Lowassa kutoka muathirika(victim) mpaka Muathiri(aggressor)

Lowassa kutoka muathirika(victim) mpaka Muathiri(aggressor)

Yani hata mfanyeje mi napenda kuwaambia kuwa bila sisi kuomba sana kwa mwenyezi Mungu basi Tanzania itakuwa chini ya freemason na hii ni kweli we ona watu wanavyomkubali lowassa yani tumeshaingiwa na pepo mbaya sasa
Mkuu,
Maombi bila matendo ni kazi bure!

Fanya kazi yako kwa kutumia nyenzo alizokupatia Mungu wako!
 
Mkuu,
Hii ya kupasuliwa wala isikupe tatizo, niachie mimi.

Jenga hoja mbadala na kama unadhani hakuna hoja, basi hata kusoma na kuondoka inahesabika ni kutoa mchango.

Mkuu una busara sana..thou nko upande wa UKAWA' ila kiukweli emotional intelligence yako kubwa sana!
 
Dr. Slaa naye si achukue form tu au kuzuiwa.
Mkuu,
Ulishuhudia kile kilichofanyika wakati Lowassa akikabidhiwa fomu za kugombea Urais kwa tiketi cha CHADEMA?

Huo ulikuwa ni ujumbe unaojitoshereza wa kusema, hakuna nafasi tena kwa mwanachama mwingine ndani ya CHADEMA kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA!
 
Angebaki ccm usingekuwa na ubavu wa kusema piga ccm una kimavi kanawe una**ka
 
Lucy hivi lowassa kakukosea nini? Mwacheni baba Wa watu kwani umelipwa kiasi gani ? Kumbuka lowassa hajakukosea wewe lakini kiherehere ulichonacho kwako inashangaza ili malipo in hapa hapa duniani
 
Mkuu,
Ulishuhudia kile kilichofanyika wakati Lowassa akikabidhiwa fomu za kugombea Urais kwa tiketi cha CHADEMA?

Huo ulikuwa ni ujumbe unaojitoshereza wa kusema, hakuna nafasi tena kwa mwanachama mwingine ndani ya CHADEMA kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA!

Fomu za uraisi zilikuwa wazi toka lini?
 
katiba ya chadema ipo tofauti sana na ccm. soma hapo chini.

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-

(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili yamapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.
Na huko ndipo alipojichimbia slaa akifanya maandalizi.
 
Mkuu upo sawa kimantiki, japo CDM tatizo lao sio Lowassa kupitishwa kibabe maana kwao hakuna aliyeomba kugombea wala hakukua na makundi ya uraisi, the only problem arising ni mtu anaepitishwa kugombea uraisi ndio huyo huyo ambae waliutangazia uma kwamba ni fisadi na hafai kwenye jamii.

Sasa utata uliopo ni kundi moja likiongozwa na mwenyekiti wao wao wapo tayari kupata kura nyingi na madaraka hata kwa mambo ambayo waliyaita haramu, whili kundi lingine likiongozwa na mtendaji wao yaani katibu mkuu, wao hawapo tayari kumpokea huyu bwana kwani wanaamini si msafi na hafai kuwaongoza, bora hata kukosa kura kuliko kumtumia mchafu huyu.

So mgogoro wao mkuu ni wa kumtumia mtu waliemuita fisadi kuwaongoza kuwatoa mafisadi regardless ya uchafu wake bila kujua jamiii itawaonaje. Kiukweli EL kawaletea swna mgogoro Chadema japo hawausemi wazi wananitahidi kujificha, na kiukweli wasipotatua mapema muda si rafiki kwao wataachwa wakishangaa.
Mkuu,
Ukiweka kando hoja ya maadili ya Lowassa ambayo itajadiliwa na vikao ndani ya chama baada ya kurudisha fomu za kugombea Urais, kilichofanyika wakati wa kumpatia Lowassa fomu za ugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA kinaeleza zaidi chaguo la baadhi wakuu wa chama katika nafasi hiyo.

Picha tuliyokuwa tunaonyesha siku amabayo Lowassa anachukua fomu inasema, mlango umefungwa kwa wanaCHADEMA mwingine katika nafasi ya Urais kwa tiketi ya CHADEMA.

Kilichofanyika siku ile kimantiki ni kumtambulisha Lowassa kwa Watanzania kama ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo ndani ya CHADEMA nadhani hata UKAWA.

