Lowassa na Tatizo la Uongozi CCM

Je una maana nje ya Chadema na Lowassa watanzania hawana mbadala? I am sorry but this is a false belief!

The race is still wide open.......but those are the only possibilities we have so far. Come 2014 the political landscape would unfold and we will have a clear prediction of who is who in the race. Otherwise, now is a joke! That's my simple perspective on the matter.
 
I agree, lakini nadhani inabidi na sisi kama wananchi tuanze kuonyesha tuna hitaji viongozi wa namna gani wa kutusogeza mbele kama taifa badala ya kusubiri wanasiasa wajinadi ndani ya vikao vyao halafu tuchaguliwe na kuaminishwa kwamba fulani ndio anafaa. Ndio maana ni muhimu kwa umma kuanza kujadili aina gani ya viongozi wanao hitajika ili wale wasiotosha matakwa ya umma wajiondoe wenyewe mapema. Mijadala hii ni vizuri sana kama pia ina trickle down kwenye jamii, sio kwenye mitandao tu;
 
Tatizo linakuwa kupita kwenye machujio ya chama, wenye uchu wa urais wameisha anza tengeneza "mitandao" yao itakayo wapa support. Labda tukipewa wagombea binafsi..............nayo haitasaidia kwani itahitaji pesa kujinadi. Kama huyo M-binafsi hana pesa, itabidi apate wafadhili (King Makers) na hapo ndio tatizo kubwa.
 
Nadhani utaratibu mpya wa kupata wajumbe wa NEC ambapo unlike before, sasa wengi wanachaguliwa huko huko wilayani na pia idea ya kupunguza mrundikano wa vyeo ni mwanzo mzuri wa kupunguza mianya ya rushwa kwani ilikuwa ni rahisi sana kwa wenye nguvu ya fedha kutuma wapambe wao na maboksi ya fedha kwenye treni kutoka mwanza yenye wajumbe wa mikoa ya mwanza, kagera, mara na shinyanga, and by the time wamefika dodoma, wameshakunywa viloba vya kutosha na chips mayai na tayari wanajua nani ni wa kumpigia kura; pia boti la wajumbe kutoka zanzibar lilikuwa linahujumiwa hivyo hivyo;

Kuhusu wagombea binafsi, mimi nadhani hoja hii itapigwa dana dana kwa visingizio vingi kwamba kuna pre conditions ambazo lazima zijengwe etc kwani kusikia hata viongozi wa kizazi kipya kama Nape wakipingana na hili, ina maana kwa wakongwe wa chama, hili wazo litatupwa kwenye jalala lakini after a lot of false justification.

Tunabakia kujiuliza, Je, tutapataje kiongozi wa kweli mwaka 2015? Mimi i think we should invest zaidi kwenye a bottom - up approach kumpata mtu huyo badala ya top - down approach inayotumika sasa kuaminisha umma kwamba fulani ndio atatufaa. Pamoja na mambo mengine, credible opinion polls zianze sasa kubaini itikadi zilizopo ndani ya jamii ni zipi, misimamo ya jamii in terms of social values mbali mbali, priorities za umma ni zipi, nani wana amini anaweza kutuongoza n.k. Mchakato huu uendane na taasisi nyingine kuendeleza elimu ya uraia kuhusu umuhimu wa social, economic, political and constitutional change na pia nafasi ya wananchi in determining hayo; nadhani tukifanya haya mapema, inawezekana tusifanikiwe sana 2015 lakini hakika chaguzi za baadae zitakuwa na utofauti mkubwa sana in terms of kutupatia viongozi wazuri.
 
Huu mjadala nimeupenda sana, una mambo mengi ya kujifunza na watoa hoja wanaonyesha upeo mzuri na matakwa mema kwa nchi, siyo mijadala ya kishabiki ambayo tumeizoea humu. Hongera mleta maada na wengine.
 
Kama unaongelea viongozi, binafsi nadhani wapo kwa ajili ya kutafutia mwanga familia zao, sio kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania njia; sijui tatizo hili tutalitatua vipi hasa ikizingatia kwamba suala la uzalendo miongoni mwa viongozi limebakia kuwa voluntary;
...Sitaki kuamini kuwa viongozi wote hawajali maslahi ya nchi. Wapo wanaojali -ingawa now and then hupigana vikumbo na kufitiniana kulinda position zao, of which, in politics is a norm- na wanafahamika, kwa matendo yao.

...Lakini, after all is said and done, tuna tatizo kubwa la uongozi, we really do.
 
Mimi i think we should invest zaidi kwenye a bottom - up approach kumpata mtu huyo badala ya top - down approach inayotumika sasa kuaminisha umma kwamba fulani ndio atatufaa.
...In total support. Some people have started doing this homework, i hope others will follow. It is good for the nation.
 
.....nadhani inabidi na sisi kama wananchi tuanze kuonyesha tuna hitaji viongozi wa namna gani wa kutusogeza mbele kama taifa badala ya kusubiri wanasiasa wajinadi ndani ya vikao vyao halafu tuchaguliwe na kuaminishwa kwamba fulani ndio anafaa.
...Wananchi wataweza kufanya hivyo ikiwa tu watakuwa na uelewa wa mahitaji yao kama jamii. Its sad but also true kwamba, wengi hawajui wanahitaji nini kama jamii. Si unaona watu wanapochagua chakula na fedha kidogo wakati wa kampeni, badala ya kiongozi makini atakayesaidiana nao kujiletea maendeleo katika jamii yao.

...They don't bother looking at track record ya vitu alivyofanya na kama timu aliyonayo itamsaidia kutimiza mahitaji yao. Of course, they don't have a clue. Na hapo ndio tunakwama kama waTanzania.
 
