Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Lowassa: Elimu ya bure inawezekana!

Mkuu Mtoi
Nadhani mpaka sasa hivi unajiuliza kwa nini napingana na kauli za mh. Lowassa; yeye ndiye muasisi wa shule za kata; mpango mzima ulifeli kwasababu hakukuwa na uwiano kati ya majengo na vitendea hii ikijumuisha na idaidi walimu; mh. Lowassa ni mwanasiasa ambaye upepo wake kisiasa umezimika na anajitahidi kila siku kusema vitu ambavyo havina mpangilio; au inahitilafiana na sera makini za CCM; sisi tunasema kilimo kwanza yeye kadakia elimu kwanza; yote hii ni kuwa kaishiwa kisiasa. Mkuu Mtoi sera ya elimu ya CCM haijatukataza tusipeleke vijana wetu kwenye mashule ya binafsi; mwenyekiti MBOWE amepeleka watoto wake shule ya vichekechea nasikia analipa milioni 7 hivi unategemea Chadema ikiingia madarakani MBOWE atawapeleka wanawe kwenye shule za serikali? Sijafanikiwa kimaisha najihini ili niwapeleke shule wanangu; nimekuambia kuna siku nakula muhogo usio na towezi; mkuu usiwaamini sana hao watu wana ajenda binafsi.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama.
Hongera kwa kurudi kujadili hoja maana ulianza kunipa mashaka ulipoanza kutoka nje ya mada na nduguyo Ritz.

Naomba nijibu hoja zako lakini pia nakuomba upitie Makala ya kiuchambuzi ya Dr Kitila Mkumbo niliyoweka kwenye mchango wangu uliopita.

1. Umesema EL ndiye muasisi wa shule za kata. Kama hivyo ndiyo basi kuna udhaifu mkubwa sana unao uanika kwenye sera za ccm maana nilijua ilikuwa ni sera iliyo kuwa kwenye ilani ya chama. Hii maana yake ni kwamba kiongozi yoyote ndani ya ccm akishauriana na mkewe au kuota usiku anakuja na kutekeleza aliyoota au kushauriana na mkewe! Huo ni msiba na udhaifu wa hali ya juu!
Hata hivyo ukienda mbali zaidi unaweza kujiuliza nafasi ya makamu wa raisi, raisi, baraza la mawaziri na serikali kwa ujumla kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya majengo, vitendea kazi na walimu bora wenye sifa, hiyo ilikuwaje ili kuboresha wazo la muasisi?! kama serikali nzima iliaacha wazo la muasisi bila kuriboresha maana yake ni kwamba udhaifu ni mkubwa sana kuliko tunavyofikiri kwenye hiyo serikali husika.

2. Umeongelea upepo wa El kuzimika.
Upepo wa El kuzimika au kuwaka sio hoja ya msingi! Swala hapa ni mashiko kwenye hoja zake bila kuangalia kuwa nyota yake ina waka au imezimika. Mfano anaposema kuwa haamini katika sera ya kilimo kwanza kwangu naweza kusema kuwa yuko sahihi maana elimu ndio mama wa taaluma zote na dira ya shughuli zote za uzalishaji, hata wakulima pia wanahitaji elimu bora ili wafanye kilimo bora na chenye ufanisi na tija. Kama hivyo ndivyo, basi elimu bora ni muhimu sana ili kukipa manufaa kilimo. Na kwa mujibu wa takwimu za kitafiti kwenye uchambuzi wa mwanazuoni Kitila Mkumbo elimu bora naya bure inawezekana na hii ndiyo ilikuwa sera ya chadema, basi jamii za wakulima na wafugaji wanatakiwa kufaidi hili kama jinsi watakavyo faidi jamii za watu wengine ili kuleta tija na kuongeza uzalendo kwa taifa.

3. Sera ya ccm haija kukataza kupeleka watoto wako shule za private. Sawa kabisa! Lakini je mnapeleka watoto wenu shule za private kufuata nini na huko shule za Kayumba (Kata) mmekimbia nini na kwa nini mkimbie?! Hili ndilo la msingi, kula kwako muhogo au ndondo ili watoto wasome ni hisani yako maana ungeweza hata kuamua kufunga swaum isiyo na kikomo kwa nuizi la wanao kusoma. Hahaha.

4. Umepoteza uhalali wa kumjadili Mbowe na mimi pia napoteza uhalali huo! Kwa nini?! Umesema "nasikia analipa milioni 7 hivi unategemea Chadema ikiingia madarakani MBOWE atawapeleka wanawe kwenye shule za serikali?" Msisitizo wangu wa mimi na wewe kukosa uhalali wa kumjadili Mbowe ni hapo kwenye "NASIKIA" tusijadili kusikia bila kuwa na uhakika! Weka data ili tuepuke kujadili maneno ya mtaani, wenye tabia ya kujadili maneno ya kusikia ni watu wasio kuwa makini na huwa wana maneno laini kama maini. (Wengine huwaita wambeya).

5. Umesema "usiwaamini sana hao" hao ni kina nani unao sema wana ajenda ya siri? Na siri hiyo ni ipi maana tayari bila shaka umeshaifahamu kwa kuwa ile sifa/dhana ya usiri haipo tena. Karibu tuendelee mkuu. Majibu yako yatanisadia sana kunijenga hasa kama utaendelea kugusa masuala (issues) na si vioja kama alivyo anza na kuendeleza kaka yangu Ritz.

Kila jema na lenye kheri lisikuponyoke chama.
 
Last edited by a moderator:
I am not here to take sides but nia na madhumuni ya bandiko hili ni kuona kama kauli ya mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu ilikua na malengo ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Hpana shaka kabisa kwamba Ni ndoto ya any reasonable man kuona nchi ikiwa na maji, umeme na huduma bora.

