Lowassa, Malecela na Sitta kunyimwa nishani maana yake nini?

Ufisadi wa Lowassa utaendelea kuwa a hear say hadi hapo atakapofikishwa mahakamani na kukutwa na hatia, tofauti na hapo ni blah blah tu.

Hivyo bado uamuzi wa JK wa kutokumweka kwenye listi ya hao recipients ni uamuzi wa kisiasa tu, JK ana uhakika gani kwamba huuyu jamaa hatakuwa Rais?!
 
Apewe nishani ya nini?
What did he do?.... what if it was just a random selection. Kwani kuna vigezo maalum vilivyoorodheshwa?
Anatoa donations za milions as if it's just chocolate. Where the hell does he get that dough?
I don't think it's from his paycheck..... He don't look right.
 
Unapoingia shimoni kumtoa nyoka mbaya
kuna hatari ya kutoka wote mkiwa mmekufa
ndiyo yanayomkuta SAMWEL SITTA
 
Hivi mkuu yaani mimi nisichokuelewa ni wewe kuona EL na Sitta wanahaki ya kupewa nishani,maana umesema wamenyimwa. Labda utueleze kwanza kwanini wapewe.

Pili umesema mawaziri wakuu wote wastaafu walipewa na EL hakustaafu, kwa hiyo hakustahili kupewa tunzo.Halafu kila siku tunapiga kelele kuleta kujuana kwenye kazi sasa kwanini JK ampe nishani kisa marafiki sasa atawapa marafiki wangapi?

Hakuna aliyeona EL anashindana na rais maana JK akuomba kufanya kipindi maalum.

Naomba utuandikie sababu za muhimu wewe kuona Sitta na EL wanafaa kupewa nishani.
 
Kwani Mchango wa Warioba ni Upi!?Afadhali ya Lowassa aliefanikisha ujenzi wa shule za kata kwa kasi!tunashindwa wenyewe kuzisimamia!

Mkweche umesoma huu uzi vizuri mawaziri wakuu wastaafu wote walipewa ila EL hakustaafu.Rejea somo la urai
 
tunachohitaji ni chombo huru cha kupima michango siyo ya wanasiasa wa kitaifa tu bali raia wote jinsi tulivyochangia maendeleo ya taifa hili.............

utata wa maamuzi haya ni pamoja na:-

a) Anne Makinda hawezi kupongezwa kwa Unaibu spika na bosi wake Samweli Sitta akasahaulika.............sote tumeoza angalia mifano hii.....

b)Mwinyi kupitia mama Siti anadaiwa kujilimbikizia mali...............

c) Mkapa ana Kiwira mines na uwanja wake wa mpira alioujenga akishirikiana n na wachina.......ndiyo maana wengine wameubatiza jina lake ili tusisahau ufisadi huu wa kutisha.....

d)Warioba alikata kidari chake kwenye EPA................na jopo lilimtia hatiani kwa matumizi mabaya ya uwaziri mkuu kwenye uchaguzi wa ubunge jimbo la Bunda mwaka 1990...........

e) Msuya naye matumizi mabaya ya ofisi ya umma pale alipohamishia utajiri wa nchi kule jimboni kwake Mwanga kwa manufaa yake binafsi ya kisiasa......

f)
Spika mwingine ambaye hakutajwa kwenye orodha hiyo ni Yule aliyekuwa wa kwanza baada ya Tanzania kupata uhuru, Chifu Adam Sapi Mkwawa (1964-1973 na 1975-94) na Erasto Mang'enya (1973-75).

huu ni ushahidi ya kuwa vigezo vina walakini..........lakini usishangae kesho wakaja kusema walisahau baadhi ya majina.......

g) Malecela hana kashfa ya ufisadi........na yale matatizo ya Muungano na G55 ni ya kiitikadi na kiurasimu ambayo kuyatumia kumtosa inaonyesha JK katumia nafasi yake kumkomoa.....Malecela siku za karibuni amekuwa akihoji utendaji wa JK............hili labda ndiyo sababu ya kumtosa.......................na kumdhalilisha mzee wa watu........................lakini wanafiki hawa siku atakayokufa watamsifia sana.........................na hawatakumbuka unyama huu waliomfanyia.......

h) Dr. Salim anastahili na hana doa.....lakni kwenye sekta nyingine hivi hakuna wenye michango ya kuwazidi hawa wanasiasa............ambao wenyewe ndiyo wanajipangia tu cha kugawana katika ubinafsi wao?
 
