Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Mwanangu Mtoi umeleta hoja nzuri ingawa nasita kukubaliana na Lowassa. Nani atawaruhusu tegemezi na ombaomba kutoa elimu ya bure wakati bajeti yao inategemea wafadhili. Laiti angesema kuwa kama tutasimamia raslimali zetu na kodi vilivyo hili la kutoa elimu bure lingewezekana ningemwelewa. Lowassa anaongea kama mgombea wa urais wa Marekani Mitt Romney. Ni pendekezo zuri ingawa sijui kama alionyesha jinsi ya kulifanikisha.

Nnaomba kutofautiana na wewe hapa.Mkuu usimamizi ukiwa wa kutosha ktk raslimali zetu/matumizi makubwa yanayotokana na ukubwa wa Serikali hii(usio na tija)/kufufua viwanda vilivyokufa na mengine mengi ya kufanana na hayo ELIMU BURE INAWEZEKANA.Mimi ninadhani Lowasa anapozungumza hivyo anajua ni njia ipi itatumika elimu bere kupatika hapa Tanzania,vivyo hivyo ktk ilani ya Chadema 2010 nao walikwisha ainisha ni namna gani ya kupata elimu bure.
 
Mkuu chama.
Umekuwa na kauli changanya galasa kwa wakati mmoja! Naomba uweke sawasawa kauli hizi ili niweze kukujibu kwa ufasaha

Kwenye mchango wako umesema "Elimu ya bure kwa maana ya bure haiwezekani; labda tu angesema gharama zipunguzwe na kwa wale wanaotaoka kwenye familia zisizo na uwezo serikali iwaekee upendeleo maalumu; ukichunguza kwa undani serikali bado inatoa elimu ya bure..."

Chama ndugu yangu kama dhimira ya kweli ikiwepo kama jinsi ilani ya chama chetu ilivyokuwa iweka mfuko wa cement hata kwa shilingi 5000 inawezekana! Mbona kumekuwa na stimulus package kuuhami uchumi na bado wajanja wa ccm walizitia ndani? pesa kama ile inaweza kuingizwa kwenye mitaji ya viwanda vya cement kwa jina lingine au hata ruzuku ambayo itasaidia viwanda husika visipate hasara kulingana na gharama za uzalishaji pamoja na malighafi. tukiamua hata bati liuzwe mia 500 tunaweza! Ni dhamira tu ya kweli na mipango madhubuti kwa kuweka mikakati makini kuliwezesha hilo.
 
Last edited by a moderator:
inawezekana kulifanikisha ndugu yangu LOOK mishahara yao isiyo na umuhimu wowote, angalia sekta ya madini isiyo na faida hata pale yanapopatikana mf. hulyankulu KAHAMA na mwadui SHINYANGA hizo ni sektachache ambazo zinaweza kufanya hiyo kazi
 
Mkuu Mtoi
Elimu bure kwa maana ya Lowas hilo halipo; kama unakumbuka zama hizo wakati wa elimu ya bure mpaka madaftari ya kuandikia yalikuwa yanatolewa shule; jukumu la mzazi lilikuwa ni kuhakikisha mwanafunzi anakwenda shule gharama za elimu 100% ilikuwa ni serikali inatoa; hata sasa hivi kiwango wanachochangia wazazi bado ni kidogo haziendani na gharama halisi; vijana wangu walifaulu kwenda shule bweni niliamua kuwapeleka shule private hicho nilichokuwa nilipe serikalini na nilicholipa private ni tofauti kabisa; bado serikali imejitwisha mzigo mkubwa; kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo serikali inaendelea kuchangia kiasi kikubwa; narudia kama hukuelewa serikali bado inatoa elimu bure ingawaje imetumia hekima za kisiasa kuwaridhisha IMF na WB; ilichoomba serikali badala ya wao kutoa 100% imeomba wananchi nao wachangie walau 20%. Mh. Lowasa anataka kuwadanganya watanzania analijua hilo fika; serikali bado ina majukumu mengi ya kuwahudumia wananchi; mkuu mwanasiasa asikudanganye kinacho determine selling price ni production cost; bei za bidhaa hazipangwi kwenye majukwaa ya siasa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Mwanangu Ciril vipi AR hamjambo. Kimsingi tunaongea kitu kimoja sema kwa approaches tofauti. Ila tuambie hiyo njia unayoamini Lowassa anajua badala ya URomney or romnesia.
 
Mkuu chama.
Mchango wako una mashiko sana lakini kwa heshima na taadhima naomba nikuambie kuwa tukiwa na dhamira ya dhati na kuwa na viongozi wenye kutembea juu ya kauli zao huku wakihakikisha kuwa kila senti kwenye raslimali zetu inatumika ipasavyo bila upotevu au kudondokea kwenye matundu ya wajanja wachache, tunaweza kabisa kuwa na mashule bora yenye vifaa bora na walimu bora na elimu bora ya bure inayogharimiwa na serikali husika.

