Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Mkuu naona umeamua kutumia fikra zako na kutunga simulizi...Lowassa ni CCM hawezi kwenda popote.

Ni kweli ni CCM, lakini kwa tamaa yake ya madaraka na kwa jinsi ambavyo CDM wanajua kuwa-win wana-CCM kama hao, hakuna atakayeshangaa kuona anaibukia huko.
 
Teh teh teh, si afadhali mtei, wanaweza hata kumteua LEMA au LISSU
Kwani CCM watamteua nani tofauti na fisadi Lowassa?

Kuna tetesi kuwa mama Salma au Ridhwani huenda wakateuliwa kuwa wagombea urais wa CCM, nafikiri itakuwa poa sana!!
 
OCAMPO FOUR

Kaka nimekusoma, ila jibu hoja LAIGHWANAN apokelewe CDM?
 
CONCRETE

Kwani mtu akitoka CCM maana yake ni makapi? Kutoka chama kimoja kwenda kingine ni mambo ya kawaida tu katika siasa. Tusimchukie Lowasa eti tu kwa vile anahamia CDM au tusimchukie T. Lisu akihamia CCM maana hiyo ni haki yao ya kidemokrasia
 
Jana katika runinga Vuvuzela wetu CCM akijigamba kuwa "Sera ya Elimu" ni sera ya CCM na sio CHADEMA. Kitu ambacho hakusema ni kuwa sera ya elimu bure ilikuwa ni Sera na ilitekelezwa na "CCM ya Nyerere ya Wakulima na Wafanyakazi; na sio CCM hii ya walanguzi wa raslimali za taifa".

Ili tuweze kubaini kama "CCM hii ya walanguzi wa raslimali za taifa" inaweza kutekeleza sera ya "elimu bure au la" tutazame utekelezaji wa Sera ya elimu ya CCM na Serikali yetu ya hivi sasa ambapo Serikali inatakiwa kuzipelekea Shule za Msingi "Capitation Grant" ya Shs 10,000/= tu kwa kila mwanafunzi kwa ajli ya Vitabu,Vifaa vya kufundishia, ukarabati wa Majengo na Uchapaji wa Mitihani.

Katika Shule ya Msingi anayosoma mwanangu hapa jijini Dar yenye wanafunzi 750,mwaka 2010 ililetewa Shs 1,160,000/= tu badala ya Shs 7,500,000/= ikiwa ni aslimia 15% tu. Kushindwa kwa CCM na Serikali yetu kutekeleza kwa vitendo "Sera yetu ya Elimu ya Msingi, husababisha wazazi kurundikiwa michango isiyoisha kama vile kulipa mlinzi, kutengeneza madawati, ukarabati wa majengo, kuchapa mitihani n.k

Kama hivi sasa CCM na serikali yetu inatekeleza Sera yake ya Elimu ya Msingi kwa 15% kwa kumtumia kila mwanafunzi wa msingi Shs 1,546/= tu badala Shs 10,000/= tujipangia wenyewe na kupitishwa katika bajeti ya Wizara ya Elimu na Tawala za Mikoa. Je tutaweza vipi kutekeleza Sera ya Elimu Bure?

Kwakuwa katika bajeti kila mwaka hupitishwa Shs 10,000/= kwa kila mwanafunzi wa shule za msingi hapa nchini, CCM na Nape wanapaswa kwanza kutueleza Shs 8,454/= kwa kila mwanafunzi wa msingi zidisha kwa idadi ya wanafunzi wote wa msingi Tanzania nzima zinakwenda wapi kila mwaka? Hizi na haki za watoto wa Tanzania zitokanazo na kodi tunazolipa wananchi bial ya kujali vyama vyetu.

Kama CCM hii hii ya akina Nape, Mwingulu, Makamba wameshindwa kufuatilia haki hizi za watoto kwa takribani miaka miwili waliyokuwa madarakanii katika Sekreterieti ya CCM, wataweza vipi kutekeleza kuisimamia serikali hivi sasa kama anavyodai Nape jana katika runinga? nakubkuka miaka miwili iliyopita Nape pia alitoa kauli kama hii lakini hadi sasa hakuna kilichotokea hata ufisadi mkubwa ulipotokea na ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali kiuwatuhumu baadhi ya mawaziri Sekreterieti yao ilishindwa kabisa kuchukua hatua hadia waziri Mkuu kutishiwa kung'olewa.

CCM na viongozi wake wengi aina ya akina Nape hawajatambu kuwa watanzania wa sasa sio watanzania wa kale, bado wanapiga poyoyo na kufikiri kuwa wataweza kuwafunga kamba wananchi kama walivyofanya miaka ya nyuma. Tunawaomba muache kukichafua chama chetu kwa taarifa zisizofanyiwa utafiti na zisizo za kweli katika mazingira haya ya ushindani mkali wa kisiasa.
 
