Lowassa Kwenda Ikulu Kumpongeza Magufuli, Kilichofanya Kuwa Big News, ni Lowassa na Sio Rais Magufuli!, Why?-Jicho Letu

Mkuu pascal mi kuna swali nimelipenda toka dotto bulendu kwamba vyombo vya habar vinaripot sawasawa taarifa za hawa wabunge wanaohamama?

Mwandishi mmoja kajibu bado kuna vitu vya kuhoji nyie kama waandishi ili mwananchi wa kawaida ajue kwa nini kajiuzulu chama A ktk huo wadhifa wake na kupewa tena kugombea kupitia chama B nini kipo nyuma ya pazia?
Mkuu Radika, hili ni swali la msingi sana linalojielekeza moja kwa moja katika udhaifu wa media zetu kufanya kitu kinachoitwa a follow-up story, yaani media zetu zikiisha ripoti tukio, huishia hapo hapo, hakuna kufuatilia story muendelezo, mfano hata hili la Lowassa, hakuna media inamfuata Lowassa aelezee mchakato mzima ulivyokuwa hadi kutinga Ikulu, nini kilimpeleka, kwa nini hakuwashirikisha viongozi wenzake, na mwisho walizungumza nini?, what was the most important items kwenye mazungumzo yao, ni kupongeza tuu, au pia walizungumzia mustakabali wa taifa hili na uminyaji wa demokrasia unaofanywa na rais Magufuli na vyombo vya dola kuwanyanyasa wapinzani.

Media yetu Tanzania, we have a long way to go, kuisaidia the society.

Paskali
 
kwa sababu magu sii lolote sii chochote..watu wooote wameona Hana maana na Hana jipya
Mkuu Silent Kills, sii kweli kuwa Magu sii lolote, sii chochote, kwa sababu Magu ndie rais wa nchi yetu, ndie rais wako, ndie rais wa Lowassa, ndie rais wa Mbowe, ndiye rais wa Watanzania wote, waliomchagua, wasiomchagua, hata wasiopiga kura, na kwa mujibu wa katiba yetu, rais ndio kila kitu, hadi wengine wetu humu kumfananisha na Alfa na Omega, Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba!
hivyo asiwe na maana au asiwe na jipya, bado yeye ndio kila kitu!.

Ila kwenye subject matter ya kutembelewa na Lowassa, aliye make big news ni Lowassa kumtembelea rais Ikulu na kumpongeza, kila siku rais Magufuli anatembelewa Ikulu na anapongezwa, ila hii ya kutembelewa na Lowassa ni kubwa kuliko, ndio maana ikaleta big impact.

Paskali
 
Waliofanya big news ni Chadema sio CCM kwa sababu walihisi kuwa kampelekea mafaili ya siri na flash yenye siri zote za Chadema. Aliyepewa haikuwa issue issue ilikuwa aliyepeleka
Mkuu Yehodaya, naunga mkono hoja, Chadema ni wakurupukaji sana na waropokaji, hawana nidhamu, wala hawa breki, kila mtu ni msemaji wa Chadema!, baada ya tukio lile walipaswa kutulia na kujibu no comment, hadi wapate the official version of what transpired between them!.

Sasa sura zitawashuka!.

P.
 
Wanabodi,

Kama kawaida ya kila Jumamosi asubuhi, kila nipatapo muda, huangazia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa mubashara na Star TV, chini ya Uongozi wa nguli Dotto Emmanuel Bulendu.

Habari kubwa wiki hii, ni mkutano wa Edward Lowassa na rais John Pombe Magufuli. Waalikwa ni waandishi wa habari, Denis Ngonyani na Yohani hoja hapa ni kwa nini mkutano ilikuwa a big news!, aliyesababisha iwe ni Big News sio Rais Magufuli Bali ni Edward Lowassa, kwa nini?.

Mjadala unahusi ni nini haswa kilichofanya ziara ya Lowassa kwenda ikulu kumpongeza rais Magufuli kuwa big news, nini kilichosababisha habari hii kuwa big news na kutawala kurasa za mbele za magazeti yote with big headlines, jee ni kwa sababu Rais Magufuli ni Big Name?, jibu ni hapani, kilichofanya habari hii kuwa kubwa na kuattract big headlines ni Edward Lowassa na sio rais Magufuli, kwa kitendo cha mpinzani Mkuu wa rais Magufuli aliyepinga matokeo ya urais na kudai hautambui ushindi wa Magufuli, kwa hoja mshindi halali ni yeye Lowassa, lakini mwisho wa siku, mtu huyu huyu aliyelalamika bila kuyafuta malalamiko yake, akaibukia Ikulu kumpongeza rais Magufuli, this is big news!.

Kilichoipa nguvu Zaidi ziara hiyo ni kile kilichozungumzwa na wote wawili, Lowassa akimpongeza Magufuli, badala ya kulalamikia uminywaji wa demokrasia na ukanyagwaji wa katiba, yeye Lowassa kaona mazuri tuu ya Magufuli na kumpongeza, this was a big news!.