You make very valid points. Kwa mtazamo wangu ambao pengine haupo sawa sana, vijijini sio tu kwamba hawana uelewa juu ya nini wanahitaji, but to make matters worse, hawaelewi:

1. Pia wengi hawajui haki zao kikatiba – za kijamii, kisiasa na kiuchumi (economic, social and political justice). Ndio maana kwa wengi, the injustice under CCM hawaitambui sana kutokana na kutokuwa that exposed.

2. Vile vile wengi hawana ufahamu kwamba serikali ina wajibu wa kuwatumikia in terms of huduma za kijamii.

Pia nina mtazamo ufuatao ambao vile vile nao unaweza kuwa haupo sahihi sana. Ni hivi: Tukumbuke kwamba Tanzania is predominantly rural (over 70% of the population) na nchi yetu ni kubwa sana, yenye population ambayo ipo very sparse - watu wengi huko vijijini wanaishi wachache hapa, wachache pale…., ni maeneo machache sana yenye concentration kubwa ya idadi ya watu huku vijijini. Pia katika mazingira haya, hakuna miundombinu ya kueleweka ambayo inaweza kusaidia jamii mbalimbali za vijijini to interact and exchange ideas kuhusu mwenendo na mabadiliko ya dunia, maeneo mengi hayana umeme wa kuwawezesha kuona kwenye TV nini kinaendelea huko nje; kitaifa magazeti yanasomwa na only 1 to 2% of the population, na mengi ni mijini tu; na hata kwa yale yanayofika vijijini, wananchi wengi kule hawawezi kusoma Kiswahili. Wengi wanakisikia Kiswahili lakini Radio stations zinazowafikia barely presents content ambazo ni relevant kuwapa ufahamu kuhusu masuala mbalimbali ya dunia ya sasa. Njia pekee iliyobakia ni kwa vyama vya siasa kwenda kufanya amsha amsha, lakini navyo pia kwa kiasi kikubwa vinakabiliwa na uhaba mkubwa wa resources kufanikisha hilo. Angalau Chadema kimeanza kidogo kulishughulikai hili tatizo.

Kwahiyo katika jamii ya namna hii ambayo generally speaking haina tofauti sana na jamii iliyokutwa na mkoloni, what mattered to most of hawa ndugu zatu vijijini ilikuwa ni intervention ya mkoloni katika maisha yao ya asili ambayo waliyazoea na kuyapenda sana i.e. traditional and subsistence oriented life style. Mkoloni alipowaingilia, ndoto yao ikawa moja tu - kumuondoa mkoloni ili kama jamii, warudie katika hali zao za zamani. Ndio maana harakati za TANU ziliungwa mkono na wengi na hata baadae, ikawa rahisi sana kwa wazo la UJAMAA kukubalika. Lakini tatizo ni kwamba - kwa kiasi fulani, Sera ya Ujamaa ikapalilia tatizo lililopo kwa maana ya kwamba – Ujamaa haukusaidia to bring about modernity, social progress/mobility, na kujenga liberal democracy i.e. [representative democracy inayoendeshwa chini ya misingi ya liberalism, yenye kuhimiza fair, free and competitive elections, rule of law katika maisha ya kila siku, separation of powers, protection of human rights and civil rights kwa watu wote n.k.], badala yake, UJAMAA in large part ulirudisha mfumo wa kikoloni (producing surplus for watawala/elites, urbanites na kwa ajili ya masoko ya nje kwa very low returns), lakini this time around, in a more organized way

Ndio maana muda mfupi baadae, wananchi wengi vijijini wakaanza kupata fatigue ya UJAMAA - kwani ulikuwa unawarudisha kule kule kwa mkoloni – kuzalisha mazao ya biashara zaidi kuliko ya chakula – mazao haya ya biashara kama tunavyojua hayakumfaidisha sana mwanakijiji, na ndio maana wengi kwa kiasi fulani hawakuona tofauti mfumo wa Ujamaa na Ukoloni in terms of uhuru wa kuendeleza maisha yao ya awali yenye kuwapatia uhuru na pia uhakika wa chakula n.k. Pole pole, anything to do with state's intervention kwenye maisha yao ya kila siku begun to be received with hostility. Ndoto yao ikarudi kule kule - to do away with mfumo uliojaa coercion, exploitive state that made them become unnecessarily dependent, lack of freedom and loss of touch with maisha ya enzi za mababu zao.

Leo hii, wananchi wengi vijijini hawana ufahamu or atleast interest juu mfumo wa utawala (RAIS, MAHAKAMA, BUNGE), kwani haya yote hayana much significance kwenye msiaha yao ya kila siku. Wengi wanategemea serikali na mabaraza ya vijiji lakini muhimu zaidi elders wenye busara katika jamii kutoa mwongozo, ushauri na kutatua migogoro mbalimbali. Sasa during political campaigns (san asana ngazi ya urais), wengi wanashindwa kuelewa kwa upana umuhimu wake ni nini, ingawa kwa mazoea na pia mkumbo, wanapiga kura bila kujua thamani ya kura zao. More importantly, kwa wengi, chaguzi ni msimu wa mavuno kama ilivyokuwa kwa msimu wa mavuno ya bidhaa za kilimo ambazo uambatana na kucheza ngoma, kunywa pombe n.k.