Mkuu Ritz
Makamanda hawana mgombea wanahaha kila kona usije kushangaa kusikia Mzee Mtei ndio mgombea wao 2015

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu Chama, comment kama hii inakushushia sana hadhi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Chama, comment kama hii inakushushia sana hadhi.

Mkuu Soki
Hali sio shwari mtaa wa Togo; mgombea hakuna huo ndio ukweli wenyewe; watu wameamua kama noma na iwe noma usije kushangaa kukawa na Chadema Kaskazini na Chadema ukanda wa maziwa hiyo ndiyo hali halisi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu galiya mumeo membe anakutumia vibaya sana..

Galiya akaangalie kule kwenye kura ya maoni mgombea wake anaburuzwa vibaya na mgombea aitwaye "none of them",Hapa wogombea wote wawili Membe na "none of them" kwa pamoja wanaburuzwa na EL,Hapa ndio useme Mgadafi wako atauweza mziki wa Dr Slaa!
 
Ni kweli ni CCM, lakini kwa tamaa yake ya madaraka na kwa jinsi ambavyo CDM wanajua kuwa-win wana-CCM kama hao, hakuna atakayeshangaa kuona anaibukia huko.

Hivi kwa akili yako kweli unafikiria Lowassa anaweza kuamia Chadema.
 
ENL haendi kokote zaidi ya kubaki CCM!!

Ukitaka mwana CCM "maarufu" kuhamia CDM basi usiangalie mbali zaidi ya Frederick Sumaye.......lakini yeye pia sio rahisi kwenda huko kama ataondoka peke yake, kwani kwake yeye hataweza kufanikiwa CDM bila ya kuwa na "proven" former members of CCM.
 
Mkuu Ritz
Makamanda hawana mgombea wanahaha kila kona usije kushangaa kusikia Mzee Mtei ndio mgombea wao 2015

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,
Makamanda wanatamani Lowassa awe mgombea wao sasa Dr Slaa wamemchoka.
 
Last edited by a moderator:
hilo wameshindwa hapo dar kwakuwa viongozi wote wapo hapo ndo wametoa hiyo 15% amini usiamini huku kwetu wametoa kayti ya sh 40 na 100. watoe zote hizo za nini watoto wao kawatafute kwenye shule za st. hizi zenu za kayumba zinawahusuni. hali ni mbaya chezea sisiem ww
 
Pumba tu huyu hafai Msikitini wala Kanisani,toka lini ulisikia CDM wanapokea watoa na wala rushwa tena kutoka CCM na wewe nadhani ni pandikizi ndani ya CDM.

Walowahi CDM ni watu safi tena vijana wenye uwezo wa kuleta mabadiliko tena wanachukia rushwa,siyo hao wapenda rushwa unaowapigia debe,CDM hakuna kununua uongozi CDM tena wana uchungu na nchi hii iondokane na zimwi au joka la rushwa.
 
mtoa mada haeleweki anaonyesha kuwa ana ndimi mbili, CCM kuna uhuru wa kuongea , na si vibaya kutofautiana na maazimio ya chama linalopitishwa ndo la wote kwa utekelezaji na huzuiwi kutoa mawazo yako, kama kuna uhitaji utajibiwa, na si dhambi ktk CCM kusifia kizuri cha CDM, ila ilikuwa ni dhambi kusifia kizuri cha ccm ukiwa CDM , lkn mh, ZZK amejitahidi kusimamia msimamo wa taifa kwanza chama baadaye mpaka leo na wengine wanainuka nakusifia mazuri ya ccm,wanasiasa ndani ya chama kimoja kutofautiana au kuwa na mawazo sawa ni kitu cha kawaida mbona uelezei kuwa mawazo ya MH JK na EL juu ya ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu wote wanamsimamo sawa. juu ya serikali itoe maamuzi magumu na maamuzi magumu yakatolewa huoni kuwa ni mawazo sawa.mgombea ambaye anaonekana anamuunga mkono EL akishinda basi rushwa imetumika , mh MEMBE inasemwa hamuungi mkono EL angeshindwa ingesemwa ameshindwa kwa rushwa. eti EL kashinda ujumbe wa NEC wilayani Monduli kwa kutoa rushwa mnyonge,mnyongeni haki yake mpeni.
 
Wadau, je LAIGHWANAN apokelewe CHADEMA?? capital N O! period.
 
kama lowasa akaruhusiwa kujiunga na CDM Baasi ndo mwisho wa CDM
 
Back
Top Bottom