JK ni mnafiki sana............................alipokuwa anazindua jengo la Makumbusho ya taifa lililojengwa na wachina............juzijuzi Dar.......................alikosoa kukosekana kumbukumbu ya Filbert Bayi kwenye jengo tajwa.................................lakini naye kamtosa Bayi katika nishani za taifa...................................Filbert bayi ni mtanzania wa kwanza kuvunja rekodi ya dunia kwenye mbio za aina zote.....................hivi kweli hana nishani yoyote ya kitaifa anayostahili............................................???????????????????

nionavyo alipaswa kupewa nishani ya juu kabisa ya J.k Nyerere................
 
RAIS Jakaya Kikwete amewatunuku nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili wanasiasa mbalimbali waliowahi kushika nyadhifa za Uwaziri Mkuu na Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania, huku akiwatosa Edward Lowassa, John Malecela na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambao nao, waliwahi kutumikia nafasi hizo.

Vilevile, amemtunuku nishani hiyo spika wa zamani wa bunge, Pius Msekwa na wa sasa, Anne Makinda na kumtosa Samuel Sitta ambaye aliongoza Bunge la Tisa, kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, Oktoba mwaka jana.

Katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam juzi, kama sehemu ya maadhimisho ya kilele cha kumbukumbu ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, Rais Kikwete alitunuku nishani za aina tatu kwa Watanzania 57 waliotoa michango mbalimbali ya kutukuka kwa maendeleo ya nchi katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wake.

Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na Mawaziri Wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Katika kundi hilo, Rais Kikwete aliwatunuku watu 10 na kuwaacha Malecela, Lowassa na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kujiuzulu mwaka 1984, kufuatia kile kilichoelezwa kuwa, machafuko ya hali ya hewa kisiasa Zanzibar.

Waliotunikiwa nishani hizo ni Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Mzee Abeid Aman Karume, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Hayati Edward Moringe Sokoine, Hayati Idrisa Abdul Wakili na Hayati Dk Omary Ali Juma.

Wengine ni Rais wa sasa wa Zanzibar ambaye aliwahi pia kuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana , Dk Ali Mohamed Shein, na mawaziri wakuu wastaafu, Cleopa Msuya, Joseph Warioba, Dk Salim Ahmed Salim na Fredereck Sumaye.

Malecela akosa

Malecela alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1990 hadi 1994, wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Mbali na nyadhifa hizo za juu serikalini, mwanasiasa huyu pia aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM mwaka 1995 hadi 2007, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (1964-1966), Waziri wa Mambo ya Nje (1972-1973), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki (1975-1976), Mkuu wa Mkoa wa Iringa (1980-1984) , pia amekuwa Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza.

Akiwa katika kilele cha siasa za Tanzania, Malecela alionekana kuwa mwanasiasa mwenye nguvu na kuaminiwa katika Serikali ya Awamu ya Pili, hatua iliyompa nafasi kubwa kwamba huenda angemrithi Rais Mwinyi baada ya kumaliza muda wake kikatiba mwaka 1995.

Hata hivyo, rekodi yake ilichafuliwa wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutunga kitabu alichokiita ‘Uongozi wetu na hatma ya uongozi Tanzania' kilichoainisha udhaifu kadhaa kisiasa wa kiongozi huyo na kumkosoa.