Katika suala la wabunge kwenye vijiji kama hivi – wananchi wengi huchagua wabunge kutokana na influence ya wazee katika jamii na vigezo mara nyingi huwa ni personalities - kwamba fulani ni msomi au ana akili au uwezo wa kung'arisha nyota yetu kwa mfano wadigo au wanyaturu kwenye anga ya kitaifa. The ultimate decision making process katika kupiga kura, mbali na kuwa ni msimu mwingine wa kulewa na kupata zawadi, its mainly suala la social status kwani; vinginevyo kwa wengi, kiuchumi wana amini kwamba mungu ndio mweza na mtoaji wa yote (sio serikali), kwahiyo wana furaha ya kuishi maisha yao ya asili kama vile before ukoloni. When it comes to social progress, kwa bahati mbaya au nzuri wameshazoeshwa kujiendeleza kupitia shughuli za kujitegemea - in terms nguvu kazi ya bure na pia michango yao kifedha kama vile kulima barabara, kuchimba visima vya maji n.k; Vinginevyo kama ni suala la mazao ya kilimo, wapo wanunuzi binafsi (sio serikali) ambao wanawapatia bei nzuri zaidi ya vyama vya ushirika chini ya Ujamaa; kama ni huduma za kijamii, zipo NGOs nyingi kwa ajili hiyo, na pia yupo mbunge ambae atafadhili hiki na kile, na hivyo kuiondoa kabisa Serikali katika maisha yao ya kila siku.

Haya ndio mawazo yangu ambayo yametokana na stimulation of my mind baada ya kusoma maoni yako. Nina fahamu yana mapungufu, hayapo structured na hayana takwimu, lakini nadhani kwa kiasi fulani bado yanabainisha changamoto zinazotukabili katika kuleta mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, hasa miongoni mwa watanzania wanaoishi vijijini.
 
Pia nina mtazamo ufuatao ambao vile vile nao unaweza kuwa haupo sahihi sana. Ni hivi: Tukumbuke kwamba Tanzania is predominantly rural (over 70% of the population) na nchi yetu ni kubwa sana, yenye population ambayo ipo very sparse - watu wengi huko vijijini wanaishi wachache hapa, wachache pale…., ni maeneo machache sana yenye concentration kubwa ya idadi ya watu huku vijijini. Pia katika mazingira haya, hakuna miundombinu ya kueleweka ambayo inaweza kusaidia jamii mbalimbali za vijijini to interact and exchange ideas kuhusu mwenendo na mabadiliko ya dunia, maeneo mengi hayana umeme wa kuwawezesha kuona kwenye TV nini kinaendelea huko nje; kitaifa magazeti yanasomwa na only 1 to 2% of the population, na mengi ni mijini tu; na hata kwa yale yanayofika vijijini, wananchi wengi kule hawawezi kusoma Kiswahili. Wengi wanakisikia Kiswahili lakini Radio stations zinazowafikia barely presents content ambazo ni relevant kuwapa ufahamu kuhusu masuala mbalimbali ya dunia ya sasa. Njia pekee iliyobakia ni kwa vyama vya siasa kwenda kufanya amsha amsha, lakini navyo pia kwa kiasi kikubwa vinakabiliwa na uhaba mkubwa wa resources kufanikisha hilo. Angalau Chadema kimeanza kidogo kulishughulikai hili tatizo.
...Kweli kiasi kikubwa cha wananchi kiko vijijini, ambako kuna kila aina ya changamoto za maendeleo ya mwanadamu. Nina hamu ya kuona sensa itatoa figure gani this time around. Tatizo ninaloliona tunalo kama taifa, ni kupuuzia ushauri, tafiti na maoni yenye uelewa juu ya nini kifanyike kuleta maendeleo katika nchi yetu. Kimsingi, watu wa vijijini wanahitaji kupewa umuhimu mkubwa na serikali katika masuala ya elimu na mawasiliano. Namaanisha serikali kuwekeza zaidi katika eneo hili huko. Mijini uwekezaji huu ni rahisi kufanywa na sekta binafsi, bila kupuuzia mchango wa serikali.

...Kwa mtu anayefahamu elimu ya maendeleo atabaini kuwa, ili kuwe na maendeleo ya kweli, lazina watu vijijini waelimike na wawasiliane na wengine popote pale katika nchi kwa urahisi. Kwa nchi yenye wakaazi wengi vijijini. Na ni kweli kwamba, kazi hii si ndogo. Hata hivyo, haimaanishi kuwa haiwezekani, kama baadhi ya wavivu wanavyopenda tuamini.

Kwahiyo katika jamii ya namna hii ambayo generally speaking haina tofauti sana na jamii iliyokutwa na mkoloni, what mattered to most of hawa ndugu zatu vijijini ilikuwa ni intervention ya mkoloni katika maisha yao ya asili ambayo waliyazoea na kuyapenda sana i.e. traditional and subsistence oriented life style. Mkoloni alipowaingilia, ndoto yao ikawa moja tu - kumuondoa mkoloni ili kama jamii, warudie katika hali zao za zamani. Ndio maana harakati za TANU ziliungwa mkono na wengi na hata baadae, ikawa rahisi sana kwa wazo la UJAMAA kukubalika. Lakini tatizo ni kwamba - kwa kiasi fulani, Sera ya Ujamaa ikapalilia tatizo lililopo kwa maana ya kwamba – Ujamaa haukusaidia to bring about modernity, social progress/mobility, na kujenga liberal democracy i.e. [representative democracy inayoendeshwa chini ya misingi ya liberalism, yenye kuhimiza fair, free and competitive elections, rule of law katika maisha ya kila siku, separation of powers, protection of human rights and civil rights kwa watu wote n.k.], badala yake, UJAMAA in large part ulirudisha mfumo wa kikoloni (producing surplus for watawala/elites, urbanites na kwa ajili ya masoko ya nje kwa very low returns), lakini this time around, in a more organized way
...Kimsingi, watawala waliona ni rahisi zaidi kuendeleo kutumia tools za kiutawala za mkoloni, kwani ziliwapunguzia bughudha. Hata hivyo, i can argue kwamba, nazo zimechangia kurudisha maendeleo nyuma. Wananchi wamejiona kama wao ni tabaka tofauti na watawala, katika maana ya mahitaji, matamanio, matazamio na nafasi ya kufaidi nchi yao.

