lufungulo k
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 2,607
- 2,062
mimi si mpinzani bwana , ntapinga kila kitu na hata kitu changu ninachoamini ukiniunga mkono sintakupongeza ntalalamika umeniibia hiyo ndiyo tanzania zaidi ya uijuavyo
Hiyo ndiyo dhamira ya ccm kwa sasa na hili litawezekana pamoja na kuwasaidia wananchi katika ujenzi wa nyumba bora za kisasa chama changu pongezi kwa kuwajali watanzania
Mtoi,
I hate to say this, kwenye watu wanaoongelewa kuuwania uraisi, huyu bwana EL, licha ya wizi wake na ulevi wake wa madaraka akiwa nayo, ndio pekee ameonyesha kuwa na mawazo yenye meno ambayo nchi yetu inahitaji. Tatizo ni vigumu kumuamini kutokana na historia yake mbovu anapopewa madaraka. Tufanyeje sasa Watanzania?
Mkuu wangu Father of All
Naamini Lowasa ni sawa na kata inayoingia kwenye mtungi, si unakumbuka ule msemo "siri ya mtungi aijuaye kata", anajua kuwa serikali ni tegemezi sana hasa kwenye bajeti lakini nachelea kusema huenda ana kifuniko cha siri moyoni na anajua kuwa waliyo kuwa wanapinga yanawezekana.
Nakubaliana na wewe kuwa hajaonyesha njia kuwa itawezekana vipi (Romnesia) lakini naamini anajua kuwa kama wenzake wa ccm wakiwa naka uzalendo kidogo na huruma kwa taifa hili, wanauwezo wa kutoa elimu bure kuanzia msingi hadi sekondari na hata kuwapatia wastaafu wa nchi kiasi cha shilingi elfu 30 kwa mwezi kwa kuanzia ili angalau kuwapunguzia machungu ya kulipa bili za umeme za na maji au kununua mafuta ya taa kwa ajili ya vibatari vyao na kandili zao.
Inawezekana! Waliyopinga miaka 3 iliyopita leo wanakiri hadharani kuwa inawezekana. Hizi ni alama za wanafiki kwenye imani yangu.
Na kasema kwa nchi changa kama ya kwetu muhimu kuwa na intersectoral articulation kwa maana ya elimu,kilimo,miundombinu,viwanda kuwepo na direct link baina ya sekta na sekta..lowasa hata akikosa urais lazima tukubali kuwa ana vision na dira.
Mwanangu Mtoi umeleta hoja nzuri ingawa nasita kukubaliana na Lowassa. Nani atawaruhusu tegemezi na ombaomba kutoa elimu ya bure wakati bajeti yao inategemea wafadhili. Laiti angesema kuwa kama tutasimamia raslimali zetu na kodi vilivyo hili la kutoa elimu bure lingewezekana ningemwelewa. Lowassa anaongea kama mgombea wa urais wa Marekani Mitt Romney. Ni pendekezo zuri ingawa sijui kama alionyesha jinsi ya kulifanikisha.
Akiongea kupitia kituo cha channel 10 kwenye taarifa ya habari ya saa 1 leo 18 Nov,2012 Mheshimiwa Lowassa amesema serikali inaweza kugharamia elimu ya msingi na sekondari kwa wananchi wake kuwa bure, na elimu ya sekondari ikafanywa kuwa ya lazima na ya kiwango (quality). Ili kuwafanya vijana kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira.
Kauli hii ni muendelezo wa wana CCM kuendelea kukubali sera kadhaa kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010, juzi Kinana alisema serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawezi kujenge nyumba bora kwa ajili ya makazi.
mimi si mpinzani bwana , ntapinga kila kitu na hata kitu changu ninachoamini ukiniunga mkono sintakupongeza ntalalamika umeniibia hiyo ndiyo tanzania zaidi ya uijuavyo
Natamani sana tuwe na journalists navyombo vya habari vinavyoweza ku-retreave controversial statements za wanasiasa walagai kama magamba.
Akiongea kupitia kituo cha channel 10 kwenye taarifa ya habari ya saa 1 leo 18 Nov,2012 Mheshimiwa Lowassa amesema serikali inaweza kugharamia elimu ya msingi na sekondari kwa wananchi wake kuwa bure, na elimu ya sekondari ikafanywa kuwa ya lazima na ya kiwango (quality). Ili kuwafanya vijana kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira.
Kauli hii ni muendelezo wa wana CCM kuendelea kukubali sera kadhaa kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010, juzi Kinana alisema serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawezi kujenge nyumba bora kwa ajili ya makazi.
nasikia kapata magurudumu mapya, hayapati pacha hayo....Nilifikiri wamesham write off by now? kumbe bado yupo kwenye mbio?