Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,507
Hakuna asiyefahamu kama zoezi la kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM lilikuwa limegubikwa kwa usiri, sintofahamu na ubabe. Baadhi ya watu walipiga kelele sana wakiwazodoa CCM katika hitimisho la mchakato huo ambao ulizaa uteuzi wa John Pombe Magufuli kama mgombea Urais wa tiketi ya CCM.
Demokrasia ya CCM ilikuwa imesimama katika idea ya consequentialism ambayo inesema, the ends justify the means. Ninaweza kusema viongozi wa CCM walifanya foul/abominable katika zoezi la uteuzi ili kumpata waliyekuwa wakimtaka!
Edward Lowassa alilalamika sana katika zoezi hilo ambalo liliua ndoto yake ya kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi CCM. Foul zile zile ambazo Lowassa alizipigia kelele sana ndizo kwa sasa anazifanya au zinafanywa ndani ya CHADEMA/UKAWA ili zimsaidie katika kufikia malengo yake ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA!
Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wanafanya/wamefanya pia zoezi La kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA kuwa la usiri, sintofahamu na ubabe kama ilivyokuwa ndani ya CCM.
Kwa sasa tunaambiwa Lowassa ni mgombea pekee wa kiti cha Urais kwa tiketi ya CHADEMA wakati huo huo kuna viongozi na wanachama wanalalamika kuhusu taratibu na kanuni zilizotumika kufikia uamuzi huo.
Ama kweli ukishangaa ya CCM utayaona ya CHADEMA/UKAWA!
Hizi ndizo demokrasia za Tanzania!

Last edited by a moderator: