Lowassa na Kiingereza chake!

Lowassa na Kiingereza chake!

Kujua kingereza sio shida ndio maana WAchina wanaenda na wakalimani
 
Mkuu suala la kuongea kiingereza kwa shida haina maana kuwa huyo mtu hajui kiingereza,maana hiyo elimu aliyonayo ameipata kwa lugha ya kiingereza,sasa ukiniambia hajui kiingereza nitakushangaa. Kuongea kiingereza kwa shida ni tatizo la wengi ila halina maana kuwa hawajui.

Mkuu kutokujua kiingereza au kuongea kiingereza kwa shida bado ni aibu kwa Taifa. Kiingereza kama kilivyo kiswahili kuwa lugha yetu ya Taifa ilitakiwa tukiongee vizuri bila kusitasita!! Kushindwa kufanya hivyo ni dalili za elimu mbovu tuliyopewa na CCM. Imagine mtu aliyesoma miaka ya 70 anapata kigugumizi, sasa sisi wa miaka ya 90 kabla hata ya academy inakuwaje!!?
 
kwani kujua kiingereza hadi uwe na lafudhi ya Obama¿

misamiati na tungo sahihi ndo kujua lugha.

lakini kujua pia jinsi ya kutamka. hivi kweli kutamka "sorry" kama "soree" ni sawa?
 
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri

umesahau jamaa alisomea mazingaombwe
 
Last edited by a moderator:
kiingereza ni lugha ya waingereza. we leo ukijifunza kispanish, au kirussia, tukucheke kwa sababu hujui vizuri?? kwani ni lugha yako ya kuzaliwa?....kujua kingereza sana sio sifa nzuri, ni dalili ya kutawaliwa kiutamaduni (cultural imperialism)

Wapo tele hapa omba omba na ki English chao cha kuzaliwa. None sense innit! 😀
 
Mkuu kutokujua kiingereza au kuongea kiingereza kwa shida bado ni aibu kwa Taifa. Kiingereza kama kilivyo kiswahili kuwa lugha yetu ya Taifa ilitakiwa tukiongee vizuri bila kusitasita!! Kushindwa kufanya hivyo ni dalili za elimu mbovu tuliyopewa na CCM. Imagine mtu aliyesoma miaka ya 70 anapata kigugumizi, sasa sisi wa miaka ya 90 kabla hata ya academy inakuwaje!!?

Ushawahi kufikiri kwa nini watu huongea kiingereza kwa shida? Na si hapa afrika.
 
Mbona kaongea vizuri kbs.Ulitaka aongee kama Hashim Thabit wabongo tunawadudu na funza kichwani sio bure.

T

Umenena Mkuu, mfano hapo Kama anayemsikiliza ni Mzungu wala asingeshangaa! Mtu mwenye matatizo ni huyu huyu mweusi mwenzetu tena mwingine anamshangaa Lowasa ukimwambia aongee yeye unakuwa vioja, huu ulimbukeni mkubwa sijui utaisha lini?
 
Mkuu kutokujua kiingereza au kuongea kiingereza kwa shida bado ni aibu kwa Taifa. Kiingereza kama kilivyo kiswahili kuwa lugha yetu ya Taifa ilitakiwa tukiongee vizuri bila kusitasita!! Kushindwa kufanya hivyo ni dalili za elimu mbovu tuliyopewa na CCM. Imagine mtu aliyesoma miaka ya 70 anapata kigugumizi, sasa sisi wa miaka ya 90 kabla hata ya academy inakuwaje!!?
Taaluma na Lugha ni vitu viwili tofauti, Taaluma hupatikana kwa kichina, kireno, kihispania, kijerumani nk, kuongea kingereza si Usomi na kutojua kingereza si Aibu kwani si Lugha mama ya Taifa, wapo Marais kibao hawajui kingereza na wakienda kule UN hutoa Hotuba kwa Lugha zao mama hawakuendekezi kingereza Kama malimbukeni wa Tanzania.
 
Ushawahi kufikiri kwa nini watu huongea kiingereza kwa shida? Na si hapa afrika.

Kwa sababu si Lugha yao mama pia Wazungu wenye Lugha hiyo hawana shida hata ukichapia huwa hawakushangai ! Wakosoaji wa Lugha wapo huku huku tunao humu humu, Yaani watu weusi huwa hawaishiwi vioja.
 