...Kumejengeka imani kwamba, kundi fulani ndilo lenye haki zaidi ya kutumia na kufaidi matunda ya nchi. Hii imechangia pia uzalendo kupotea.

Ndio maana muda mfupi baadae, wananchi wengi vijijini wakaanza kupata fatigue ya UJAMAA - kwani ulikuwa unawarudisha kule kule kwa mkoloni – kuzalisha mazao ya biashara zaidi kuliko ya chakula – mazao haya ya biashara kama tunavyojua hayakumfaidisha sana mwanakijiji, na ndio maana wengi kwa kiasi fulani hawakuona tofauti mfumo wa Ujamaa na Ukoloni in terms of uhuru wa kuendeleza maisha yao ya awali yenye kuwapatia uhuru na pia uhakika wa chakula n.k. Pole pole, anything to do with state’s intervention kwenye maisha yao ya kila siku begun to be received with hostility. Ndoto yao ikarudi kule kule - to do away with mfumo uliojaa coercion, exploitive state that made them become unnecessarily dependent, lack of freedom and loss of touch with maisha ya enzi za mababu zao.
...Wakati tunapata uhuru, vyama vya ushirika vilikuwa na afya nzuri kiuchumi kuliko wakati mwingine wowote. Hii ilisaidia pia vyama hivyo kuwekeza katika elimu, na miradi mingine ya maendeleo. Unaweza kusema kuwa, wakulima walinufaika.

...Hata hivyo, baada ya uhuru, mahitaji ya fedha kwa ajili ya miradi ya kitaifa ya maendeleo, kama, viwanda, vyuo vikuu, n.k., ilibidi yatimizwe kwa kile unachoweza kuiita kumwongezea kodi mkulima, kwa kutwaa vyama vya ushirika, kupanga bei ya mazao na kula cha juu -faida iliyopatikana baada ya kuuza nje mazao hayo- bila kujali mkulima anaathirika vipi.

...Hii ikichangiwa na usimamizi mbaya wa vyama hivi, uliochangia kuviua na hivyo kuua uzalishaji na kipato cha mkulima, na kuongeza umasikini.

Leo hii, wananchi wengi vijijini hawana ufahamu or atleast interest juu mfumo wa utawala (RAIS, MAHAKAMA, BUNGE), kwani haya yote hayana much significance kwenye msiaha yao ya kila siku. Wengi wanategemea serikali na mabaraza ya vijiji lakini muhimu zaidi elders wenye busara katika jamii kutoa mwongozo, ushauri na kutatua migogoro mbalimbali. Sasa during political campaigns (sana sana ngazi ya urais), wengi wanashindwa kuelewa kwa upana umuhimu wake ni nini, ingawa kwa mazoea na pia mkumbo, wanapiga kura bila kujua thamani ya kura zao. More importantly, kwa wengi, chaguzi ni msimu wa mavuno kama ilivyokuwa kwa msimu wa mavuno ya bidhaa za kilimo ambazo uambatana na kucheza ngoma, kunywa pombe n.k.
...Elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yeyote. Kama jamii haijaelimika, hata ukivutia wawekezaji -wa nje na hata wa ndani- hawatawekeza, kwa kuwa hawatapata wafanyakazi wanaowahitaji. Vile vile kutumia ujinga wa watu kama political capital ni janga, kwani utakuwa unakuza duara la umasikini. Si itabidi waendelee kuwa wajinga ili na kesho uwatumie, kama jana.

Katika suala la wabunge kwenye vijiji kama hivi – wananchi wengi huchagua wabunge kutokana na influence ya wazee katika jamii na vigezo mara nyingi huwa ni personalities - kwamba fulani ni msomi au ana akili au uwezo wa kung’arisha nyota yetu kwa mfano wadigo au wanyaturu kwenye anga ya kitaifa. The ultimate decision making process katika kupiga kura, mbali na kuwa ni msimu mwingine wa kulewa na kupata zawadi, its mainly suala la social status kwani; vinginevyo kwa wengi, kiuchumi wana amini kwamba mungu ndio mweza na mtoaji wa yote (sio serikali), kwahiyo wana furaha ya kuishi maisha yao ya asili kama vile before ukoloni. When it comes to social progress, kwa bahati mbaya au nzuri wameshazoeshwa kujiendeleza kupitia shughuli za kujitegemea - in terms nguvu kazi ya bure na pia michango yao kifedha kama vile kulima barabara, kuchimba visima vya maji n.k; Vinginevyo kama ni suala la mazao ya kilimo, wapo wanunuzi binafsi (sio serikali) ambao wanawapatia bei nzuri zaidi ya vyama vya ushirika chini ya Ujamaa; kama ni huduma za kijamii, zipo NGOs nyingi kwa ajili hiyo, na pia yupo mbunge ambae atafadhili hiki na kile, na hivyo kuiondoa kabisa Serikali katika maisha yao ya kila siku.
...Hapo ndio kazi ilipo. Kizazi hicho hakitoweza kujibidiisha kufanya kazi hata siku moja.

