Lowassa Kwenda Ikulu Kumpongeza Magufuli, Kilichofanya Kuwa Big News, ni Lowassa na Sio Rais Magufuli!, Why?-Jicho Letu

Lowasa hawezi siasa za ushindani. Dunia nzima ni very unusual upinzani kusifia chama tawala kwa sababu ya kuepuka kumpa advantage mshindani wako wa kisiasa..

Rejea kauli zake,
"zamu yetu kkkt kuwa na Rais"
Kwa kauli hiyo Nampe aliitumia kumchapa

"mtaangalia vizuri ilani kwenye Internet kwa sababu ninyi wote hapa ni wasomi"

"nikishindwa urais nitarudi kijijini kijijini kuchunga ng'ombe"

"Today the president has made my day, tumuunge mkono anafanya kazi nzuri"

Kauli hizo ni mtaji wa kisiasa kwa chama tawala. Lowasa hana elements za upinzani. Na hajawahi kuwa mpinzani moyoni mwake

BTW unategemea nini mtu aliyekaa kwenye system ya chama tawala for the most of his political career leo akawa kinyume 100 percent? Siri zote anazijua. Anakula malupulupu ya serikali. Mali zake zipo chini ya huruma ya serikali. Hawezi kuwa mshindani huyu

Lowasa alitumika na Chadema 2015 kwa sababu alikuwa mtaji mkubwa wa kisiasa kwa mlengo wa upinzani. Mission imekwisha.

Hillary Clinton akimsifu trump itakuwa ni big story dunia nzima. Lakini hata kama Trump atafanya kizuri Clinton hatomsifu hadharani daima kwa sababu anajua nini maana ya siasa za ushindani.
 
Mkuu Kiatu Kipya, hebu tueelimishane, what kuwa na mvuto, got to do with foul play?.

Lowassa alipokuwa CCM alikuwa na mvuto wa ajabu hadi watu kumuimbia wimbo wa "Tunaimani na Lowassa...", hivyo alipojoin Chadema, tulitumai angehama na mvuto wake na mtaji wake kuja nao huko, lakini sasa baada ya zile kura millioni 6 za 2015, what is his position now?.

Nguvu ya mamba ni mu mayi, na nguvu ya Lowassa ni CCM, akirejea, itarejea!.

Kwa lengo la kuelimishana kuhusu mvuto, karibu pande hizi

Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda!

Matumizi ya 'human shield' ya makundi ya watu as 'pressure group' kwa vikao vya CCM

Paskali
Uzuri mkuu Paschal huwa unakumbukumbu nzuri sana kipindi flani ulishaweka mada ikisema bila tume huru wapinzani( ingawa silipendi ili jina) hawawezi penye kwenye uchaguzi mkuu hasa kwa urais kutokana na vinasaba vya chama dola na tume( zikiwemo kanuni zinamteua chairman wa tume pamoja na mkurugenzi) na hiki ndo kilitokea by 2015 kwa ufirauni wa watu wachache ingawa kila mgombea alikuwa na mapungufu yake,fair play nayozungumzia ni sheria iliyopitishwa na mdomo wa bwana mkubwa ya marufuku ya mikutano ya kisiasa unadhani nyota ya EL ingefifia kwa speed hii? Tuwe wakweli kuna matatizo katika kuandaa viongozi wetu huyu wetu bado tutaja shuhudia makubwa zaidi ya haya
 
Wanabodi,

Kama kawaida ya kila Jumamosi asubuhi, kila nipatapo muda, huangazia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa mubashara na Star TV, chini ya Uongozi wa nguli Dotto Emmanuel Bulendu.

Habari kubwa wiki hii, ni mkutano wa Edward Lowassa na rais John Pombe Magufuli. Waalikwa ni waandishi wa habari, Denis Ngonyani na Yohani hoja hapa ni kwa nini mkutano ilikuwa a big news!, aliyesababisha iwe ni Big News sio Rais Magufuli Bali ni Edward Lowassa, kwa nini?.

Mjadala unahusi ni nini haswa kilichofanya ziara ya Lowassa kwenda ikulu kumpongeza rais Magufuli kuwa big news, nini kilichosababisha habari hii kuwa big news na kutawala kurasa za mbele za magazeti yote with big headlines, jee ni kwa sababu Rais Magufuli ni Big Name?, jibu ni hapani, kilichofanya habari hii kuwa kubwa na kuattract big headlines ni Edward Lowassa na sio rais Magufuli, kwa kitendo cha mpinzani Mkuu wa rais Magufuli aliyepinga matokeo ya urais na kudai hautambui ushindi wa Magufuli, kwa hoja mshindi halali ni yeye Lowassa, lakini mwisho wa siku, mtu huyu huyu aliyelalamika bila kuyafuta malalamiko yake, akaibukia Ikulu kumpongeza rais Magufuli, this is big news!.

Kilichoipa nguvu Zaidi ziara hiyo ni kile kilichozungumzwa na wote wawili, Lowassa akimpongeza Magufuli, badala ya kulalamikia uminywaji wa demokrasia na ukanyagwaji wa katiba, yeye Lowassa kaona mazuri tuu ya Magufuli na kumpongeza, this was a big news!.

Kitendo cha rais Magufuli kumsifia Edward Lowassa kuwa ni kiongozi safi, wakati alikuwa akituhumiwa kwa ufisadi wa Richmond, hivyo Magufuli kumsafisha Lowassa, this pia is Big News.

Hoja za msingi sasa tujadili jee kitendo kile. was it a was it a good move, was it a right move?, maneno yaliyotamkwa na pande zote ni kauli ya kujenga au kubomoa?.

Endelea kufuatilia

Paskali
Lowassa alisifiwa na JPM kuwa ni kiongozi mzuri.
 
Wanabodi,

Habari kubwa wiki hii, ni mkutano wa Edward Lowassa na rais John Pombe Magufuli. hoja hapa ni kwa nini mkutano ilikuwa a big news!, aliyesababisha iwe ni Big News sio Rais Magufuli Bali ni Edward Lowassa, kwa nini?.

Kitendo cha rais Magufuli kumsifia Edward Lowassa kuwa ni kiongozi safi, wakati alikuwa akituhumiwa kwa ufisadi wa Richmond, hivyo Magufuli kumsafisha Lowassa, this pia is Big News.

Paskali
Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alitoa,
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Back
Top Bottom