Kitendo cha rais Magufuli kumsifia Edward Lowassa kuwa ni kiongozi safi, wakati alikuwa akituhumiwa kwa ufisadi wa Richmond, hivyo Magufuli kumsafisha Lowassa, this pia is Big News.

Hoja za msingi sasa tujadili jee kitendo kile. was it a was it a good move, was it a right move?, maneno yaliyotamkwa na pande zote ni kauli ya kujenga au kubomoa?.

Endelea kufuatilia

Paskali
Paskali wakati mwingine unaamua kupotosha kwa makusudi kabisa. Niwekee clip inayoonysha Magufuli akisema Lowassa ni Kiongozi SAFI. Myalla wewe ni Mwandishi mkongwe na nguli kabisa kusema kitu amabacho hakipo ili kuridhisha mtima wako ni aibu kwa Kwa tasnia nzima ya habar na wewe pia.
Alichokisema magufuli ni Siasa za kistarabu zinazofanya na Lowassa tangu ahamie CDM. Na akasisitiza kabisa kuwa Lowassa siyo muumini wa siasa maji taka za matuzi na uzushi kama huu unaotaka kuuleta hapa [HASHTAG]#Paskali[/HASHTAG] Mayalla.
Mimi niwaase tu waandishi wa habar itendeeni haki taaluma yenu. Mahaba myaweke pembeni mnapokuwa mnatekeleza wajibu wenu wa kitaaluma.
 
Lowasa ndiyo mwanasiasa bora mwenye mvuto aliyebaki kwa sasa.
Hoja kuwa Lowassa ndio mwanasiasa bora mwenye mvuto, inaitwa mtazamo, yaani point of view kwa unavyoona wewe, ili kuitia nguvu hoja yako, ungeelezea huo ubora wa Lowassa kwa sasa na una faida gani kwa Chadema, kisha ukaelezea kuhusu huo mvuto, anamvutia nani na mvuto huo umeleta faida gani kwa Chadema. Kwa wenye mtazamo mwingine, mwanasiasa bora kabisa kwa sasa na mwenye mvotu nchini Tanzania, ni John Pombe Magufuli, ubora wake ni kuvunja vunja upinzani Tanzania, na mvuto wake ni viongozi hadi wa juu wa vyama vya upinzani kuvutika na kumfuata kwa kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM.

Paskali
 
Kwenye Uwanja wa Mapambano anaetangaza kuweka Silaha Chini na kutangaza kumuunga Mkono Adui yake ndio huwa 'talk of the town' sio anaeungwa Mkono !

Kwenda kumuunga Mkono Rais uliewaaminisha malofa kuwa kakuibia kura sio jambo Dogo
Mkuu Pohamba, hapa nakuunga mkono, hata mimi katika uzi wangu huu, nilimshauri Lowassa kwanza abatilishe kauli hizi alizowahi kuzitoa, ndipo sisi wazito wa kuelewa, tumwelewe!.
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.
Paskali
 
Habari ni nini kilichompeleka
Kifupi ni kuomba tu mambo yao yawe mepesi kwani vyuma vimekaza na kujam hakuna mzunguko mwisho vingevunjika kama wangezidi kulazimisha kuvizungusha.
 
Kilicholeta issue ni namna Lowassa alivomkubali mazima JPM.

Ikumbukwe kauli ya kutomtambua JPM na kususia susia baadhi ya mikutano ya JPM huko awali.

CDM haijawahi kuitisha press na kusema tunamtambua JPM kama Rais wetu.

EL Fanya Kazi yako Walikuchafua Wenyewe, Wakakuchukua na madodoki wamekusafisha na sasa amua mwenyewe future yako

Hahahahahaha
Nimeipenda hii, siasa nayo ni sayansi ya siasa, unafanya calculations za faida na hasara, unafikia maamuzi utakayofaidika nayo, hata kama yatawakera wengine, ama hutaeleweka au hata kukiangamiza chama chako. Tanzania bado tunafanya primitive politics, ni siasa za struggle for existence, survival is only for the fittest, kama ili ku survive kwenye game of politics ni kujiunga CCM, then ma survival wote watajiunga CCM, ambao hawatajiunga, 2020, they will simply perish!.

Kwenye modern politics, by now voice note za Lowassa aliwahi kusema kumhusu Magufuli, na sasa anasema nini, kisha strong media zinamkabili Lowassa na kumuuliza which is which?, au akanushe kauli za mwanzo, au hizi pongezi kwa Magufuli, ni just paying lip services kwa maandalizi ya next move, kurejea CCM!.
Angalia hapa Lowassa alisema nini
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.
Paskali
 
Wanabodi,

Kama kawaida ya kila Jumamosi asubuhi, kila nipatapo muda, huangazia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa mubashara na Star TV, chini ya Uongozi wa nguli Dotto Emmanuel Bulendu.

Habari kubwa wiki hii, ni mkutano wa Edward Lowassa na rais John Pombe Magufuli. Waalikwa ni waandishi wa habari, Denis Ngonyani na Yohani hoja hapa ni kwa nini mkutano ilikuwa a big news!, aliyesababisha iwe ni Big News sio Rais Magufuli Bali ni Edward Lowassa, kwa nini?.

Mjadala unahusi ni nini haswa kilichofanya ziara ya Lowassa kwenda ikulu kumpongeza rais Magufuli kuwa big news, nini kilichosababisha habari hii kuwa big news na kutawala kurasa za mbele za magazeti yote with big headlines, jee ni kwa sababu Rais Magufuli ni Big Name?, jibu ni hapani, kilichofanya habari hii kuwa kubwa na kuattract big headlines ni Edward Lowassa na sio rais Magufuli, kwa kitendo cha mpinzani Mkuu wa rais Magufuli aliyepinga matokeo ya urais na kudai hautambui ushindi wa Magufuli, kwa hoja mshindi halali ni yeye Lowassa, lakini mwisho wa siku, mtu huyu huyu aliyelalamika bila kuyafuta malalamiko yake, akaibukia Ikulu kumpongeza rais Magufuli, this is big news!.

Kilichoipa nguvu Zaidi ziara hiyo ni kile kilichozungumzwa na wote wawili, Lowassa akimpongeza Magufuli, badala ya kulalamikia uminywaji wa demokrasia na ukanyagwaji wa katiba, yeye Lowassa kaona mazuri tuu ya Magufuli na kumpongeza, this was a big news!.

Kitendo cha rais Magufuli kumsifia Edward Lowassa kuwa ni kiongozi safi, wakati alikuwa akituhumiwa kwa ufisadi wa Richmond, hivyo Magufuli kumsafisha Lowassa, this pia is Big News.

Hoja za msingi sasa tujadili jee kitendo kile. was it a was it a good move, was it a right move?, maneno yaliyotamkwa na pande zote ni kauli ya kujenga au kubomoa?.

Endelea kufuatilia

Paskali
Wewe ni mwanahabari nguli, kwa nini UNACHANGANYA CHANGANYA lugha ktk kuandika?
 
Mkuu Radika, hili ni swali la msingi sana linalojielekeza moja kwa moja katika udhaifu wa media zetu kufanya kitu kinachoitwa a follow-up story, yaani media zetu zikiisha ripoti tukio, huishia hapo hapo, hakuna kufuatilia story muendelezo, mfano hata hili la Lowassa, hakuna media inamfuata Lowassa aelezee mchakato mzima ulivyokuwa hadi kutinga Ikulu, nini kilimpeleka, kwa nini hakuwashirikisha viongozi wenzake, na mwisho walizungumza nini?, what was the most important items kwenye mazungumzo yao, ni kupongeza tuu, au pia walizungumzia mustakabali wa taifa hili na uminyaji wa demokrasia unaofanywa na rais Magufuli na vyombo vya dola kuwanyanyasa wapinzani.

Media yetu Tanzania, we have a long way to go, kuisaidia the society.

Paskali
Kwani Mbowe mwaka 2015 alivyoenda kumshawishi Lowassa ahamie Chadema aliwashirikisha viongozi wenzake?!!...... Ndio njia hiyo hiyo ya kubadili gia angani imetumiwa na Lowassa na hapa ndipo ukweli wa Dr Slaa unathibitika kwamba hakushirikishwa katika mchakato wa kumleta Lowassa Chadema!
 
Hata mimi niliona na nikaazisha uzi kuwa kumbe Lowassa hakuwa fisadi maana hata mkuu amethibitisha hilo ila waliufuta
Ni kweli Lowassa hajawahi kuwa fisadi ndio maana hajawahi kushitakiwa kwa lolote, ila ukweli unabaki kuwa mafisadi wote wakuu ni CCM, hivyo japo Lowassa hajawahi kuwa fisadi, haisafishi ufisadi wa CCM, kwa jinsi ile ile rais Magufuli anavyopiga vita ufisadi, haiwezi kumsafisha na ufisadi wa uuzaji wa nyumba za serikali, kivuko cha MV Bagamoyo, au hasara ya Samaki wa Magufuli, kinachofanyika ni just superficial lakini deep down, inside, ufisadi uko pale pale kwa sababu usafi unafanyika nje tuu, wakati ufisadi halisi uko ndani yao, inside CCM!,na Watanzania tulivyo watu wa ajabu, tunashangilia hizi superficial, wakati the real things ziko pale pale!, Richmond tumeliwa, nyumba za serikali zimeuzwa, kivuko cha MV Bagamoyo tumepigwa na kiko juu ya mawe, Samaki wa Magufuli, taifa limekula hasara, lakini watu tunashangilia usafi wa watu wale wale, na chama kile kile!.

Paskali
 
Back
Top Bottom