Kinachoendelea kwa sasa ni kutimiza taratibu tu zingine za kikanuni!
 
hivi lowassa kakukosea nini? Mwacheni baba Wa watu kwani umelipwa kiasi gani ? Kumbuka lowassa hajakukosea wewe lakini kiherehere ulichonacho kwako inashangaza ili malipo in hapa hapa duniani
Mkuu,
Mimi ninaandika kile ambacho kiko katika fikra zangu.

Lowassa hawezi kuepuka mijadala inayomhusu yeye kwa sababu kuu ni mwanasiasa anayetafuta ajira kupitia sanduku la kura kutoka kwa wapiga kura.

Kinachotakiwa ni kujibu hoja kwa kutumia hoja mbadala!
 
Tanzania hutujawa democracy iliyo imaalika kutokana kuwa na mfumo wa serikari ya chama kimoja kutawara vyama vingi.hivyo kwa vyama vichanga kama chadema,cuf na vinginevyo ukisema uchaguwe viongozi wa wa chama kwa njia ya kidemocrasia utakuta unapata viongozi ambao nidhaifu kununuliwa na chama tawala. Ndio maana hawa viongozi wa vyama vya upizani wanakuwa viongozi wa mda mrefu.hivyo Luwasa lazima apite bila kupingwa kwa sasabu moja nayo kuwaonyesha wana ccm kuwa nchi ni ya watu sio ya viongozi
 
Hakuna asiyefahamu kama zoezi la kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM lilikuwa limegubikwa kwa usiri, sintofahamu na ubabe. Baadhi ya watu walipiga kelele sana wakiwazodoa CCM katika hitimisho la mchakato huo ambao ulizaa uteuzi wa John Pombe Magufuli kama mgombea Urais wa tiketi ya CCM.

Demokrasia ya CCM ilikuwa imesimama katika idea ya consequentialism ambayo inesema, the ends justify the means. Ninaweza kusema viongozi wa CCM walifanya foul/abominable katika zoezi la uteuzi ili kumpata waliyekuwa wakimtaka!

Edward Lowassa alilalamika sana katika zoezi hilo ambalo liliua ndoto yake ya kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi CCM. Foul zile zile ambazo Lowassa alizipigia kelele sana ndizo kwa sasa anazifanya au zinafanywa ndani ya CHADEMA/UKAWA ili zimsaidie katika kufikia malengo yake ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA!

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wanafanya/wamefanya pia zoezi La kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA kuwa la usiri, sintofahamu na ubabe kama ilivyokuwa ndani ya CCM.

Kwa sasa tunaambiwa Lowassa ni mgombea pekee wa kiti cha Urais kwa tiketi ya CHADEMA wakati huo huo kuna viongozi na wanachama wanalalamika kuhusu taratibu na kanuni zilizotumika kufikia uamuzi huo.

Ama kweli ukishangaa ya CCM utayaona ya CHADEMA/UKAWA!

Hizi ndizo demokrasia za Tanzania!


Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mstakhabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na Makaburu kama mkakati wa kujinusuru na kutoa nafasi kukabiri janga kubwa kuliko zote wakati huo la kuondolewa serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na Makaburu. Wakomunisti wa Afrika ya Kusini waliingia ubia na ANC ya mabwanyenye weusi ili kutokomeza kwanza ukaburu na mapambano na ubepari yaje baadaye. Katika Vita Kuu ya Dunia ya Pili wakomunisti walishirikiana na mabwenyenye wa mrengo wa kulia na kati kutokomeza janga kubwa zaidi wakati huo la ufashisti, yaani ubepari wa mrengo wa wa kulia kupitiliza. Hivyo hivyo mapambano ya kuleta uhuru wa Tanganyika yalivyo unganisha nguvu za mabwenyenye wazungu na waasia pamoja na zile za wakulima na wafanyakazi wa rangi zote kwa azimio lile la mkutano mkuu wa Tanu wa 1958 pale Tabora. Hivyo hivyo Mandela na ANC waliingia "urafiki wa mashaka" na De Clerk kiongozi wa Makaburu ili kuondolewa ukaburu kuwe kwa amani ya "kula matapishi" ya kuwalaani huko nyuma kuwa ni wabaya wa Mwaafrika!!