Haya ndio mawazo yangu ambayo yametokana na stimulation of my mind baada ya kusoma maoni yako. Nina fahamu yana mapungufu, hayapo structured na hayana takwimu, lakini nadhani kwa kiasi fulani bado yanabainisha changamoto zinazotukabili katika kuleta mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, hasa miongoni mwa watanzania wanaoishi vijijini.
...Ndugu yangu, pamoja na kwamba takwimu ni muhimu, hata hivyo haya ni majadiliano mepesi yasiyohitaji kuthibitishiana hoja kwa takwimu. Nimeona takwimu mbili, tatu, hapo juu!
 
lowasa 'AKUNAGA'kama unabisha ukawaulize wakina Nepi na mzee Sittakinataka na nyimbo zao za magamba kiko wapi!?
 
lowasa 'AKUNAGA'kama unabisha ukawaulize wakina Nepi na mzee Sittakinataka na nyimbo zao za magamba kiko wapi!?

Siasa za Lowassa hakunaga hazitusaidii; moja ya matatizo makubwa yanayotukabili ni vyama vyetu vya siasa kuendeshwa na nguvu ya personalities badala ya itikadi; kama wenzetu kwa mfano wa marekani wangekuwa na siasa za JFK hakunaga, au Lincoln hakunaga, na hawa wote hawapo tena duniani, vyama vyao vingekuwa vipo mpaka leo kweli? Ushauri wangu ni kwamba pamoja umuhimu wa kuwa na mapenzi na viongozi, lakini tuwe na upeo zaidi kwani CCM inatakiwa iendelee kuwepo na kuzidi kushamiri whether Nape, Lowassa au Sitta wapo au hawapo;vile vile chadema, whether Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika, etc wapo au hawapo; hapo ndipo tutakuwa tunajivunia kuwa na demokrasia iliyokomaa na pia ushindani wa kisiasa wenye tija kwa wananchi;
 
Nimeipenda article yako na uchambuzi wako makini, hayo maneno ni kweli ila ningependa kuongeza kidogo kwa kulingana na wakati huu wa vyama vingi. Ni kweli kuna wanasiasa na viongozi wa siasa lakini ukumbuke kwenye demokrasia ya kweli vyama vyote nguli vya siasa huwa vina faction(makundi) ndani yake, kwa hiyo sio kitu cha ajabu kuona CCM nayo ikiwa hivyo ni kitu cha kawaida kwa chama ambacho ni kikongwe kuliko vyote hapa nchini, hata CDM na CUF wanaelekea hukohuko suala ni muda au siku wakishika madaraka tutayaona hayo kwao pia.

Tatizo jingine kwenye demokrasia ya vyama vingi ni rahisi ukiwa mpinzani i.e. CDM au CUF kuonyesha udhaifu wa utawala bila hata kueleza wewe utafanyaje tofauti, ni rahisi siku zote kukosoa ila ngumu kuongoza. Ila kwa hili tuliliona wazi kwenye bajeti mbadala pale CDM walipochemka na kutoa bajeti yao ambayo hata wanachama wao waliona ina mapungufu(i.e. haikuleza wapi watatoa mapato yao) mengi zaidi ya ile ya serikali.

Vilevile kwenye demokrasia ya vyama vingi wanasiasa wengi hujikita zaidi kwenye populist agenda sababu wanaangalia uchaguzi ujao na hili tatizo sio kwetu tu hata kwa nchi zilizoendelea i.e. US na UK ni hivyohivyo wanaangalia na watu wanataka matokeo now!! na ndio tofauti na China ambayo kwa vile ni chama kimoja wana uwezo wa kuangalia mbali na kupanga mambo yao bila kujali wananchi wao na kuleta maendeleo ya muda mrefu.

hii ndiyo tatizo la democracy kwa nchi maskini..wapinzani wakiwa nje wanaona kila kitu hawa tunawaita counter elites or elites out of power, wakiingia ndani wanakua elites in power na hapo tayari wako elevated wanakua mabwana wakubwa wanashindwa kufanya kilichowapeleka pale. Wanabaki kua busy na siasa kuhakikisha kua wanabaki kwenye dola ikiwa ni pamoja na kukandamiza wale ambao ni wapinzani sasa.

Kuna watu wanasema demokrasia kwenye traditional societies kama zetu (elimu duni, umaskini, upeo mdogo, imani za jadi, kukosekana kwa taasisi zenye nguvu na huru za kitaifa) ni anasa tu.

Na hili ni tatizo Afrika yote kuamini upinzani tu wa kisiasa unaweza kua ni suluhisho la matatizo yetu. Tunahitaji zaidi CSO's kuliko vyama hivi vya siasa na electoral politics. Ila kujenga demokrasia ya kweli unahitaji taasisi huru za kitaifa, CSO's, vyama makini vya siasa vyenye agenda na malengo yanayoeleweka (zaidi ya kuingia tu ikulu) na ili kuyafikia haya tunahitaji elimu zaidi.

Hata hii katiba mpya ikiwa nzuri kiasi gani (kumpa nguvu mwananchi) bado tutashindwa kufikia malengo yetu ya kitaifa kimaendeleo kwa ujumla kwa sababu ya ukosefu wa upeo na elimu inayotufanya kua washiriki kikamilifu kwenye demokrasia yetu kwa kuzipa taasisi zetu mbali mbali za kidemokrasia nguvu ya kweli na siyo tu ya kwenye karatasi. Bila elimu sawa sawa hatuwezi kujipanga kudai haki zetu kwa nguvu na kua na ushawishi mzuri katika demokrasia yetu zaidi ya kutumika kutimiza tu maslahi ya wanasiasa.

