Membe S K
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 1,407
- 1,302
mimi siamin kama amehonga chadema wanasubiri ccm watamfanyaje huyu bwana, je watamtosa au atabeba bendera ya ccm na wakimtosa mbadala ni nani? ili wapange shambulizi
Hilo la Chadema kuhongwa liko wazi mno. Na kwa taarifa Lowassa ameshakubaliwa kugombea kupitia Chadema endapo jina lake litaondolewa CCM. Karata ya Lowassa sasa ni kutishia kuondoa CCM na kuitaadhalisha CCM kwamba anauwezo wa kukiua chama. Chadema nao wanasindikiza team Lowassa katika wimbo huu wa vitisho. Maana wao pesa wamekula na hapo hapo wanasubiri ccm ifanye kosa kumweka Lowassa ili wachukue nchi au kumfukuza ili ajiunge Chadema na kudhohofisha ccm.
CCM kujiokoa na kifo itachagua kumbwaga Lowassa kwenye urais maana kumpitisha yeye ni kutia sahihi kwamba ufisadi rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ndio sera za ccm. Lile gamba ambalo lilishindikana kuvuliwa sasa akina Kinana na Mangula wanaweza kulivua. Report ya Mwinyi juu ya kuwafukuza wanachama wasio waadilifu, report ambayo Lowassa na Makamba senior waliikalia, sasa nayo inaweza ikaleta matumaini kwa wanachama wa ccm. Akishafukuzwa Muhongo wa Escrow Lowassa wa Richmond na EPA naye atatakiwa apigwe chini urais ili wanaccm warejeshe imani kwenye chama. Naamini ccm haitafanya kosa na wala haipo kwenye wakati mgumu kufanya uamuzi huu sahihi. Mrema hadi sasa anajuta kuhama chama na sasa Lowassa anatayarisha meza ya majuto na sidhani kama atakuwa na ubavu wa kuhama kama anavyojaribu kutishia.
Ifahamike kwamba wanaowapa ukawa ushindi ni CCM na sio wanachama wa ukawa. Hivyo basi CCM ikionyesha dhati ya kukomesha Rushwa, utovu wa maadili, kuwawajibisha wahusika wa ubadhilifu kwa kutowarudisha madarakani, na kukemea matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kupiga vita kujilimbikizia mali kwa viongozi wa umma, ccm itakuwa imejihahakikishia ushindi. Ajabu malalamiko haya yote ya msingi kwa wanaccm sio ajenda za Lowassa na wala hutamsikia akiongelea.