Lowassa kunyang'anywa shamba

Lowassa kunyang'anywa shamba

Serikali kupitia waziri wa ardhi nyumba na makazi, imetangaza uamuzi huo bungeni wa kumnyang'anya shamba la makuyuni lililopo monduli, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond ndugu Lowassa, na kuwagawia wananchi wa eneo hilo.


Chanzo: Jambo leo
Ni vizuri akinyang'anywa ili tuendelee mbele.
Wale wenye mashamba kule mvomero, karagwe n.k watafuatia baada ya hili
 
sasa chadema ndio watajua ufisadi ni mtu na sio mfumo leo hii mbunge wa monduli analalamika kwa sababu mbunge aliyepita alijitwalia ardhi kubwa huku wananchi wake wengi wakiwa hawana ardhi hapo ndio taratibu tutaona sehemu ya pili ya sinema ya chadema na lowasa
 
Mdogo mdogo na uelewa mdogo wa #hapakazitu naona tutafikia point hata mwenye magari matatu anyang'anywe mawili ili wagawiwe wasio nayo.

Kuna watu ukimmilikisha kiwanja leo kesho anakiuza na saa nyingine sio hata kwa nia mbaya, kuna mtu mwingine anafurahi kuona shamba lake lina ng'ombe 1,000 wakati wengine wanao uwezo zaidi lakini akiwaona ng'ombe 10 tu anaridhika.

Serikali ingejiuliza kwanza ni nini chanzo cha baadhi kumiliki ardhi kubwa na wengine kukosa na kama walifuata taratibu kuipata. Tukumbuke nchi yetu tangu uhuru haijawahi kukaa hata siku moja bila serikali na tena ya chama hicho hicho.
 
mbona yapo mengi tu alijimilikisha kwa kutumia madaraka yake? Sumai je?
Walio na mashamba makubwa ilhali wanashindwa kuyaendeleza watashughurikiwa wote bila ya kujali nafasi zao.. hii ni kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 5 ya mwaka 1999.
 
Hivi kama ameamua shamba lake liwe mazalia ya swala na digidigi kunaweza tatizo! Watz bwana, wanataka kila mtu alime. Hatuna ubunifu.
 
Hiyo ni amsha popo bado kazi inakuja, ajipange tu alinyea tu kambi mwenyewe
 
Mdogo mdogo na uelewa mdogo wa #hapakazitu naona tutafikia point hata mwenye magari matatu anyang'anywe mawili ili wagawiwe wasio nayo.
Kuna watu ukimmilikisha kiwanja leo kesho anakiuza na saa nyingine sio hata kwa nia mbaya, kuna mtu mwingine anafurahi kuona shamba lake lina ng'ombe 1,000 wakati wengine wanao uwezo zaidi lakini akiwaona ng'ombe 10 tu anaridhika. Serikali ingejiuliza kwanza ni nini chanzo cha baadhi kumiliki ardhi kubwa na wengine kukosa na kama walifuata taratibu kuipata. Tukumbuke nchi yetu tangu uhuru haijawahi kukaa hata siku moja bila serikali na tena ya chama hicho hicho.


Hatutaki matatizo yanayowakumba Wakenya kutokea Tanzania hiyo ndiyo sababu, Wakenya pia waliuliza maswali kama yako miaka ya '60 na jibu lake likawa kama lako kwamba watu waachiwe wamilikia ardhi wanavyotaka hata kama hawawendelezi miaka 50 baadaye leo hii chanzo kikubwa cha ugomvi Kenya na kupelekea vita ya mwaka 2007 ni ARDHI ni makosa yaliyofanywa miaka 50 iliyopita kuna familia chache Kenya zinamilikia nusu ya nchi nzima na raia walio wengi hawana hata pa kulima bustani na kibaya zaidi hiyo ardhi wanahodhi tu na hawafanyii chochote na ili kukiepusha kizazi kijazo na adha kama ya Kenya, ndiyo maana Serikali yetu hairuhusu kuhodhi Ardhi, sheria yetu inasema kwamba Ardhi yote TZ ni mali ya Serikali na Serikali ndiyo huamua itumikaje!
 
"Ninayo hati hapa ya shamba la Makuyuni-Monduli,Arusha imesainiwa na Lowassa nasema tutairekebisha ili shamba hilo tuligawe kwa wananchi,Shamba hilo wakati wa rais Mkapa lilitaifishwa kutoka kwa mfanyabiashara Stein lakini Lowassa akalichukua."William Lukuvi bungeni jana jioni.
 
"Ninayo hati hapa ya shamba la Makuyuni-Monduli,Arusha imesainiwa na Lowassa nasema tutairekebisha ili shamba hilo tuligawe kwa wananchi,Shamba hilo wakati wa rais Mkapa lilitaifishwa kutoka kwa mfanyabiashara Stein lakini Lowassa akalichukua."William Lukuvi bungeni jana jioni.


Saafi sana! Haki haipotei hata siku moja hucheleweshwa tu!
 
Serikali kupitia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, imetangaza uamuzi huo bungeni wa kumnyang'anya shamba la Makuyuni lililopo Monduli, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond ndugu Lowassa, na kuwagawia wananchi wa eneo hilo.

Chanzo: Jambo leo
tayari wameshalichukua ama vepe naona heading imechange
 
Back
Top Bottom