Umenena Mkuu, mfano hapo Kama anayemsikiliza ni Mzungu wala asingeshangaa! Mtu mwenye matatizo ni huyu huyu mweusi mwenzetu tena mwingine anamshangaa Lowasa ukimwambia aongee yeye unakuwa vioja, huu ulimbukeni mkubwa sijui utaisha lini?
Tumekariri good english lazima uongee American Accent.Ila tutaamka tuu.
 
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri

Raisi wa china hajui kingereza amepoteza nn kuwa na akili ww
 
Last edited by a moderator:
Kizuri sana ukilinganisha na kiingereza cha Ji Jinping wa China au Kagame wa Rwanda ... Putin et al ... its all about deliverables .... Lowassa Jembe la Ukweli ...
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri

Last edited by a moderator:
Taaluma na Lugha ni vitu viwili tofauti, Taaluma hupatikana kwa kichina, kireno, kihispania, kijerumani nk, kuongea kingereza si Usomi na kutojua kingereza si Aibu kwani si Lugha mama ya Taifa, wapo Marais kibao hawajui kingereza na wakienda kule UN hutoa Hotuba kwa Lugha zao mama hawakuendekezi kingereza Kama malimbukeni wa Tanzania.
Limbukeni namba moja ni lowassa kwa kujikakamua kuongea iko kiingereza chake,kulikua na ulazima gani kwani,Si angeongea lugha anayoimudu tu,kumbe ushamba wa kubabakia viingereza unawasumbua mpaka marais watarajiwa sio walevi tu!
 
Mswahili eti akijua kingereza na yeye anataka aongee kwa kubana pua Kama Raia wa America, huu ulimbukeni unapaswa ukemewe kwa nguvu kwani Wenye Lugha Yao wao hawana shida kwenye matamshi na hata ukiongea kingereza kibovu wanakuelewa pasipo kukushangaa kwani wanajua kuwa wewe haukuzaliwa London.
 
Taaluma na Lugha ni vitu viwili tofauti, Taaluma hupatikana kwa kichina, kireno, kihispania, kijerumani nk, kuongea kingereza si Usomi na kutojua kingereza si Aibu kwani si Lugha mama ya Taifa, wapo Marais kibao hawajui kingereza na wakienda kule UN hutoa Hotuba kwa Lugha zao mama hawakuendekezi kingereza Kama malimbukeni wa Tanzania.

Mkuu hatuongelei Kiingereza kama taaluma bali kama lugha ya Taifa. kwa kuwa tumechagua Kiingereza kuwa lugha Taifa na ni ya kufundishia ni lazima tuielewe na kuimaster. Failure to do that ni KUSHINDWA KWA ELIMU!! Haiwezekani tuamue kutoa elimu kwa kiingereza halafu siku kijana anahitimu hawezi hata kujieleza kwa lugha aliyofundishiwa. Kwenda kutoa hotuba UN that is something else. Kama tungekuwa hatufundishwa kwa kiingereza au kama Kiingereza kisingekuwa ni lugha ya Taifa sidhani kama tungekuwa tunabishana hapa!!
 
Anaongea Kiswahili kwa ufasaha na kiingereza cha kijifunza, yuko vizuri. Labda ingine.
 
Kizuri sana ukilinganisha na kiingereza cha Ji Jinping wa China au Kagame wa Rwanda ... Putin et al ... its all about deliverables .... Lowassa Jembe la Ukweli ...

Acha ujinga,kagame anaalikwa kutoa mada kwenye vyuo vikuu ughaibuni na anaongea na wasomi wale very comfortable kiingereza,hajikakamui kama huyu mwanaume wenu wa shoka hapo kideoni,tafute video za kagame akiongea kiingereza zipo nyingi tu u tube,ya lowassa ni hii moja tu,hakurudia tena kuthubutu kuongea tena hadharani,
 
Limbukeni namba moja ni lowassa kwa kujikakamua kuongea iko kiingereza chake,kulikua na ulazima gani kwani,Si angeongea lugha anayoimudu tu,kumbe ushamba wa kubabakia viingereza unawasumbua mpaka marais watarajiwa sio walevi tu!

Lowasa ameongea akaeleweka hata waingereza wangemsikiliza wenyewe wasingesema neno kwani wanajua kuwa Lugha Yao si Lugha ya waafirika, wanafahamu Tz kuna lugha zetu za asili Kiswahili nk, Mtu anayekuwa na kimbele mbele kukosoa Ligha huwa ni hawa hawa Watanzania malimbukeni ambao wanaodhani ukiongea Kama Obama ndiyo unajua kingereza.
 
Back
Top Bottom