Kwa sasa hata mfumo wenyewe wa kukusanya kodi una mapungufu mengi na mapato mengi yanapotea bure. Ni Tanzania pekee ambayo mfanyakazi wa serikali wakati mwingine analipa kodi kubwa kuliko mfanya biashara anayeingiza mamilioni ya shilingi kwa siku au kwa mwezi.

Mkuu chama kwa swala la kusomesha serikali haija jitwisha mzigo! Hilo ni swala la kikatiba na ni jukumu lake la kimsingi kusomesha maana ina wakamua wananchi wake kodi kwenye huduma na biadhaa mbalimbali. Sikutegemea uionee huruma serikali kwenye hili maana ni jukumu lake la msingi tena bila visingizio.

Kaka chama! Leo umekuwa objective kutofautiana na wana ccm wenzako lakini pia na sera za ccm maana sikujua kuwa kwa mapenzi na mahaba yako unaweza kusomesha wanao private huku ukiacha shule zilizopigiwa chepuo la kufa mtu na chama chako.

Nimegundua kuwa huamini katika baadhi ya mambo ndani ya ccm! Sitaki kusema unaamini kwenye sera za chama gani lakini wewe ndio una majibu ya kina.

Kila jema na lenye kheri lisikuponyoke wangu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.
Weka sawasawa kisu kwenye mfupa! Nani kapinga na leo anakuja kukubali kuwa yanawezekana? Mpinzani ni yupi aliyesema kuwa ina wezekana akapigwa kuwa haiwezekani?

Ngoja nikusaidie kwa kiwango chako cha uelewa.

Chagua herufi ya jibu sahihi kwenye maswali yafuatayo hapa chini.

1. Chama kilicho andika kwenye ilani yake ya 2010 kuwa elimu ya bure inawezekani kuanzia msingi hadi sekondari ni?

A. Chadema
B. CCM
C. CUF

2. Chama kilicho kuwa mstari wa mbele kuwaaminisha wananchi kuwa swali hilo hapo juu (swali la 1) haliwezekani ni.

A. CUF
B. Chadema
C. CCM

Jipange urudi upya mkuu. Uache kufiri kwa kupiga mbizi. "Mbona mna akili za samaki nyie, alaaaa" - Dr Karume.(Kauli ya aliye kuwa raisi wa Zanzibar akiwaambia wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya ccm ukumbi wa kizota- Dodoma)
mimi ni mpinzani bwana CDM , ntapinga kila kitu cha CCM, na hata wakiniunga mkono na kutekeleza sera zangu kama hazitakinufaisha chama changu SINTAWAPONGEZA ntawashtaki kwa wananchi kuwa wameniibia , nadhani mkuu umenielewa hii ndiyo tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
Mtoi,
I hate to say this, kwenye watu wanaoongelewa kuuwania uraisi, huyu bwana EL, licha ya wizi wake na ulevi wake wa madaraka akiwa nayo, ndio pekee ameonyesha kuwa na mawazo yenye meno ambayo nchi yetu inahitaji. Tatizo ni vigumu kumuamini kutokana na historia yake mbovu anapopewa madaraka. Tufanyeje sasa Watanzania?

Hatutufai hata kidogo afadhali akae kimya ni wa kuogopa kama ukoma Mtu huyu
Na mwenye masikio na asikie.
 
Kwanini asilete hoja Bungeni au mswada wa sheria Bungeni wa kuhakikisha hili linakuwa kweli?
 
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!
kiwatengu,

..hakuna haja ya kutaifisha shule binafsi.

..kinachotakiwa ni kuziboresha shule za sekondari ili ziweze kushindana na private schools.

..tukifikia hapo hata matajiri wataacha kupeleka watoto wao ktk shule za private.

..nakumbuka enzi zetu wanafunzi walikuwa wanaona fahari kusoma shule za serikali kwasababu zilikuwa zinafanya vizuri kuliko shule za private.

..zaidi, enzi hizo ukisoma shule za serikali maana yake ni kwamba umefaulu, wakati wenzetu waliokwenda shule za private ni wale walioshindwa ktk mitihani.

NB:

..mimi nimesoma wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, tulikuwa tunapewa text books pamoja na madaftari bure shuleni!!!
 
Last edited by a moderator:
Waziri mkuu aluyeajiwajibisha na kuachia ngazi ameamua kutoa ya moyoni mara baada ya kusema kuelekea katika uchaguzi wa 2015 ataka ilani ya CCM iseme wazi kuwa elimu ya sekondari iwe bure kumwondolea mzigo mzazi.

Ikumbukwe kuwa CDM iliitumia katika ilani yake ya uchaguzi ya meaka 2010 na ilipingwa vikali na CCM ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi ambapo hivi majuzi kauli kama hiyo ilisikika katika vukao vya ccm ikipendekeza gharama hizo zipunguzwe.

Kwa mtazamo wangu ni kweli kuwa CCM WANAZIKATAA SERA ZA CDM MDOMONI LAKINI MOYONI WANAZIKUBALI
 
sema tu Mbunge wa Monduli inatosha. Pia hilo wazo la cdm naona liliwabana koo hadi wakaona linafaa. Juzi hapa kinana kazungumzia kuhusu kupunguza au kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kujjenga. Ni nani anaongoza Tanzania?
 
