Lowassa kuwa rais sawa, lakini kwanini anahonga?

Lowassa kuwa rais sawa, lakini kwanini anahonga?

wanajanvi nimekuja na hoja hii kwamba lowasa kuwa rais sina shida lakin kwa nin ana tumia hela nyingi kuhonga honga makanisan na misikitin? "nyerere alisema anayetaka urais kwa kuhonga watu huyo mwogopeni kama ukoma" akijenga hoja kwamba ikulu kuna biashara gani? hela anayotumia kuhonga watu amepewa na nani? na atarudishaje akiwa rais wetu? haya ni maswali ya msingi sana tunatakiwa kuweka ushabiki pembeni namtaka yeye mwenye lowasa aje atujibu kwa ufasaha kama anataka kuwa kiongoz wetu kwa sabab ikulu ni mahali pa takatifu haiwez kuwa pango la walanguz lowasa anachofanya ni ulanguz mkubwa ili aingie ikulu. nawasilisha.

Ha! Ha! Ha! Haya YAMEZUNGUMZWA SANA NA WAZALENDO WA NCHI HII , SASA SUBIRI WAZEE WA MISHIKAKI YA BURE !
 
Lowasa anatumia kanuni ya ccm waliojiwekea mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi 2005 kuhusu kuchaguliwa kuwa mgombea urahisi. Kanuni yenyewe si rasmi na wala haija andikwa popote ila inatumika rasmi ndani ya ccm.

Kanuni ina sema hivi,"Mkono mtupu wa anayetaka kupitishwa na ccm kupeperusha bendera ya kugombea uraisi jmt hauchaguliki"

Kwa hiyo anachofanya Lowasa na watarajiwa wengine ndani ya ccm ni kufanya mkono/mikono ichagulike, hivyo tu basi.
 
TEAM Lowasa inafanya kila njia kuhakikisha inaungwa mkono kila sekta,kwa sasa Team hiyo imewaweka mfukoni baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na waan dishi wao ili taarifa zake ziweze kutoka kwenye magazeti hayo bila kugugumizi tena kwa uzito wa aina yake huku taarifa mbaya isipewe nafasi.Pia kuna taarifa kuwa viongozi wa vyuo vikuu wamemwagiwa mamilioni ya fedha ili kuingiza wanachama wengi zaidi wanaomuunga mkono mzee kwa kuwapatia posho ya sh,10,000 kila mwezi inayotumwa kwa siri kubwa kwa njia ya M pesa.

Waandishi wa habari Arusha (team Lowasa) sasa ni mwendo mdundo kila siku ni press ya mkakati kwa Lowasa ,lengo ni kuhakikisha mazuri ya yake yanajulikana,hata akijikwaa kesho yake anaita press.
 
Back
Top Bottom