Mabadiliko ya haraka haraka yanayoendelea hapa Tanzania yenye lengo la kuondoa CCM madarakani kama chama dola kinachodumaza na kudhoofisha ushindani wa kisiasa miongoni mwa mabwenyenye wa tabaka tawala Tanzania ni mabadiliko yatakayoleta neema kwa Watanzania wote. Ile tu CCM kudhoofishwa na kujiunga UKAWA kwa Lowassa ni kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu ya mchukuzi.....Nikuondoa kizingiti kikuu cha kushamiri kwa demokrasia pana na maendeleo endelevu Tanzania ambacho ni kuhodhiwa na ukiritimba wa chama dola cha CCM kinachojinadi kama chama cha mrengo wa kushoto wakati ni chama cha mrengo wa kulia kama vyama vyote vya siasa Tanzania kwa sasa.

Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi ka wana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005, ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakaochukua sura ya demokrasia zaidi ili kuwa na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia (tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo), sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Ghafla mwanasiasa mwenye nguvu nyingi ndani ya chama cha kifisadi cha CCM, mwanasiasa ambaye umaaarufu wake umetokana na kuongoza mtandao uliouweka utawala wa sasa wa CCM madarakani, Ndugu Edward Lowassa, amekasirishwa na kukatwa jina lake na aliodhani ni rafiki zake ndani ya CCM na kuamua kusema basi na lolote liwe kwa kujiunga na vuguvugu la kupigania katiba mpya!! Naye sasa kang'amua kuwa Katiba ya sasa na ile Pendekezwa ni za ovyo maana haziruhusu kuwepo mgombea huru bila mizengwe. Hasira za Lowassa zimezaa tunda zuri la kug'amua kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Hasira hizi za mkizi ni furaha ya kunguru na ni busara kwa viongozi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla kutoongopa "kula matapishi yao" kwa kumkaribisha Ndugu Lowassa...huyu huyu waliomwita fisadi... kujiunga na UKAWA na kugombea urais. Nafasi ya kihistoria imejitokeza ya kukiondoa CCM madarakani kwa amani!!

Sishangai wasaliti wa vuguvugu la kukiondoa CCM madarakani wanatushauri sisi Watanzania wenye shauku ya kuutumia upenyo huu wa mpasuko ndani ya CCM kukiondoa CCM madaraka!!! Eti tuombe radhi kwa" kula matapishi yetu" wote tulio wahi kumwita Lowassa fisadi! Wao wanataka tuendelee kuvumilia kutawaliwa na CCM labda kwa miaka mitano au zaidi hivi mpaka chama kipya cha watakatifu kiitwacho ACT-Wazalendo kitakapo kuwa tayari kututawala badala ya CCM!! Sishangai kusikia ushauri huu kutoka kwa wasaliti hawa ambao kazi yao hata huko nyuma imekuwa ni kuudhoofisha upinzani dhidi ya CCM na kukisaidia CCM kiendeleee kuwa madarakani!! Hawa jamaa ni wasomi sana na ni wajanja sana, ilo lazima kulikiri!!!

Sitashanga kama haya ninayoyasema yatapigwa madongo na wasaliti hawa!! Historia itakapoandikwa baada ya UKAWA kupata viti vingi zaidi Bunge lijalo au hata kuutwaa urais na kupata Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba, itawapa hukumu yao stahiki, wajanja na welevu hawa! Bila shaka wanaoomba UKAWA ishindwe kupata viti vingi Bunge lijalo na iukose urais na hivyo tuendelee kutawaliwa na CCM na wao wapate viti vya kutosha kuwa viongozi wakuu wa eti upinzani muruwa wenye maadili ya Azimio la Arusha Tanzania!! Ni haki yao ya binadamu kuendelea na matumaini haya kama na sisi tulivyo na haki ya kuendelea na matumani yetu ya uwezekano wa ushindi mnono chini ya UKAWA dhidi ya ukiritimba wa chama kimoja chama dola cha CCM!
 
Yaani wewe ni ndumilakuwili. Lowasa akirudi CCM na wewe rutakuona ukijipendekeza tena

Inawezekana Mbowe ni zaidi ya tulivyokuwa tunamwamini. Uteuzi wa awali ulishavuja kwamba Slaa ndiye mgombea mteule wa Chadema, lakini Mbowe ambaye alitakiwa kutangaza au kuidhinisha mchakacho uendelee akasitisha kwa sababu kumbe alikuwa na dau la kumpata Lowasa nje ya utaratibu wa kawaida.

Sishangai kwa ukimya na kujificha kwa Dr Slaa, hatutaki yamtokee yaliyompata Chacha Wangwe. Uenyekiti Chadema ni wa kurithishwa toka kwa Mtei mkwe wake. Hawa wengine ni wapambe tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom