Matukio yaliyojiri hivi karibuni katika medani ya siasa nchini yameonyesha kua mustakabali wa kisiasa wa Mwanasiasa mkongwe Mh Edward Ngoyai Lowasa una utata mkubwa!
Lowasa ni kada wa siku nyingi wa chama chetu cha Mapinduzi. Ni kada ambae amefanya mambo mengi katika chama toka alipokua UDSM miaka ya mwanzoni mwa 1970 enzi za TANU na amewahi kushika nyadhifa mbali mbali za Uongozi katika CCM. Mh Lowasa, kama wote tujuavyo, kwa kutumia ushawishi mkubwa wa fedha ambazo yeye pamoja na familia yake wanazano, aliweza kupata ushindi mnono jimboni kwake Monduli katika chaguzi za NEC pamoja na watu wake wengi kushinda katika NEC wilaya mbalimbali nchini. Kama hiyo haitoshi, kwa kutumia ngawira aliweza pia kuingiza watu wengi katika jumuia zote tatu za chama(Wazazi, Wanawake na Vijana).
Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM katika hotuba zake kwenye jumuia zote tatu alitoa hotuba nzito za kulaani matumizi makubwa ya rushwa kwenye chaguzi. Haiitaji kua "Rocket Scientist" kutambua kua makombora hayoya mwenyekiti wetu mpendwa yalimlenga LAIGHWANAN. Kana kwamba hiyo haitoshi, Mwenyekiti ameunda Secretariat kabambe ya maadili ikiongozwa na Watanzania wazalendo ambao jamii yote (Isipokua wale wabishi wa kuzaliwa ) wanatambua kua wanaichukia SANA rushwa (Mangula na Kinana). Lengo la Mwenyekiti ni kikirudisha chama kwa wananchi na kukiondoa kwa wala rushwa.
Aidha kauli ya mwenyekiti kua "Kuna watu wenye Ndimi mbili, yaani mara wanakisema vizuri chama cha Mapinduzi lakini wakati mwingine wanakiponda" ni dhahili mlengwa ni Laighwanan. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Laighwanan amekua akitoa kauli zenye utata mkubwa ambazo si tu zinapingana na sera za chama chake mwenyewe bali pia zinakidhalilisha chama. Mfano akichangia ujenzi wa shule ya Mkinde tar 2.5. 2012 Laighwanan alisema "Vijana wengi waliokua ccm wamehamia chadema kwani ccm haiwajali na haina nia ya kuwaendeleza". Kauli hiyo ilijibiwa na Waziri Mkuu Mh Pinda tar 6.5. 2012 ambae alisema kua "CCM bado inapendwa na vijana na ccm ina mikakati mingi ya kuwaendeleza, tuache kusikiliza porojo". Aidha, wakati wa chaguzi za ccm huko Dodoma, Mwenyekiti alimpiga kijembe Laighwanan kwa kusema "Wapo wanaosema Vijana wote wamehamia upinzani, ccm tumechagua viongozi wengi vijana na wasomi wazuri na tunaamini watatupa mawazo mapya ya kisasa".
Aidha majuzi Lowasa, bila kupepesa wala kungata maneno nae akawapiga vijembe ccm kwa kusema "Elimu ya sekondarilazma itolewe bure". Hii ni Sera ya wazi ya Chama Dume-Chadema ambayo Mh Dr. W. Slaa aliilezea kwa ufasaha mkubwa kama agenda ya Chadema 2010 lakini ilipingwa vikali na ccm ambayo iliwabeza Chadema kwamba wasiwadanganye na kuwahadaa wananchi hilo haliwezekani kabisa!
Lowasa ameishawatanguliza vijana wake kadhaa kuhamia Chadema mfano Steven Mlontei na James Millya. Kwa hakika, kiroho, LAIGHWANAN yupo CHADEMA!Vile vile , kwakua Lowasa inajulikana wazi kua alitumia rushwa ambayo ilikua ikigawiwa vyooni, kwa mama ntilie na kwenye vibanda vya vocha na kuandikwa sanana magazetini hivyo kitendo cha watu wake kuingia kwa wingi katika NEC inaonyesha wazi rushwa hiyo ililipa. Kutokana na hali hii, kauli kali iliyotolewa na Mh P. Mangula pale mnazi Mmoja ambapo alisema "Wale wote ambao waliingia kwa rushwa watafukuzwa ndani ya Miezi sita" inaonyesha kwamba lowasa huenda nae akatimuliwa CCM kwani haitaeleweka kwa Mangula na wenzake kuwatimua Dagaa na kumwacha KAMBARE.
Je WANACHADEMA, Kwakua Mh S. Sita alisema Chadema ni chama kizuri ambacho kilisifiwa hata na Baba wa Taifa lakini hakina viongozi wa kutosha, ikitokea LAIGHWANAN ametimuliwa CCM apokelewe CHADEMA na kuibeba bendera yake mwaka 2015? Hii pia inazingatia maoni ya baadhi ya watu humu JF ambao wamekua wakisema LAIGHWANAN ni JEMBE na kama Dr Slaa asiposhinda 2015 bora Lowasa awe Rais.
Wadau, je LAIGHWANAN apokelewe CHADEMA??