Magamba ni wanafiki mbona hakupendekeza hilo alipokuwa Pm?
 
CDM bana ! Eti elimu ya sekondari bure hoja hiyo walianzisha wao, Acheni unafki wa kwanza alikua LIPUMBA,Na MKAPA alimwita profesa uchwara,lipumba alisema mtoto atasoma bure mpaka mwisho wa akili hadi chuo,lkn baada ya mwaka wakafuta karo ya shule ya msingi na kapunguza ya sekondari,sijajua we mtoa mada pengine ulikuwa mtoto.
 
Waziri mkuu aluyeajiwajibisha na kuachia ngazi ameamua kutoa ya moyoni mara baada ya kusema kuelekea katika uchaguzi wa 2015 ataka ilani ya CCM iseme wazi kuwa elimu ya sekondari iwe bure kumwondolea mzigo mzazi.

Ikumbukwe kuwa CDM iliitumia katika ilani yake ya uchaguzi ya meaka 2010 na ilipingwa vikali na CCM ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi ambapo hivi majuzi kauli kama hiyo ilisikika katika vukao vya ccm ikipendekeza gharama hizo zipunguzwe.

Kwa mtazamo wangu ni kweli kuwa CCM WANAZIKATAA SERA ZA CDM MDOMONI LAKINI MOYONI WANAZIKUBALI


Tukubali iwe bure kwa masharti yafuatayo: Watoto na wajukuu wa wanasiasa waanze kusoma katika hizo shule za bure.
 
"Serikali ina mapesa mengi sana lakini inapeleka kwenye mabarabara na kwenye kilimo, ina wezekana pesa hizo ziingizwe kwenye elimu" Edward Lowassa.
 
Ni kuhusu elimu bure hadi sekondari, asema iwe moja ya ajenda za ccm 2015

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema wakati umefika kwa sasa hapa nchini elimu ya Sekondari iwe elimu bure na kumwondolea mwananchi wa kawaida mzigo wa kubeba gharama za elimu hiyo.

Lowassa akizungumza jana mjini Babati alisema, mjadala kuhusu elimu kutolewa bure hadi sekondari haukwepeki, hivyo kuwataka wadau wa elimu kuanza sasa kujadili suala hilo na kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kulifanya hilo kuwa moja ya ajenda zake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Alisema elimu ya sekondari ikifanywa bure, itakuwa ni fursa kwa kila mtoto wa Kitanzania kuipata. Hatua ambayo itaongeza weledi na uelewa wa mambo mengi katika jamii.

"Ninasema sasa wakati umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa watoto kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne," alisisitiza Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM).

Kwa kauli hiyo, Lowassa ni kama ameunga mkono Sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao waliingia katika mgogoro na CCM kuhusu elimu kutolewa bure wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Chadema wamekuwa wakisisitiza kwamba elimu bure inawezekana hadi ngazi ya sekondari, lakini wakati wote CCM wamekuwa wakisema kuwa suala hilo haliwezekani na kwamba kauli za aina hiyo ni kuwahadaa wananchi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema, Dk Willibrod Slaa alitumia sera ya elimu bure kuanzia chekechea hadi sekondari kama kete ya kusaka ushindi, huku akisema chama chake kingetenga asilimia 35 ya bajeti kwa ajili ya kuboresha elimu na kutoa elimu bure.

Hata hivyo, aliyekuwa mgombea wa CCM na baadaye kupata ushindi, Rais Rais Jakaya Kikwete alikuwa akiwatahadharisha wapigakura kuwa kwamba ahadi ya Chadema ni hewa na kwamba hilo lisingewezekana.

Mvutano huo uliwaingiza makada wengine ambao ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye wakati huo alikuwa Meneja Kampeni wa CCM na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta na kwa upande wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo naye alijitokeza kutetea sera ya chama chake.

Katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Novemba 10, 2010 katika Kata ya Mchangimbore katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Rais Kikwete alisema "Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure" na kwamba lazima wananchi wachangie.


"Nimebahatika kukaa serikalini muda mrefu hiyo sera ya bure tulijaribu na ikatushinda na wakati huo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, tulikaa naye tukaona hilo haliwezekani tukaamua tubadilishe sasa nawashangaa wenzetu wanawadanganya eti watatoa bure."


Kwa upande wake Dk Slaa akiwa mjini Arusha katika moja ya mikutano yake alisema kwamba CCM walikuwa wakipinga sera ya elimu bure hadi sekondari kutokana na kulea ubadhirifu na kuthamini anasa kuliko maendeleo kwa wananchi.

Kauli ya Lowassa
Jana akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati, Lowassa alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuzungumzia suala hilo bila ya woga
 
siku zote tunasema cdm wanapiga ngoma ccm wanacheza.
 
Back
Top Bottom