Mfano kwenye red hapo nimekua nikijiuliza swali hili hili hawa CDM wataongeza vipi pato la taifa? kwa kodi zaidi, kuomba zaidi nje, maana yake hata ukizuia misamaha ya kodi na kubana mianya ya ufisadi kuokoa haka kakipato chetu unachookoa hapo bado ni kidogo kutekeleza haya majukumu makubwa na inakubidi uje na mbinu za kuongeza pato.

Wananchi wa kawaida hawajiulizi hili wanashabikia tu na kujipa matumaini ya uongo mwisho wa siku tunakuja kupoteza matumaini kama taifa na utaifa wetu kabisa.
 
Nyerere alimaliza shule akawa mwalimu akafundisha kidogo akajikita kwenye siasa moja kwa moja.

Mwinyi sina hakika sana na background zake za kazi lakini nadhani na yeye hana zaidi ya mambo ya kisiasa kwenye CV yake.

Mkapa angalau kidogo alijitahidi kama mtumishi wa umma lakini alifanya kazi kwenye magazeti ya Chama , wakati ule hizo kazi ni kama za kisiasa maana magazeti yalikuwa kwa ajili ya propaganda zaidi. Baada yapo mkuu wa wilaya etc

Kikwete alipomaliza shule akaingia TANU then CCM akaenda Monduli akafundisha chuo cha jeshi lakini hata yeye hana zaidi ya siasa kutoka Zanzibar , Singida, Mtwara nk kote kama mtumishi wa Chama.

Ndoto yangu siku moja tupate rais ambaye ana background ya Private sector mtu ambaye Lawyer ame practice, Banker, Doctor , Engineer, CEO,CFO, Manager, Enterpreneur, etc alete ladha tofauti hapo Magogoni. Hawa watu wenye background za chama na serikali huwa mtazamo wao wakiserikali serikali. Speed yao inakuwa ndogo wanaamini kila kitu kina take time.

Lete CEO wa benki mpe urais uone kama hajaanza kuwafanyia Performance appraisal mawaziri na wao wataenda kwa watu wao chini kufanya the same. Halafu uone huduma za umma zitakavyobadilika. Tatizo tunapenda sana watu wanaoweza kucheza na maneno :happy:

kuna kitu nilisoma kuhusu China na Deng Xiaoping kuhusu kubadilisha china kutoka kwenye kujikita kwenye siasa zaidi hadi kua efficient bureaucratic machine inayoongozwa na wataalamu haswa haswa engineers.

Promotion ndani ya chama na uongozi wa juu unafanywa kwa kuangalia matokeo ya kazi na si siasa na mtu yeyote mwenye background ya siasa siasa kwa sana bila ya kua technocrat kwenye mfumo wao hapati nafasi.

Deng mwenyewe aliwahi sema kwenye mkutano mmoja ili kutohamasisha hotuba ndefu za kusifiana na itikadi zisizo na msingi "if you have nothing to say save your breath the purpose of holding meetings and talk in them is to solve problems".

Tanzania inahitaji technocrats siyo wanasiasa hawa wanacheka cheka na kupiga sound bites ili wapate press time. Mkapa alijitahidi kuweka technocrats kwenye baraza lake (maprof na Phds wengi tofauti na Mwinyi aliyekua na wanasiasa wengi) na tuliona matokeo japo kidogo. Fikiria tupate kiongozi wa aina hii na baraza lake miaka 10 nchi inakua kwenye mstari na utamaduni mpya wa uongozi unazaliwa utakaodumu kwa vizazi vingi vijavyo.
 
....yet himself (Mkapa) was not a PhD, and neither pursued nor accepted even an honorary one...
 
...Nina hamu ya kuona sensa itatoa figure gani this time around. Tatizo ninaloliona tunalo kama taifa, ni kupuuzia ushauri, tafiti na maoni yenye uelewa juu ya nini kifanyike kuleta maendeleo katika nchi yetu. Kimsingi, watu wa vijijini wanahitaji kupewa umuhimu mkubwa na serikali katika masuala ya elimu na mawasiliano. Namaanisha serikali kuwekeza zaidi katika eneo hili huko. Mijini uwekezaji huu ni rahisi kufanywa na sekta binafsi, bila kupuuzia mchango wa serikali.

Kinachosikitisha ni suala la Sensa kuingia siasa. Kipimo cha uongozi pia kipo hapa. Mimi sijawahi sikia katika nchi yoyote Census inakuwa Censored, kwa mfano viongozi wa serikali kupiga marufuku hiki au kile kisijumuishwe wakati wa zoezi hili. Unless kama kuna vitu ambavyo tunataka kuvificha na havina maslahi kwa taifa. Vinginevyo kwa uelewa wangu, zoezi hili hata Umoja wa mataifa unahimiza umuhimu wake – kwamba lifanyike kila baada ya miaka kumi kwa imani kwamba huu ni muda tosha kwa nchi kuweza pata takwimu muhimu kuhusu wananchi wake.
Mimi sidhani kama viongozi wetu wanafanya kila jitiada kuhakikisha umma unahamasika na zoezi hili. Pengine kwao ni mradi mwingine wa kulipana posho na kupenyeza fedha za walipa kodi kijanja kwenda kwenye mradi huo kisha zichukuliwa juu kwa juu kwa matumizi mengine bila ya ridhaa ya walipa kodi au wawakilishi wao (wabunge). Vinginevyo, fundamentally, census inasaidia kuipa serikali facts muhimu kwa kwa ajili ya kuandaa sera na mipango ya Maendeleo;

Findings za sensa ni muhimu sana katika decision making zenye kulenga to facilitate the development of socio-economic policies, kwa nia ya kuleta/kuboresha ustawi wa jamii; hata kwa sekta binafsi ambayo umeitaja, findings za census ni muhimu kwa sekta hii kujua wapi wafanye allocation or reallocation of businesses, wapi wapeleke bidhaa au huduma gani n.k. Lakini Tatizo ni kwamba Viongozi wetu hawawekezi katika kuelimisha umma umuhimu wa sensa ili wananchi wajue faida zake kwa maisha yao, san asana viongozi wetu ni kuwatisha na kuwachanganya tu wananchi juu ya zoezi hili kwa malengo ya kisiasa. By the way, uchaguzi mkuu is only three years away, what a political timing for the ruling elite!!

