Lowassa katika kashfa mpya! Ni ya uuzwaji kiholela wa UDA

Unafikir yeye siyo mjinga, akila manyoya anatupia kwa jirani.
Subiri kitu solex kiingie mjengoni, hao wamiliki vivuli lazima waonyeshe vyanzo vya mapato vilivyowawezesha kununua hizo Runch. Lazima watazikimbia tu.

Lowassa na Sumaye wanataka kudefend mali zao ndo maana wamekomaa, wanataka kushika dola. Pombe ikiingia ikulu ndo watajua kuwa maharagwe sio supu.
 
Hivi huyu Lowassa ni genius kiasi gani? Hakuna mtu anayeweza kumzuia kufanya lolote nchi hii? Inawezekana kweli? Ni huyu huyu Masaburi wakati wabunge wa Dar wanamshambulia bungeni kuwa kauza UDA alisema wabunge wa Dar wanafikiri kwa kutumia Makalio. Leo hii nae Kaanza kufikiri kwa kutumia makalio?

Dr Masaburi Anajisafisha kwa fagio la chuma subiri tarehe 25-10-2015 ametuma maombi atapata majibu
 
Mbona muda huo wote walikuwa hawajamsema kwamba ndiye mhusika na uuzaji wa shirika la Uda na tunasikia haya baada tu ya kuhamia Ukawa au shirika hilo liliuzwa baada ya yeye kuhamia Ukawa? Sitetei (kama kweli ni yeye alisimamia huo uuzwaji, lakini ninachoshangaa ni kwamba wakati akiwa CCM kulikuwa kimya na sasa kwa vile ametoka kelele nyingi).

Huu ni utamaduni wenu wanasiasa hata kabla hajaamia UKAWA ukawa walimuita fisad papa leo ni shujaa,amin usiamin mtaji mkubwa wa wanasiasa tz ni ujinga na uvivu wa kufikir wa watz,leo ccm kumtuhum lowasa ni upuuz pia kwani wao ndo wamemtengeneza kufikia hapo alipo. Tunahtaji self determination kama taifa ili kuuona ukweli wa mambo mengi ya hovyo yanayoendelea hapa nchini
 
Mbona muda huo wote walikuwa hawajamsema kwamba ndiye mhusika na uuzaji wa shirika la Uda na tunasikia haya baada tu ya kuhamia Ukawa au shirika hilo liliuzwa baada ya yeye kuhamia Ukawa? Sitetei (kama kweli ni yeye alisimamia huo uuzwaji, lakini ninachoshangaa ni kwamba wakati akiwa CCM kulikuwa kimya na sasa kwa vile ametoka kelele nyingi).

Mbona huelewi somo? Huyu Masaburi aliulizwa swali kwenye mdahalo akituhumiwa kuuza UDA. Ndipo akaeleza mchakato mzima wa jinsi UDA ilivyouzwa na ikaonekana Lowasa kuhusika.
 
Masaburi anamchokoza Ridhwan Kikwete na Kisena aka Simon Group ... Ilikuwaje UDA ikatumika kwenye kampeni za CCM ?

Yaani unaanzisha mada nyingine ili watu wahame siyo, mwone sura kama Lowassa yuko Geita anaji...
 
Huyu mzee atakuja kufia chooni kwa pressure kutokana na msukumo wake wa kutaka kulazimisha mambo ambayo hayahitaji njia za ulaghai. Kwanza sijaona hata sababu za CCM kumchagua kama mgombea Ubunge.
 
