Lowassa, Malecela na Sitta kunyimwa nishani maana yake nini?

Big up JK
....hawa waache wamalize kwanza ugomvi wao ndipo wachukue NISHANI mwaka 2014 kwenye miaka 50 ya TANZANIA
 
Watanganyika wengne very lazy kuwaza, lowasa anapewa nishani ya nhni wakati hakustaafu? Hata km alifikia daraja ila hakidhi viwango vya kupewa nishani so angepewa ya nini? I thnk people mjitaid kuwaza mpaka nje ya mstari bhana sio mnashadadia mambo ya ajaaabu! Kabaaang!
 
Sitta na Lowassa sasa wamewekwa kundi moja na vigogo wa CCM na huenda wote wakatoswa pamoja.

Ni bora. Kwa sababu kuwaacha hawa ama kumruhusu mmoja asimame kwenye nchi hii ni hatari. Wote wanapenda sana ubinafsi na wanaendekeza makundi. Hizo si siasa nzuri kwa ustawi wa taifa letu.
 
MIMI Rais kanishangaza na kuniacha na maswali magumu
1.kutoa hotuba ambayo kaoengelea lami tu kama ndo issue kubwa lenye hadhi ya kuongelea katika miaka hamsini???
2.ktunuku wastaafu nishani ya heshima ya mwal. Nyerere ktika viwanja vya ikulu mbele ya wateule wachache? badala ya mbele ya watanzania waliokwenda uwanjani na kupigwa na jua huku wakiambulia gwaride la kila mwaka
na hotuba ya dk 15 yenye kusema issue za lami

hili linatueleza nini?????????????????????????????????????

Ikulu nako kuna heshima kubwa saana. Nadhani hapa tuwaulize waandishi wa habari, kwanini hawakutangaza tukio hili? Tukisema wamenunuliwa tutakuwa tunawaonea?
 
Nimefuatilia suala la mzee Sitta kutokupewa nishani. Nimeambiwa kuwa Sitta na Nahodha bado hawajastaafu. Baada ya kutoka ktk nafasi ya spika wa bunge, Sitta bado analitumikia Taifa ktk nafasi aliyonayo sasa ya Waziri wa Afrika Mashariki. Nahodha baada ya kutoka ktk nafasi ya Waziri Kiongozi, sasa ni Waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Sijajua kwanini Lowasa hakupewa, na bado hakuna mtu aliyekuwa tayari kutoa sababu za kutopewa nishani
 
Ni bora. Kwa sababu kuwaacha hawa ama kumruhusu mmoja asimame kwenye nchi hii ni hatari. Wote wanapenda sana ubinafsi na wanaendekeza makundi. Hizo si siasa nzuri kwa ustawi wa taifa

Hivi Sitta ana kosa gani la kufananishwa na Lowasa?
 
Kumchanganya Sitta na Lowassa kundi moja ni kichekesho, hata kama ana makosa. Huo ni utoto wa kutupa.
 
Hoja hii naona imegusa mfupa kama ile aliyoitoa mzee Kasori. Wachangiaji wenye mtizamo fulani wameshindwa kuchangia kama tulivyozoea kuwaona, na badala yake WAMEINGIA mitini.
 
Si kuingia mitini tu wameanza na kuchanganya madawa, lakini kituko ni kuchanganya fisadi na mpiga filimbi. Lowassa na Sitta hawawezi kuwekwa kundi moja hata kama Sitta naye ana mapungufu yake.
 
Nimefuatilia suala la mzee Sitta kutokupewa nishani. Nimeambiwa kuwa Sitta na Nahodha bado hawajastaafu. Baada ya kutoka ktk nafasi ya spika wa bunge, Sitta bado analitumikia Taifa ktk nafasi aliyonayo sasa ya Waziri wa Afrika Mashariki. Nahodha baada ya kutoka ktk nafasi ya Waziri Kiongozi, sasa ni Waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Sijajua kwanini Lowasa hakupewa, na bado hakuna mtu aliyekuwa tayari kutoa sababu za kutopewa nishani

Kwani Makinda amestafu?
 
Labda tungeanza kwanza kwanini Lowassa apewe nishani ametoa mchango gani ? maana kuwa rafiki na rais sio sababu ya yeye kupewa nishani.

Pia sitta kwa lipi alilofanyia taifa hili?
Kwani Mchango wa Warioba ni Upi!?Afadhali ya Lowassa aliefanikisha ujenzi wa shule za kata kwa kasi!tunashindwa wenyewe kuzisimamia!
 
..Komandoo Salmin Amour Jumaa amepewa nishani yoyote?

..nimeona ametajwa Shekhe Idris Abdul Wakili[r.i.p] ambaye alikuwa Raisi wa Zanzibar.
 
Kwani Mchango wa Warioba ni Upi!?Afadhali ya Lowassa aliefanikisha ujenzi wa shule za kata kwa kasi!tunashindwa wenyewe kuzisimamia!

Tofautisha Waziri Mkuu mstaafu na Waziri Mkuu aliyefukuzwa. Warioba hakustaafu kwa kashfa, na hata baada ya kuondoka madarakani ameendelea kutumiwa vizuri sana Kimataifa. Hebu tueleze huyu fisadi Lowasa anatumiwa na nani baada ya kufukuzwa?
 
hata pale uwanjani JK alimsalimia EL kimagumashi sana(kama macho yangu yako sahihi)

Wewe uko sahihi kabisa. Usiyatilie mashaka macho yako hata kidogo. Washauri wa Lowasa sijui wanamshauri nini huyu mzee maana naona wanazidi kumtumbukiza ktk shimo tu.
 
Tanzani nakupenda Tanzania! Chekundu, cheusi, chupe! Cheusi kiko wapi? Hizi ni karata tatu! Msichezee umma
 
Kwa namna yeyote itakavyochukuliwa hapa naona ukweli ni kuwa kile kikatuni cha mathudi kilichotoka baada ya Edward Lowasa kujiuzuru kinabeba maana halisia sasa, yaani Lowasa hana mvuto tena.
 
Hakuna mtu aliyenyimwa NISHANI YA MWL.NYERERE, bali wale wote wasiopata hawakuwa na vigezo vya kupata, tusipende kukuza mijadala bila sababu za msingi
 
Back
Top Bottom