...Kumejengeka imani kwamba, kundi fulani ndilo lenye haki zaidi ya kutumia na kufaidi matunda ya nchi. Hii imechangia pia uzalendo kupotea.

...Elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yeyote. Kama jamii haijaelimika, hata ukivutia wawekezaji -wa nje na hata wa ndani- hawatawekeza, kwa kuwa hawatapata wafanyakazi wanaowahitaji. Vile vile kutumia ujinga wa watu kama political capital ni janga, kwani utakuwa unakuza duara la umasikini. Si itabidi waendelee kuwa wajinga ili na kesho uwatumie, kama jana.

Mapungufu ya Uongozi miongoni mwa wanasiasa wetu pia yanajitokeza katika suala la usimamizi wa sekta ya elimu. Kama tunavyozidi kushuhudia, sekta ya elimu ni janga kubwa, ila worse, it is a timing bomb. Baada ya ujio wa soko huria na ulegezaji wa uchumi, sekta ya elimu nayo ikageuka kuwa bidhaa inayoshindaniwa kwa nguvu za soko. Key decision makers katika sekta hii (public schools) hawana interests tena zaidi ya kutumia ajira zao kwenye sekta kama sehemu ya ulaji. Tukumbuke kwamba Sekta ya elimu hii ina wadau wa aina mbili: Kwanza ni wazazi, wanafunzi, local leaders (viongozi wa vijiji, mitaa), na walimu; Kundi la pili ni watungaji sera, mitaala, na wasimamizi wa sekta ambao nimewazungumzia (hawa wapo huko wizarani na kwenye relevant departments/institutions). Tatizo ni kwamba, tangia elimu ipewe bei price tag inayoendana na ubora wa elimu (ndani ya soko huria), watunga sera na wasimamizi wa sekta hii licha ya kwamba wengi wao watoto wao hawaendi katika shule hizi, bado ndio wenye kauli na maamuzi ya mwisho kuhusu muhstakabali wa shule zetu za umma (public schools) ambazo majority ya watoto wanaoenda shule hizi ni watoto wa maskini. Hapa ndio chanzo cha tatizo!!

Viongozi hawahitaji kuwa na upeo wa ziada kuelewa kwamba like kundi la kwanza la wadau (wazazi, wanafunzi na local leaders) ndio inatakiwa liwe na kauli kubwa na pia influence juu ya maendeleo ya sekta hii kwani kundi hili ndilo linakuwa ‘directly affected’ na maamuzi yanayofanywa kisera. Badala yake, kundi hili mawazo yao hayasikilizwi, concerns zao hazipewi uzito unaostahili, huku kundi lile la pili likiendelea kutunga sera na kutoa maamuzi in a top – down fashion (bila ya kujali mahitaji ya kundi la kwanza ni yepi), na matokeo yake ndio balaa tunaloendelea kushuhudia likizidi kujengeka kila kukicha. Sijui kwa nini viongozi wetu wanaidanganya kwamba hakuna tatizo au kwamba vitisho vya mahakama vikifanikiwa, basi hali imerudi shwari. Wanashindwa kuelewa kwamba hakuna mgomo mbaya kama mgomo baridi.

Lakini education administrators and policy makers hawajali kwani watoto wao hawasomi shule zinazokabiliwa na changamoto hizi, kwani wengi wao wana watoto kwenye shule binafsi za ndani na nje ya nchi; matokeo yake yanashahabiana na hoja yako kuhusu “kujengeka kwa kundi fulani linalojihisi kwamba ndio lenye haki ya kufaidi matunda ya nchi yetu” – kwani chini ya mfumo huu wa dual system ya elimu (elimu inferior na ile superior), viongozi wetu (aidha kwa kujua au kutojua) wanajenga taifa la watanzania wa matabaka mawili yanayochochewa na dual system ya sekta ya elimu – mfumo mmoja ukiwa inferior to the other; tayari jamii yetu inakabiliwa na tofauti kubwa sana za kipato; tayari tuna makabila mengi sana na dini kuu mbili huku kila upande ukihisi kwamba historia ya nchi yetu haikuitendea haki; sasa tunajiongezea tatizo kubwa zaidi ambalo tolerance itakuwa ngumu (ikilinganishwa na tolerance dhidi ya udini na ukabila ambayo tumefanikiwa sana); matabaka mapya yatayotokana na tofauti za mfumo wa elimu zitaipasua nchi yetu vipande vipande, na watakaoumia zaidi itakuwa the privileged (watoto wa policy makers and decision makers) kwani watakuwa wachache kulinganisha na wale ambao watakuwa under privileged;
 
hii ndiyo tatizo la democracy kwa nchi maskini..wapinzani wakiwa nje wanaona kila kitu hawa tunawaita counter elites or elites out of power, wakiingia ndani wanakua elites in power na hapo tayari wako elevated wanakua mabwana wakubwa wanashindwa kufanya kilichowapeleka pale. Wanabaki kua busy na siasa kuhakikisha kua wanabaki kwenye dola ikiwa ni pamoja na kukandamiza wale ambao ni wapinzani sasa.
...My friend, let me take you head on. Nionyeshe nchi maskini yenye demokrasia ya kweli?....ipi, Zambia? Ingawa inafahamika kwamba nchi hiyo is as far as poor africa can get in democracy.