Kitabu hicho kilizima ghafla ndoto ya Malecela kuzidi kukwea milima ya kisiasa na kuwaacha njiapanda wachunguzi wa mambo ya kisiasa walioamini kuwa alikuwa kete muhimu ya Rais Mwinyi kurithi kiti chake, bila kujua mtu wa kurithi nafasi hiyo, kabla ya Rais Mkapa kuibuliwa na kuwa Rais ambaye hakutarajiwa na wengi.


Lowassa atoswa

Kwa upande wake Lowasa alikuwa Waziri Mkuu tangu mwaka 2005 hadi Februari mwaka 2008, katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete .

Lowassa ambaye ni mshirika wa siku nyingi kisiasa wa Rais Kikwete, alijiuzulu kufuatia kashfa ya utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, Lowassa alijaribu kujitetea dhidi ya kashfa hiyo lakini hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema bado hajawa safi mbele ya serikali inayoongozwa na swahiba wake Rais Kikwete.

Lowassa alisema hakuhusika moja kwa moja katika hilo lakini alilazimika kujiuzulu kwa sababu waliozembea na maofisa walioko chini yake.

Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa dhamira yake ilikuwa kuvunja mkataba wa Richmond jambo alilomjulisha pia mkubwa wake(Rais Kikwete) kwa simu akiwa nje ya nchi, lakini Rais alimwambia asubiri kwanza kwani alipata ushauri kutoka kwa makatibu wakuu kuhusu jambo hilo.

Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa gazetini kwa kile walichoeleza nafasi zao nyeti ndani ya serikali, walisema utetezi wa Lowassa bado haujakidhi kumfanya awe safi, ndio maana hakuweza kutunukiwa tuzo hiyo.

Walitoa mfano kwamba kwenye sherehe hizo, Rais Kikwete alimtunuku Nishani ya Juu ya Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ingawa naye aliwahi kujiuzulu kutokana na kashfa ya mauaji ya vikongwe mkoani Shinyanga wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Mwalimu Nyerere. Kwa uwajibikaji huo, Rais Kikwete aliutaja kuwa ni moja ya mambo ambayo yalionyesha kuwa Mwinyi ni mwadilifu.

Wachunguzi wa mambo haya siasa wanadai kitendo cha Mzee Mwinyi kujiuzulu na leo anatunukiwa nishani hiyo ni changamoto muhimu kwa Lowassa kutambua kuwa pamoja na maelezo yake ndani ya NEC, bado usafi kwa kashfa zinazomwandama unatia shaka, kwani yeye alijiuzulu baada ya Bunge kuunda tume iliyochunguza na kutoa mapendelezo ya ‘kupima' lakini Mzee Mwinyi alipima mwenyewe uzito wa tukio na kuamua kuachia ngazi.

Mzee Aboud Jumbe Mwinyi

Mzee Jumbe ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais katika kipindi cha mwaka 1972 hadi 1984 naye ni mmoja wa watu ambao hawakutunukiwa nishani hiyo mbali na kutumikia nafasi hizo kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa utumishi wake.

Aboud Jumbe lijiuzulu mwaka 1984 kutokana na kile kilichoelezwa, machafuko ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar yakihusisha chokochoko zilizokuwa na viashirio vya kuvunja Muungano.

Samuel Sitta
Kwenye sherehe hizo pamoja na kutunuku Msekwa na Makinda wengi wamejiuliza sababu za kutoswa kwa ‘Spika wa Bunge la Kasi na Viwango', Samuel Sitta.

Baadhi ya wanasiasa wazoefu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha maspika hao kutunukiwa nishani na Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuachwa.

Mmoja wa wanasiasa hao kutoka CCM ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema huenda Sitta hakupewa zawadi kutokana na chama hicho tawala kumtuhumu kuwa anaongoza makundi ya upinzani ndani ya chama, jambo ambalo mara kadhaa mwanasiasa huyo amekuwa akilikanusha.

Alisema huenda kutokana na msimamo wake imara usioyumba wa kupambana na vitendo vya ufisadi bila woga ndilo jambo ambalo linalokera wenzake ndani ya chama hicho nakutafsiri kwamba ni kukigawa chama .

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema hajui vigezo vilivyotumika kutoa nishani hizo lakini yeye anaamini Sitta aliweza kulifanya Bunge kuendesha mambo kiuwazi kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kuwa na imani nalo.

"Alisema tangu awali Bunge lake litakuwa la ‘standard and speed' (kasi na viwango ) na liliweza kuonyesha hilo… lakini mimi Napata kigugumizi cha kusema sababu sijui vigezo vilivyotumika," alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na alihudhuria sherehe hizo.

Alisema ingawa yeye alichelewa kufika kwenye sherehe hizo, alishangazwa kusikia kuwa Makinda amepata tuzo hiyo wakati kipindi chake cha uspika hakijamalizika.

Spika mwingine ambaye hakutajwa kwenye orodha hiyo ni Yule aliyekuwa wa kwanza baada ya Tanzania kupata uhuru, Chifu Adam Sapi Mkwawa (1964-1973 na 1975-94) na Erasto Mang'enya (1973-75).

Nishani ya juu kabisa iliyotolewa ni ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo walitunukiwa maraisi wa awamu zote tatu zilizopita, Hayati Mwalimu Nyerere ambayo ilipokelewa na Mama Maria Nyerere kwa niaba yake, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

JK awatosa Sitta, Lowassa, Malecela


My take:

Vigezo na masharti ya Nishati hizi yalikuwa ni nini?? iweje Mawaziri wastaafu na maspika watajwe lakini wengine watoswe??,
 
Naweza kuelewa kuhusu Lowassa, lakini Makinda? Kikwete ametumia criteria gani kumpa nishani huyu mama aliyeharibu kabisa bunge? Rais Kikwete anatuambia nini sisi watanzania kwa kumpa nishani Makinda? Chini yake huyu mama bunge limekuwa kama lina-report kwa serikali na sio tena mhimili wa dola, Makinda kageuza bunge kuwa sehemu ya mipasho.

Kwa sababu zake anazozijua mwenyewe Kikwete anaweza akawa mstari wa mbele kuwatetea wakina Mzee Sykes kuwa walikuwa wapigania uhuru ili 'ku-dilute' nafasi ya Mwl Nyerere lakini hizi nishati zinamrudisha kwenye tope hilo hilo analotaka kuliondoa. Kwa nini Spika wa kwanza Chief Adam Sapi hakupewa nishani? Makinda ana mwaka mmoja tu kwenye hicho kiti, kweli anaweza akawa ametoa mchango kupita ma-spika wengine waliomtangulia?

Binafsi naona hizi ni 'hongo' mchana kweupe, Msekwa ni dalali wa Kikwete hili halina ubishi, na hata Makinda is not her own woman. Doa la miaka 50!
 
@NY, ndo hivyo mzee kakosa nishani ya utumishi uliotukuka. What is your opinion? Where the hell did he go wrong?
 
Mkweche umesoma huu uzi vizuri mawaziri wakuu wastaafu wote walipewa ila EL hakustaafu.Rejea somo la urai

hata malecela hajapewa wangu...sijampata bado muanzisha huu uzi...maana imekuwa kama wote tuko vijiweni sasa
 
JK ni mnafiki sana............................alipokuwa anazindua jengo la Makumbusho ya taifa lililojengwa na wachina............juzijuzi Dar.......................alikosoa kukosekana kumbukumbu ya Filbert Bayi kwenye jengo tajwa.................................lakini naye kamtosa Bayi katika nishani za taifa...................................Filbert bayi ni mtanzania wa kwanza kuvunja rekodi ya dunia kwenye mbio za aina zote.....................hivi kweli hana nishani yoyote ya kitaifa anayostahili............................................???????????????????

nionavyo alipaswa kupewa nishani ya juu kabisa ya J.k Nyerere................


wako wengi sana mkuu...vipi nishani hazifai kwa watu wa chini kabisa, lazima wawe leaders tu??

vipi waliobeba mwenge kwa mara ya kwanza, waliopandisha bendera mlima klimanjaro......list goses on and on

ndio maana the chalenji here is not who recieved and who have not received..the chalenji is what criterion of this nishani??


 
Lowasa angepewa,,mngemhukumu rais kuwa anakumbatia mafisadi.
Lowasa pia angeweza kuitumia nishani hiyo kuthibitisha kuwa yeye sio fisadi, hence njia nyeupe kwa urais.
 
mzee sitta hakutendewa haki hata kama wao hawakubaliani naye sisi watanzania tulio wengi tunaenzi na kutambua mchango wake, usikate tamaa mzee tupo nyuma yako
 
Big Dr. Kikwete,
Kutompa Lowassa nishani binafsi, mimi nimekusoma! Nzuri hiyo.
Ila kumpa nishani Makinda ambaye ni Spika kwa mwaka mmoja, mmmhhh, kama kuna kakitu hapo, mkulu
Na ukiunganisha kuwa umemnyima Spika aliyemaliza kipindi chake Mr. Sitta, hapo kidogo joto lilizidi, ukachemka
 
Taasis ya Ikulu ya wakati huu imekuwa ya watu wanaofanya mambo bila kutafiti kwa mapana! Ina watu wanaokurupuka kufanya mambo bila kufikiria madhala yake wala kuandaa majibu ya maswali yatokanayo. Imejaa watu wenye majibu mepesi, yote kwa sababu ya kukurupuka na kufanya mambo pasipo kujipa muda wa utafiti kuchuja "pros and cons".

Kwa jinsi ambavyo wametoa hizi nishan na kuzua maswali mengi, nina hakika kesho watakurupuka kujibu na miongoni mwa majibu yatakuwa kama ifatavyo:
  • kilichofanyika Ijumaa "was ceremonial" na kilitokana na muda kutoruhusu kutoa nishan kwa wote,
  • hiyo ilikuwa awamu ya kwanza, awamu ya pili ya ugawaji nishan itafuata baadae,
  • n.k.
Haya ndio madhala tunayoyapata kuwa na vichwa vilivyoingia Ikulu kishkaji! Hakuna anayejali heshima ya taasis; kila mtu anakimbizana na posho na kutafuta "cheap popularity", na linapokuja swala la msingi linakuta kila mtu amekaa mkao wa hasara wa kutotaka kuumiza kichwa. Hizi nishani zina muelekeo ambao hauingii akilini:
  • kumpa Mh. Makinda nishani ukamwacha Mh. Sitta na Pinda (maana wote wamekuwa viongozi wa juu wa mihimili ya nchi na wote bado wako katika kulitumikia Taifa).
  • Issue ya Melecela 'stinks' maana unatofautishaje utumishi wa Malecela na Warioba?! CCM na Serikali yake wamelitumia "tingatinga" zaidi ya hata walivyomtumia Warioba, na tingatinga wala halinuki kashfa ya wizi kama Warioba!
Ukweli ni kwamba kwa taasis hii ya Ikulu ya sasa tumeliwa!
 
hata pale uwanjani JK alimsalimia EL kimagumashi sana(kama macho yangu yako sahihi)
Mie niliona Lowassa akichekacheka huku kanyosha mkono kumpelekea jk Na jk alinuna ghafla na kuukwepesha mkono wake kana kwamba anachelewa kukaa ... Bifu ndio limeshaanza baada ya E.L kusema ikifika time ataweka wazi juu ya Richmond ni ya nani na ukweli wote. ndio maana jk anamuavoid sana mshikaji wake huku EL akumuenjoy kuliko maelezo jk
 
Back
Top Bottom