Lowassa Kwenda Ikulu Kumpongeza Magufuli, Kilichofanya Kuwa Big News, ni Lowassa na Sio Rais Magufuli!, Why?-Jicho Letu

Kama lema,lissu na mbowe walipata kifafa cha muda kwanini isiwe habari kubwa hata kama lowassa asinge toa maoni kitendo cha kufika ikulu tu ingekua habari kubwa kuliko magufuli kupiga dana dana mpira!
Kwa kuwa hawezi lazima ingekuwa story ila jk inafahamika kashirik michezo sio story.
 
Kwenye Uwanja wa Mapambano anaetangaza kuweka Silaha Chini na kutangaza kumuunga Mkono Adui yake ndio huwa 'talk of the town' sio anaeungwa Mkono !

Kwenda kumuunga Mkono Rais uliewaaminisha malofa kuwa kakuibia kura sio jambo Dogo
Hili nalo neno.
 
Ni bahati mbaya sana kuwa Ikulu ilifanikiwa kutufanya tusikie kile walichotaka tu tukisikie. Hii kwa maoni yangu ndio imeleta taharuki yote hii. It was not fair kwa Lowassa. Mbaya zaidi na yeye mwenyewe amekuwa kimya. Lakini ajabu pia hata waandishi hawakufanya ya kutosha kupata neno kutoka kwa Lowassa kuhusu suala hilo. Hii imefanya clip iliyotlrekodiwa na kuwa edited na Ikulu kuwa ndio "ukweli" wote kwa sasa.

Wangetaka iwe fair baada ya mazungumzo kungekuwa na press conference na wanahabari kuwauliza maswali wote wawili. Najua hili CCM wasingetaka litokee!
 
Mkuu pascal mi kuna swali nimelipenda toka dotto bulendu kwamba vyombo vya habar vinaripot sawasawa taarifa za hawa wabunge wanaohamama?

Mwandishi mmoja kajibu bado kuna vitu vya kuhoji nyie kama waandishi ili mwananchi wa kawaida ajue kwa nini kajiuzulu chama A ktk huo wadhifa wake na kupewa tena kugombea kupitia chama B nini kipo nyuma ya pazia?
 
Kama Waziri mkuu aliyejiuzuru na mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita ndugu Lowasa anaweza kutumia 'Mara Nyingi' (labda zaidi ya mwaka) kuomba kuonana na Magufuli ili kujadiliana kuhusu mustakabali wa nchi na mambo yanavyo kwenda lakini bila mafanikio mpaka pale alipoamua yeye tena kwa kuwatumia akina Gambo watangaze kwanza kuwa Lowasa anawabembeleza akiomba kukutana na rais. Lakini ikachukua siku 11 hadi 12 tu kwa wafungwa walioachiwa huru kwa kosa la kulawiti watoto, Babu Seya and The Gang kuomba kwa ombi la mara moja kukutana na rais na kufanikiwa kuonana naye.
Mpaka hapo kama una akili timamu utagundua hiyo nchi ni yenye viongozi wa aina gani na inastahili nafasi gani in return.
Uongozi wa ajabu kabisa kuwahi kutokea toka tumepata uhuru.
 
Hoja kama hii mimi huijibu kwa mkato kama ifutavyo;
"Ukimuona simba mjini ujue kajileta, na hata kama kaletwa basi ni kwa vibali maalum; hapo utamshangaa. Ila ukimuona simba mbugani, hutoshangaa, maana ni mahala pake"

Mh Lowassa kwenda ikulu lazima iwe habari kama vile vile inavyoweza kuwa habari ukimkuta Mh Magufuli Kariakoo akiwa bila msafala bali gari moja kama alivyoenda ikulu Mh Lowassa, hiyo itakuwa habari. Vivyo hivyo kwa kinyume chake.
 
Back
Top Bottom