...Ukweli ulio wazi ni kuwa, hata "wapinzani" wakichukua nchi there is not much they can change. Kwa kuwa, nchi ishavurugika kabisa, and we are nearing the state of anarchy. Sasa, itabidi wafanye kazi kubwa kuweka mambo sawa, na hiyo itatokana na vitu vikuu viwili. First, their political capital [how they are being trusted by the people, especially on reforms]. Second, how much economic health we'll be left with, to carry those -at times- costly reforms. For sure, as things stands, the last one will be the most challenging.

Kuna watu wanasema demokrasia kwenye traditional societies kama zetu (elimu duni, umaskini, upeo mdogo, imani za jadi, kukosekana kwa taasisi zenye nguvu na huru za kitaifa) ni anasa tu.
...Wakati mwingine, hakuna formula ya kupata demokrasia, maendeleo, n.k. iliyo rasmi kwa jamii fulani fulani. Nakubaliana nawe kwamba strong and somewhat independent institutions ni muhimu kwa demokrasia kushamiri, hata hivyo kuwa na demokrasia katika jamii fulani ni mchakato. Infact, kuzaliwa kwa demokrasia ndio huleta hizo taasisi huru na zenye nguvu.

Na hili ni tatizo Afrika yote kuamini upinzani tu wa kisiasa unaweza kua ni suluhisho la matatizo yetu. Tunahitaji zaidi CSO's kuliko vyama hivi vya siasa na electoral politics. Ila kujenga demokrasia ya kweli unahitaji taasisi huru za kitaifa, CSO's, vyama makini vya siasa vyenye agenda na malengo yanayoeleweka (zaidi ya kuingia tu ikulu) na ili kuyafikia haya tunahitaji elimu zaidi.
...Now, lets be real. Katika hali kama ya kwetu kwasasa, unategemea kwamba tusipokuwa na vyama vya siasa na uchaguzi tutapata hizo taasisi? Labda utufahamishe, zitazaliwa vipi?

...Je, unafahamu kwamba ni vyama hivi vya siasa na uchaguzi at least ulio huru, ndio uliopelekea kufahamika, kufichuliwa, na kuchukuliwa -angalau- hatua dhidi ya uozo mwingi, na kuwafanya watendaji kukaa chonjo?

Hata hii katiba mpya ikiwa nzuri kiasi gani (kumpa nguvu mwananchi) bado tutashindwa kufikia malengo yetu ya kitaifa kimaendeleo kwa ujumla kwa sababu ya ukosefu wa upeo na elimu inayotufanya kua washiriki kikamilifu kwenye demokrasia yetu kwa kuzipa taasisi zetu mbali mbali za kidemokrasia nguvu ya kweli na siyo tu ya kwenye karatasi. Bila elimu sawa sawa hatuwezi kujipanga kudai haki zetu kwa nguvu na kua na ushawishi mzuri katika demokrasia yetu zaidi ya kutumika kutimiza tu maslahi ya wanasiasa.
...Tuko pamoja! Ila, unafahamu kazi ya kuelimisha jamii inavyozidi kufanywa siku hadi siku, na watu kama HakiElimu?

...Vuta subira ndugu, kazi kama hizo huchukua miaka kadhaa kuonyesha mafanikio yeyote.

Nimekua nikijiuliza swali hili hili hawa CDM wataongeza vipi pato la taifa? kwa kodi zaidi, kuomba zaidi nje, maana yake hata ukizuia misamaha ya kodi na kubana mianya ya ufisadi kuokoa haka kakipato chetu unachookoa hapo bado ni kidogo kutekeleza haya majukumu makubwa na inakubidi uje na mbinu za kuongeza pato.
...Swali la msingi kabisa. Hata hivyo haimaanishi kwamba hamna mtu kwasasa atakayeweza kuongeza mapato ya nchi. Ukiweka mazingira rafiki ya uwekezaji -hasa wa ndani- , ukapunguza rushwa -hasa katika utoaji huduma na haki- , Ukawekeza katika miundo mbinu [nadhani inafahamika], utakuwa umewatendea haki sana waTanzania katika kuwakwamua kwenye tope la umasikini. Hatimae, wakichangamkia fulsa hiyo, utaongeza kipato cha nchi.

Wananchi wa kawaida hawajiulizi hili wanashabikia tu na kujipa matumaini ya uongo mwisho wa siku tunakuja kupoteza matumaini kama taifa na utaifa wetu kabisa.
...Tusipoweza kujiuliza maswali haya na mengine mengi kama wananchi, basi, hatuna chetu na hakuna wa kumlalamikia.
 
kuna kitu nilisoma kuhusu China na Deng Xiaoping kuhusu kubadilisha china kutoka kwenye kujikita kwenye siasa zaidi hadi kua efficient bureaucratic machine inayoongozwa na wataalamu haswa haswa engineers.
...I admire what that leader did to his country. Wamarekani wana msemo unaoenda kama hivi....."it is the economy, stupid". It tells a lot, of a society.

Promotion ndani ya chama na uongozi wa juu inafanywa kwa kuangalia matokeo ya kazi na si siasa na mtu yeyote mwenye background ya siasa siasa kwa sana bila ya kua technocrat kwenye mfumo wao hapati nafasi.
...I bet kama wenyewe wanasoma huu ukweli, na kuuelewa.

Tanzania inahitaji technocrats siyo wanasiasa hawa wanacheka cheka na kupiga sound bites ili wapate press time. Mkapa alijitahidi kuweka technocrats kwenye baraza lake
...Amen.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom