Mtoi,
I hate to say this, kwenye watu wanaoongelewa kuuwania uraisi, huyu bwana EL, licha ya wizi wake na ulevi wake wa madaraka akiwa nayo, ndio pekee ameonyesha kuwa na mawazo yenye meno ambayo nchi yetu inahitaji. Tatizo ni vigumu kumuamini kutokana na historia yake mbovu anapopewa madaraka. Tufanyeje sasa Watanzania?
Channel ten ilipaswa kumhoji EL ilikuwaje 2010 magamba walidhamini matangazo yakupotosha wakati wa campaign za Dr. Slaa kuwa elimu bure haiwezekani? Tena kupitia channel ten hiyo iyo?
Mkuu chama.
Mchango wako una mashiko sana lakini kwa heshima na taadhima naomba nikuambie kuwa tukiwa na dhamira ya dhati na kuwa na viongozi wenye kutembea juu ya kauli zao huku wakihakikisha kuwa kila senti kwenye raslimali zetu inatumika ipasavyo bila upotevu au kudondokea kwenye matundu ya wajanja wachache, tunaweza kabisa kuwa na mashule bora yenye vifaa bora na walimu bora na elimu bora ya bure inayogharimiwa na serikali husika.
Kwa sasa hata mfumo wenyewe wa kukusanya kodi una mapungufu mengi na mapato mengi yanapotea bure. Ni Tanzania pekee ambayo mfanyakazi wa serikali wakati mwingine analipa kodi kubwa kuliko mfanya biashara anayeingiza mamilioni ya shilingi kwa siku au kwa mwezi.
Mkuu chama kwa swala la kusomesha serikali haija jitwisha mzigo! Hilo ni swala la kikatiba na ni jukumu lake la kimsingi kusomesha maana ina wakamua wananchi wake kodi kwenye huduma na biadhaa mbalimbali. Sikutegemea uionee huruma serikali kwenye hili maana ni jukumu lake la msingi tena bila visingizio.
Kaka chama! Leo umekuwa objective kutofautiana na wana ccm wenzako lakini pia na sera za ccm maana sikujua kuwa kwa mapenzi na mahaba yako unaweza kusomesha wanao private huku ukiacha shule zilizopigiwa chepuo la kufa mtu na chama chako.
Nimegundua kuwa huamini katika baadhi ya mambo ndani ya ccm! Sitaki kusema unaamini kwenye sera za chama gani lakini wewe ndio una majibu ya kina.
Kila jema na lenye kheri lisikuponyoke wangu.
Akiongea kupitia kituo cha channel 10 kwenye taarifa ya habari ya saa 1 leo 18 Nov,2012 Mheshimiwa Lowassa amesema serikali inaweza kugharamia elimu ya msingi na sekondari kwa wananchi wake kuwa bure, na elimu ya sekondari ikafanywa kuwa ya lazima na ya kiwango (quality). Ili kuwafanya vijana kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira.
Kauli hii ni muendelezo wa wana CCM kuendelea kukubali sera kadhaa kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010, juzi Kinana alisema serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawezi kujenge nyumba bora kwa ajili ya makazi.
Mkuu Mtoi
Suala la elimu bado ni mzigo kwa serikali; umefika wakati watanzania inabidi ujiulize umeifanyia nini serikali na sio serikali imekufanyia nini; lengo sio serikali kuutua mzigo huo mojamoja la hasha na sisi wananchi wenye uwezo tuchangie angalau wale wasio na uwezo kabisa wapelekwe shule; Serikali ingejizatiti kwenye elimu ya msingi na sekondari hizo na zitolewe bure au uchangiaji kidogo kama tunavyofanya; elimu za vyuo bodi ya mikopo iboreshwe ili kuhahakisha kila anayechukua mkopo anarejesha; hivi sasa wapo watu wengi wamechukua mikopo wanauwezo wa kurejesha lakini hawalipi hilo ndilo linaloiongezea serikali mzigo; tunapoongelea rasimali za nchi hata hii mikopo ni sehemu ya rasilimali zetu; ruzuku kwa vyama vya siasa ni moja ya matumizi mabaya ya rasimali zetu; mkuu unapoongelea yapo mambo mengi unayafumbia macho kwasababu za kisiasa; matatizo ya ukusanyaji ni matokeo ya kuwa na wafanyakazi ambao sio waaminifu, wapo wanasiasa utawakuta kwenye majukwaa wakikemea ukusanyaji mbovu wa kodi; kumbe wao ndio vinara wa kwenda TRA kupiga deal za kukwepa kulipa kodi; nina uhakika katika hili wapo wanachadema wengi wanajihusisha na hujuma hizi
Mkuu Mtoi kupeleka watoto private najima siku nyingine nakula muhogo usio na kitoweo yote nawatafutia watoto urithi;
Inshallah kwa dua zako nawe Mola akupe kila lilo na heri na wewe.
Chama
Gongo la mboto DSM
Akiongea kupitia kituo cha channel 10 kwenye taarifa ya habari ya saa 1 leo 18 Nov,2012 Mheshimiwa Lowassa amesema serikali inaweza kugharamia elimu ya msingi na sekondari kwa wananchi wake kuwa bure, na elimu ya sekondari ikafanywa kuwa ya lazima na ya kiwango (quality). Ili kuwafanya vijana kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira.
Kauli hii ni muendelezo wa wana CCM kuendelea kukubali sera kadhaa kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010, juzi Kinana alisema serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawezi kujenge nyumba bora kwa ajili ya makazi.
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!
Akiongea kupitia kituo cha channel 10 kwenye taarifa ya habari ya saa 1 leo 18 Nov,2012 Mheshimiwa Lowassa amesema serikali inaweza kugharamia elimu ya msingi na sekondari kwa wananchi wake kuwa bure, na elimu ya sekondari ikafanywa kuwa ya lazima na ya kiwango (quality). Ili kuwafanya vijana kushindana kikamilifu kwenye soko la ajira. Kauli hii ni muendelezo wa wana CCM kuendelea kukubali sera kadhaa kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010, juzi Kinana alisema serikali iondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawezi kujenge nyumba bora kwa ajili ya makazi.