Na kwa kuzingatia hayo ndugu yetu alikuja na kauli yake kugusia hilo, kauli yenyewe ilikuwa kama ifuatavyo nanukuu " Ndugu zangu, naanza safari ya ndoto zangu, ambayo itatimiza ndoto za watanzania kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika"

Kwa mtazamo wangu sentensi hiyo hapo juu, haijaweka wazi nia ya mtoa tamko kama inavyotafsiriwa na wengi.

Sijawahi kuona wala kusikia Ndugu huyu anayetuhumiwa akitamka wazi kuwa ana nia ya kugombea Urais.

Kutoa michango ni moja wapo ya huduma anazozifanya kwa nafasi yake ya uongozi, jambo ambalo kila mtu analifanya.

Tatizo linakuja katika matumizi ya media pale anapohusika katika shughuli hizo za kijamii, hii ni kutokana na nafasi aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma kama waziri mkuu, muunganiko wa media na statement aliyoitoa imetoa picha na tafsiri inayokinzana na lengo halisi la mtoa tamko.

Nilivyoielewa kauli yake sina shaka kuwa shughuli za sasa ni kama huduma tu za kijamii kama wafanyavyo watanzania wengine kwa wakati wao wanaoona unafaa.

Sidhani kama kuna muda muafaka wa mtu kufanya jambo kama akiona muda huo anapolifanya ndio sahihi kwake, kuna uwezekano wa mgongano wa kimaslahi lakini kusiwe na madhara ya lengo na dhumuni la mtu kwa wakati huo.

Nawasilisha.
 
tatzo nikwamba ccm wamesha ona sasa lowassa hakamatiki tena,wanachofnya ni kujaribu kumpunguza speed, ila sahv amewaacha mbali mno
 
tatzo nikwamba ccm wamesha ona sasa lowassa hakamatiki tena,wanachofnya ni kujaribu kumpunguza speed, ila sahv amewaacha mbali mno,ila nimshaur mangula,yaliyomtokea kipindi kile yasisije yakamtokea tena
 
" Ndugu zangu, naanza safari ya ndoto zangu, ambayo itatimiza ndoto za watanzania kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika"

.
kwa mfumo uliopo sasa wa uongozi wa nchi hii chini ya CCM huwezi kutekeleza kauli hii kabisa, tuwe wakweli wakati mwingine.
 
Lowassa na zuma wana undugu..ni magwiji wa mipango na technicalities...sasa huyu mkazi wa msoga kakutupuka tu anaanza kurusha mate bila hata kuelewa
 
" Ndugu zangu, naanza safari ya ndoto zangu, ambayo itatimiza ndoto za watanzania kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika"

Sijawahi kuona wala kusikia Ndugu huyu anayetuhumiwa akitamka wazi kuwa ana nia ya kugombea Urais.

Bila kumun'gunya maneno jamaa EL anautaka urais ,period..............................
 
Naona Nyumbu wa Lumumba mshaanza kugawanyika na kutawanyika.
CJADEMA tuta wa swagilia mbali mtoni mkaliwe na Mamba vizuri
 
Hili suala jepesi sana kwa magwiji wa siasa kama jk na kinana jinsi litakavyotatuliwa wala hamtakaa muamini jk kastaarabika sana kwenye mambo haya.
 
endeleeni kuwa vipofu kwa rushwa za lowasa, kila anachozungumza mnaona ni kama malaika fulani hivi
 
Uzuri wa ccm mambo yao yote huisha kwa vikao na majadiliano hata hili tayari majibu yapo.
 
kwa mfumo uliopo sasa wa uongozi wa nchi hii chini ya CCM huwezi kutekeleza kauli hii kabisa, tuwe wakweli wakati mwingine.

kipimo cha utendaji hakipo katika hisia bali uhalisia, uhalisia unaonyesha shughuli nyingi za kimaendeleo zilizofanywa, zinazoanywa na zitakazofanywa na CCM, kiwango cha ubora ni kadri ya yule akipimae, vipimo hutokana na hulka na utashi wa watu mbali mbali
 
Naona Nyumbu wa Lumumba mshaanza kugawanyika na kutawanyika.
CJADEMA tuta wa swagilia mbali mtoni mkaliwe na Mamba vizuri

mgawanyiko uku pekee katika uchanga, ila katika ukomavu kila jambo ni changamoti ya kuwa bora zaidi, CCM ni kama mvinyo , jinsi muda unavyodizi kwenda ndivyo inavyozidi kuwa bora zaidi, hii ni kama spice ya kuboresha muungano ndani ya chama
 
Ni rahisi sana kufanikisha.Tufilisi mafisadi wote.Halafu tuzibe mianya yote ya wizi wa nyara na fedha za serikali,ikiwa pamoja na madini.Pia tuzuie matumizi mabaya ya fedha za serikali ikiwa pamoja na kodi mbalimbali.Pesa iko kibao tu,wala hatuhitaji wezi wa nchi za magharibi.

we usifnye kaZ,subir sna chadema iingie ikulu ndio wakupe hela
 
CCM itaimarika kama jiwe lakini imechelewa kwa sasa yamkini CHADEMA kikaikwaa ikulu lakini tukashudia maisha magumu kuliko wakati wowote kwa sababu CHADEMA watukutana na hali ngumu ya kuendesha serikali ukakuta CCM inatumia mwanya huo kurudi madarakani kwa sababu ya CHADEMA kushindwa kuweka mambo sawa huku CCM kikiwa chama kikuu cha upinzani
 
Back
Top Bottom