Nani asiyemjua Masaburi, kwamba upigaji ndio hulka yake kama supplies officer tangu akiwa KIBUKU, baadaye mradi wa Elimu nk. Sisi tuliokuwa karibu naye tunamjua nje ndani. Hata u Dr wake ni wa kupiga tu, aache danganya watu hapa. CCM wote no timu ya wapigaji, ndio maana lazima itoke hata kwa panga. Mwizi huwa anasurubiwa na CCM suruba yake imetimia.
 
ccm wanatapatapa wakajiulize mwenye simoni group ni nani wakimjua basi hakuna sababu ya kulalama ni kuiondoa ccm tu
 
Nani asiyemjua Masaburi, kwamba upigaji ndio hulka yake kama supplies officer tangu akiwa KIBUKU, baadaye mradi wa Elimu nk. Sisi tuliokuwa karibu naye tunamjua nje ndani. Hata u Dr wake ni wa kupiga tu, aache danganya watu hapa. CCM wote no timu ya wapigaji, ndio maana lazima itoke hata kwa panga. Mwizi huwa anasurubiwa na CCM suruba yake imetimia.
Watakuja magamba na kumtetea huyo bweg. . Masaburi humu..
 
Huyu mzee sasa anatia uvivu hata wa kudhani kuwa angegombea urais. Watanzania tuamke nchi inaenda kuuzwa hiii. Mtu anakuwa na kashfa lukuki za uuzwaji wa ranchi za ufugaji ng'ombe taifa, richmond na sasa UDA. Tuachaneni na huyu mtu jamani.

Hapo ndio umeambiwa na ukatumia na akili zako! usingeambiwa je! Mpuuzi wewe!!
 
masaburi anatapatapa kwani shirika la uda lipo chini ya jiji la dar es salaam. sasa kumsingizia waziri mkuu ni kujaribu kupotosha ukweli tu. na kama ni lowassa mbona masaburi hakuzungumza hayo miaka yote na mbona waliopelekwa kortini ni akina iddi simba na lowassa hakuguswa? Masaburi ndiye aliyeuza kwani alipotaka fedha ziongezwe na hazikuongezwa ni kwamba alitumia mbinu hiyo ili kumshawishi kisena amnyamazishe na alipopata mgawo wake akaanzisha chuo chanika na akakaa kimya muda wote huo.
Akizungumza kwenye mdahalo uliondaliwa na kurushwa na AZAM TV jana, Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo, , Dr. Didas Masaburi(CCM), alisema anayepaswa kulaumiwa kwa uuzwaji holela wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) ni LOWASSA, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, kwani ndiye aliyekuwa msimamizi wa mchakato huo mwaka 2006 hadi 2008.

"Kwa mujibu wa sheria , Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa Serikali za Mitaa", alisema Dr. Didas Masaburi katika mdahalo uliohudhuriwa pia na wgombea wengine, Said Kubenea wa Chadema, Zangina Shangana(ACT-Wazalendo) na Renatus Muhabi(CCK).

Awali ilidhaniwa kuwa hoja ya uuzwaji wa UDA ungempa wakati mgumu Dr. Masaburi, lakini hali haikuwa hivyo kwani alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi ulioeleweka na kumtupia lawama Lowassa. Mbali na Richmond, Lowassa pia anatuhumiwa kuwa na hisa katika kampuni ya Integrated Property Limited inayohusishwa na ujenzi ambayo haikuiorodhesha kwenye Tume ya Maadili kwa mujibu wa sheria kama mtumishi wa Umma.

Mimi sijahusika na ufisadi katika uuzwaji wa UDA, nilichokifanya ni kupandisha bei yake kutoka bil.1 hadi sh.bil. 5.7nilipoingia kwenye UMEYA na kukuta shirika hilo limeuzwa isivyo halali.

Meya 2011niligundua mkataba usio sawa wa uuzwaji wa UDA baada ya kuajiri kampuni ya Ukaguzi wa hesabu ya KPMG, Bei yake haikulingana na thamani ya mali za shirika hilo, hivyo niliamuru mnunuzi, Simon group kuongeza fedha.

Soma zaidi RAIA TANZANIA.
View attachment 289852
 
Huyu mzee sasa anatia uvivu hata wa kudhani kuwa angegombea urais. Watanzania tuamke nchi inaenda kuuzwa hiii. Mtu anakuwa na kashfa lukuki za uuzwaji wa ranchi za ufugaji ng'ombe taifa, richmond na sasa UDA. Tuachaneni na huyu mtu jamani.
Kwani amekuoa mpaka uachane nae?
 
Back
Top Bottom