Lowassa: Masikini hafai kuingia Ikulu!

Lowassa: Masikini hafai kuingia Ikulu!

Alisema Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi sana hivyo watu wake hawapaswi kuwa masikini. ”Nikiingia Ikulu nitaendesha nchi kwa mchakamchaka....siombi nafasi hii kwenda Ikulu tu, Ikulu mimi napafahamu,” alisema na kuongeza;. “...Wala sina njaa, Mwenyezi Mungu amenijalia kuwa nacho kidogo kwa hiyo siendi pale Ikulu kujitafutia bali ni kwenda kupambana ili wananchi waondokane na umasikini….

umasikini umekithiri, nami nauchukia sana umasikini,” alisema Lowassa na kusisitiza kuwa, kiongozi masikini hafai kuingia Ikulu kwani hatakuwa na jipya.

“Nashangazwa na baadhi ya wagombea wanaojinadi kuwa eti wanaweza kuongoza nchi kwa kuwa wao wanatoka kwenye familia masikini. Kiongozi anayesujudu umasikini msimchague,” alisema na kuongeza; “...Nchi hii inakabiliwa na changamoto nyingi; sasa kama kiongozi naye atakuwa masikini atawaongozaje watu masikini?” Alihoji Lowassa.
Huyu mtu hafai kabisaa! Kwake criterion # 1 ya kuingia Ikulu ni utajiri! Na hapa naona kama vile alicopy maneno aliyotumia lile tajiri jinga Trump jana kutangaza nia ..
 
Kumbe Lowasa mjinga kiasi hiki sasa ngoja.....

Ni mjinga sana na kauli kama hii inapaswa kuwa sifa tosha ya kukatilia jina lake mbali hata lisifike kwa ishirini bora wa CCM. Yeye anacheza na umaskini ambao yeye amekuwa sehemu ya chanzo chake. Toka akiwa kijana sijui katibu wa CCM hadi kuwa Waziri Mkuu na hadi leo kuendelea kuwa mbunge na waziri mkuu mstaafu analipwa (na wakati huo huo kufisidi) kutoka katika kodi ya hao hao maskini.

Mafao ya uwaziri mkuu hajawahi kuyakataa japo alijiuzulu kwa kashfa ya ufisadi. Mafao hayo yanatokana na kodi zetu maskini. Leo hii anakuja kututambia kuwa hicho kidogo alichonacho amejaliwa na Mungu. Amejaliwa na Mungu au ni ujanja wa kutuibia na kutufisdi maskini! huyu jamaa mshenzi sana. Lowassa anafikiri akili za Watz bado ni zile za 2005 ambazo alitungia wimbo wa 'maisha bora kwa kila mtanzania' na watu wakaamini. Sasa anageuza title kidogo na kuiita 'ninachukia umaskini'. Akaondoe umaskini kwanza huko Monduli.
 
Lowasa weka wazi utawafanya nini wezi wa richmond??? Au utawasamehe na kujisamehe??
 
Kw hyo ww unaupenda umaskini mkuu,ama unataka uonekane tu na ww ulicomment hapa

Hakuna anae upenda umasikini wala hakuna anae uchukia utajiri tatizo ni kauli ya Lowassa ya (masikini hafai kwenda Ikulu) wakati Ikulu ni ya Watanzania wote masikini na matajiri, anapo sema kuwa masikini hafai kwenda Ikulu kwani ameambiwa kuwa Ikulu ni mahali pakwenda kugawa fedha?kiasi cha kuona kuwa anaefaa kwenda Ikulu lazima awe tajiri kwa kuwa ana fedha za kugawa.
 
Hii ni zaidi ya kufuru!!

Kwa kauli hii jina lake linastahili kukatwa katika hatua za awali kabisa.

Yaani hafai kabisa.


You're just a salary slip and not a PAYROLL. Hayo maoni yako hayana logic yoyote na impact yoyote kwa mtu ambae anachambua mambo.

Who told you kwamba a president has to be poor in order for him to lead well?
 
Mnaomshauri, mwambieni kauli za kichovu kama hizi zitamwumiza. Nani alisema mwenye utajiri ndo haibi!!! Wakati wanasuka dili la richmond hakuwa tajiri?

Kuridhika ni roho ya mtu asikudanganye, eti mtu anaridhika kwa sababu ana vingi. Wenye vingi ndo wanatamani kuzidishiwa kila siku. Utajiri upo rohoni na kwa ushahidi wa wakati sifa hiyo hana. Ni mtu aliyejaa tamaa, ambaye yuko tayari kuuza mbuzi mmoja wa maskini kumpa mgeni wake wakati yeye ana ng'ombe 1,000.

Sifa ya tamaa anayo na inaonekana hata kwa nguvu anayotumia kukipata cheo hiki. Walioridhika hawana haja ya kutumia maguvu yoote anayotumia.

Laana yake kubwa ni tamaaa na tamaa haimalizwi kwa kuwa na vingi.
 
Pasco huyu ndio mtu ulikuwa ukimpigia chapuo!

Who told you that one has to be poor in order for him to meet the threshold of credibility and be a president?

This is quite ridiculous from a learned friend like you.

Vivaa Lowassa.
 
Last edited by a moderator:
You're just a salary slip and not a PAYROLL. Hayo maoni yako hayana logic yoyote na impact yoyote kwa mtu ambae anachambua mambo.

Who told you kwamba a president has to be poor in order for him to lead well?
Hiyo kauli ni ya kibaguzi dhidi ya masikini.Hafai kabisa.
 
You're just a salary slip and not a PAYROLL. Hayo maoni yako hayana logic yoyote na impact yoyote kwa mtu ambae anachambua mambo.

Who told you kwamba a president has to be poor in order for him to lead well?
And who told you a good leader must not be Poor? Kiongozi mzuri ni yule anayeelewa matatizo ya wananchi na ambaye yuko tayari kusaidia kuyatatua tena kama ni tajiri hata kwa fedha zake.
Tanzania ni Masikini, huyu amekuwa Kiongozi wa Masikini toka awamu ya kwanza, na hii ni ya nne na yeye anataka kuongoza ya Tano, Kwanza awaambie watanzania Masikini kuwa amewezaje kujitajirisha tena akiwa mtumishi wa Umma ili wawe na cha kujifunza toka kwake.
Si dhambi Kiongozi kuwa Tajiri na hasa kama ameupata kihalali.
 
Hiyo kauli ni ya kibaguzi dhidi ya masikini.Hafai kabisa.

Kwani si kweli kwamba masikini wapo? Kuna tatizo gani kusema atawasaidia wananchi? Kama hawezi kutusaidia kuondokana na umaskini sasa kwanini tumchague?

Abraham Lincoln aliewaikua Rais wa Marekani alisema hivi' You cannot help the poor by destroying the rich'
'Huwezi saidia maskini kwa kuwakandamiza matajiri'

Amka kaka!!
 
Monduli ni moja ya maeneo yenye kiwango cha juu cha umasikini!!! Hutaki una lako jambo,nimekuwepo hapo muda mwingi wa maisha yangu,uzuri ni kwamba masikini wa monduli hata hawajui tofauti ya umasikini na utajiri,hivyo wanaona yote ni sawa tu,na mzee akienda huko mwisho wa mwaka anawachinjia ngombe kadhaa,anawanunulia na bozer la bia na kuwaambia tanzania nzima inatamani maisha kama ya watu wa monduli,anawaambia kuwa wao ni matajiri wa kutisha,na wamasai wa watu wanachekacheka tu,inatia huzuni mno.
 
Hakuna tajiri mwenye nia ya dhati ya kusaidia masikini...
Wasitufanye watanzania wajinga...
 
Back
Top Bottom