aina tatu ya viongozi ndani ya CCM kama ifuatavyo:
· Wanaitikadi (Ideologues);
· Wapambe (Jesters);
· Wachochezi (trouble makers);
1. Wanaitikadi (Ideologues) – Ingawa hawa wamebakia wachache na ni wa kauli na sio vitendo, bado ni muhimu tukajadili kundi hili. Katika nchi iliyokomaa kisiasa, kwa kawaida, leaders define themselves in terms of a set of beliefs and values ambazo wanaziamini na kuzi tekeleza, lakini muhimu zaidi ni kwamba they consistently base their political action in the context of ideologies that they believe in. Suala la itikadi limeshajadiliwa sana humu JF lakini
ni muhimu kuhimiza tu kwamba itikadi ni suala la kijamii huku siasa ikiwa ni chombo tu cha utekelezaji wa mtazamo na malengo ya jamii husika. Siasa haizai itikadi, ni jamii ndio huzaa itikadi na siasa hujaribu kutelekeza itikadi husika.
Nchi za wenzetu kuna wanaitikadi (ideologues) wa aina nyingi lakini common zaidi ni liberals, conservatives, moderates n.k. Kwa viongozi wa kisiasa katika jamii hizi ni common practice kujipambanua na kuji position mbele ya umma/jamii kwa vigezo vya itikadi wanazoziamini na kuzisimamia. Vile vile, viongozi wa aina hii hujitofautisha na washindani wao (upinzani) kwa vigezo vya itikadi. Ni jadi misimamo, kauli na matendo yao kushahibiana na itikadi zao na zoezi hili uendela katika maisha yao yote ya uongozi. Ndio maana kwa wenzetu, ideologues die in their ideological boots.
Wanaitikadi wa dhati wameisha CCM. Walipo leo ni wale wanaojaribu kujipambanua kama wana itikadi wa ujamaa, lengo ikiwa ni kuwaadaa wananchi kwani wanatambua kwamba CCM hakikuwaandaa watanzania kuhamia kwenye mfumo wa soko huria kutoka kwenye ule wa awali wa Ujamaa. Watanzania wengi leo hii wamebakia kuduwaa na wasijue jinsi gani ya kukabiliana na maumivu ya sera za soko huria huku viongozi wanaohimiza CCM ni chama cha kijamaa wakiishi maisha ya ubepari uliopitiliza.
2. Wapambe (Jesters) – kundi la pili la viongozi wa CCM lile la wapambe. Hawa wamejaa ndani ya CCM na kwa jadi yao, wakipewa nyadhifa, kazi yao kubwa ni to ‘amuse', ‘cheer' and ‘charm' their masters (waliowapa madaraka). Hivyo ndivyo jinsi wapambe wanavyofanikiwa kuhudumia matumbo yao na familia zao. Enzi za uchifu, hii ilikuwa ni ajira rasmi, lakini katika dunia ya sasa ya serikali ya jamhuri, upambe sio ajira rasmi ingawa wapo wanaoteuliwa kwa vigezo hivi na wapambe hawa ni nuksi kweli kweli. Na ni heri ufarakane au tofautiane na the master kuliko mpambe kwani career-wise, kibiashara na mara nyingine kimaisha unaweza angamizwa. Vinginevyo kila siku tunashuhudia jinsi gani wapambe ndani ya CCM wanatumia nyadhifa walizopewa kiupambe to amuse viongozi waliowapa madaraka lakini muhimu zaidi, kukisaidia CCM to divert attention ya umma/wananchi from major issues of the day. Wapambe wamejaa kwenye majukwaa ya siasa za CCM, lakini wengi zaidi wapo bungeni.
3. Wachochezi (Political trouble makers) – kundi la tatu na la mwisho la viongozi wa CCM ni lile la wachochezi. Kazi kubwa ya viongozi hawa ni kushawishi na bamboozle umma, na wanatumia vyema prejudices na stereotypes zilizopo kwenye jamii yetu kwa maslahi ya CCM. Lakini hasa wakubwa waliowapa madaraka. Tabia na matendo yao viongozi wa namna hii mara nyingi ni very irrational and inhuman. Viongozi wa namna hii hawaheshimu mantiki (logic), human decency, consistency na hawana muda kusoma alama za nyakati.
Wachochezi hustawi na kujiendeleza kisiasa kwa kutengeneza kauli mbiu na misamiati ya ovyo ambayo CCM inaichukua na kujengea hoja na propaganda kwamba huo ndio ukweli uliosadidika, usiopingika na unaotakiwa kuabudiwa. Mtu yoyote ambae anapingana na viongozi wa namna hii, basi watamuita kila aina ya majina – haramia, adui, mhuni, mkabila, n.k, na mara nyingine kujikuta hatarini kimaisha Viongozi wa namna hii kwa kawaida hawana muda wa kuheshimu dhana ya uhuru wa mawazo na huwa hawaoni any merit on a political opponent (mfano tazama tabia na kauli zao dhidi ya upinzani bungeni) na badala yake wanajaribu kuwatuhumu wale wote wanaowa ‘challenge' kwa mbinu za udini, ukabila, ukanda, n.k. Lakini zana muhimu inayotumiwa na wachochezi ni popular prejudices and stereotypes zilizopo katika jamii, na huwa ni mabingwa wa kupika madai na ahadi za uongo ili kujiimarisha kisiasa pamoja na CCM. Viongozi wa namna hii ni mabingwa wa ku-appeal on stereotypes, prejudices, emotions, fears, na expectations za umma kwa kujenga propaganda based on themes za kidini, kikabila, ukanda n.k.
Tumeshuhudia mara kwa mara viongozi wa aina kutwa wakishambulia wenzao na mara nyingi huchangia sana kuchafua hali ya hewa ya kisiasa nchini kwani wana inspire paranoia na kuchochea mgawanyiko. Mbaya zaidi, viongozi wa namna hii hawana muda wa kuja na nguvu ya hoja na badala yake wengi ni wavurugaji na wahujumu wakubwa wa demokrasia.
Kwa mtazamo wangu, iwapo tutaweza kupambanua na kuelewa aina ya viongozi wa CCM kwa njia hii au nyinginezo, hivyo ndivyo tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupata ufumbuzi juu ya jinsi gani kama taifa tutaweza epusha nchi yetu isiingie katika machafuko kutokana na CCM kuyumba kama alivyotabiri baba wa taifa, Mwalimu Nyerere.
Nawasilisha na Nasimama kukosolewa.